Sunday, April 29, 2012

HABARI NJEMA KWA WATU WOTE WENYE MAPENZI MEMA KWA MUNGU NA WENZAO/JUMAPILI YA LEO

Ni Jambo la kumshukuru Mungu wetu,kwa kutufikisha Jumapili ya leo,kwakuwa hatujampa kitu chochote ili atupendelee kuendele kuvuta pumzi ya uhaiwetu,zaidi ya kumuudhi na kumkasirisha kwa matendo maovu yanayotendwa na binadamu duniani kote kila dakika.Lakini amekuwa mpole na kutusameha,kwa kuwa hatujui tulitendalo.Nawatakieni Jumapili yenye faraja na furaha ya kweli ya maisha  yetu hapa duniani ambapo ni wapita njia tu.

Wednesday, April 25, 2012

ZOEZI LA KUSAFIRISHA MAHINDI KUTOKA GHALA YA CHAKULA LA TAIFA RUHUWIKO SONGEA BADO SANA , INGEKUWA NI USAFIRI WA R ELI LINGEKUWA LIMAKAMILIAKA


 Mpiga picha wetu leo ameyakuta maroli yakiwa tupu yakielekea kwenye Ghala hilo la chakula la Ruhuwiko katika Manispaa ya Songea.Lakini alipojaribu kumuuliza mmoja wa madereva wa malori hayo amesema,kazi iliyoko ni kubwa mmno,kwani foleni ya malori ambayo yanasubiri kupakia ni mengi.
Mahindi ni mengi mmno maana mengine yako Mpitimbi,Litisha  yalikohifadhiwa wakati ya hapa Somgea ni bado kabisa
Hilo ni lori lililojaza mzigo liko njia moja likielekea Dar es Salaam likitokea Mpitimbi

LEO NI SIKU YA MARELIA, SIKU YA KUMTAFAKARI MDUDU MDOGO SANA LAKINI MADHARA YAKE NI MAKUBWA SANA KWA MAISHA YA BUNADAMU,NAYE SI MWINGINE NI MBU.

Siku ya mareli ni siku iliyoandaliwa kwa kuyaangamiza mazalia ya mbu,madibwi ya maji,vichaka vya majani,kwa kumwagia dawa ,kupulizia dawa kwenye majumba.Lakini kubwa zaidi ni kutumia chandarua kilichotiwa dawa.
  Kwa taarifa ya Sekta ya afya nchini ni kwamba idadi ya vifo vya watoto kutokana na marelia vimepungua.
  Mareli yanawashambulia akina mama wajawazito na watoto wachanga.Lakini Serikali kwa kuthamini wananchi wake,imeto vyandarua vyenye dawa kwa mama mjamzito namwenye mtoto mchanga ili kuwakinga na mbu wanaosambaza vimelea vyenye marelia.

Sunday, April 22, 2012

NAWATAKIENI AMANI WASOMAJI WA BLOG HII KOKOTE WALIKO,NA TUZIDI KUMUOMBA MUNGU ATUJALIE AMANI.

Tuzidi kumuomba Mungu atuzidishie amani,upendo Duniani,kwa watu waliyokata tamaa ya muishia waliyokata tamaa kutokana na hali ya maisha kuwawia ugumu,kwa kukosa ,huduma muhimu,elimu,afya,chakula, mavazi na mambo kadha wa kadha.Mungu utuhurumie viumbe wako tuliyo wadhahifu,utupe nguvu ya kushinda majaribu yote ya dunia hii.

SIKU MAKA YA JUMAPILI YA LEO YESU KRISTO ALIWATOKEA MITUME WALIMO JIFUNGIA KWA HOFU, AKAWAAMMBIA AMANI IWE KWENU.

Yesu Kristo alipowaambia wafuasi wake amani na iwe nanyi,ile inamaana yeye mwenyewe ana amani na wanadamu ambao amekufa kwa ajili ya dhambi na udhaifu wa kibinadamu walio kuwa nao.Hivyo na waumini wa Roman Catholic wakati wa matoleo Padre husema kwa waumini wake kuwa mtakiane amani.Na waumini hupeana mikono kwa kutakiana amani. Je waumini wote wana amani mioyoni mwao?
  Mchungaji mmoja katika mahubiri yake alisema,unapo mtakia mwenzako amani ,wewe mwenyewe uwe na amani moyoni mwako,vinginevyo unamtakia mwenzako hasira.kwa kuwa amani imetoweka miongoni mwa jamii,ukweli na uwazi haupo,dunia imajaa vita,dhuluma,unyanyasaji.Amani hakuna,watu wanakimbia nchi zao wanaisha uhamishoni,na kuwa wakimbizi,tatizo hakuna amani.

Tuesday, April 17, 2012

RAIS WA VICOBA TANZANIA AZINDUA KAMPENI YA VICOBA JIJINI DAR ES SALAAM MGENI RASMI DKT REGINALD MENGI ACHANGIA SHILINGI MILIONI MIAMOJA

Rais wa VICOBA Mhe.Devota Likokola amesema Dkt Reginald Mengi ni Mtanzania wa pekee mwenye kujali watu  maskini,na mpiganaji mkuu wa umaskini Tanzania,anatumia utajiri wake kwa ajili ya kuinua maisha wa watu wenye kipato cha chini.Alisema Dkt Mengi amechangia VICOBA fedha za kitanzania Tshs.bilioni moja na milioni miamoja na ishirini,kwa ajili ya kuendeleza watu maskini,watu wenye mashaka ya maisha.
Alisema hayo kwenye uzinduzi wa Kampeni ya VICOBA Jijini Dar es Salaam, ambapo Mengi alikuwa mgeni rasmi,uzinduzi uliyoambatana na kupewa vyeti walimu 30 wa VICOBA ambao watakwenda kuhamasisha VICOBA kwenye maeneo yao.
 Dkt Reginald Mengi alisema vita vya kupigana na umasikini si vya mtu mmoja ni vya kila mmoja.Na mwenye kujua uchukungu wa umaskini ni maskini mwenyewe,yeye anaujua umaskini,hivyo ni juu yake kujitoa kwenye umaskini huo.na watu wenye vipato wao ndiyo wa kuwasaidia watokane na  umaskini wa kipato.Amewaomba matajiri kutoa sehemu yao ya utajiri kusaidia watu maskini ili na wao wawe na unafuu wa maisha.Katika uzinduzi huo Dkt Mengi amechangi shilingi milioni miamoja kwa ajili ya walimu wa VICOBA waliyopewa vyeti kwenda kufundisha vikundi vya uzalishaji mali kupitia VICOBA.
 Mwenyekiti wa VICOBA Bibi Monica Mbega alisema kuwa kazi ya wara
tibu wa VICOBA ni ya kujitolea siyo ya kipato ,aidha alisema VICOBA vimeinua sana maisha ya watu wenye kipato cha chini.Pia amempongea Dkt Mengi kwa moyo wake wa kujitoa katika uchangia wa kipato chake kwa ajili ya maskini nchini.Na Rais wa VICOBA kuwa na moyo wa kuanzisha ba kuendeleza VICOBA kwa ajili ya kuinua maisha ya wa - Tanzania wenye kipato cha chini,ikiwa ni jitihada za kupambana na vita vya umaskini.

Baadhi ya wana - VICOBA na walimu waliyo tunukiwa vyeti vya mafunzo ya kuendesha VICOBA katika maeneo yao

BREAKING NEWS ! ! WABUNGE 302 WA BUNGE LA JAM HURI YA TANZANIA LEO WAMEPIGA KURA KUWACHAGUA WABUNGE WATAKAO WAKILISHA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI

Nafasi ya wanawake ni mbili,kambi ya upinzani nao wapo na fasi ya Zanzibar wanaume na wanawake bila ubaguzi. wapatikane wabunge watakaoingia kwenye mjengo wa Bunge la Afrika Mashariki 9.Saa moja usiku tutapata majina kamili ya wabunge waliyochaguliwa.Katika uchaguzi huo uliyofanyika leo baada ya kujieleza na kisha kuomba kura kwa waheshimiwa wabunge wenzao.

Tuesday, April 10, 2012

WAZIRI MKUU KAZINDUA CHUO CHA VETA KONGOWE KIBAHA PWANI

 Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda akiongea na wananchi,uongozi wilaya na mkoa pamoja na wanafunzi kabla ya kuzindua Chuo cha VETA Kongowe Kibaha Pwani.
 Hicho ni chuo cha VETA kilichoko Kongowe aliye mbele ya jengo hilo ni mwandishi wa habari wa ITV
 Mwenyekiti wa Bodi ya VETA akimshukuru mgeni rasmi,na kusema atatekeleza yote yaliyo semwa na Waziri Mkuu.
Baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho cha VETA Kongowe.


WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mizengo Peter Pinda leo amezindua Chuo Cha VETA Kongowe Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani ambacho kina wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa fani mbalimbali.
Mhe.Pinda alisema chuo hicho ni muhimu sana kwa vijana wanaomaliza elimu ya msingi na sekondari.kwa hiyo wanafunzi wanaomaliza elimu katika ngazi hizo mkoani Pwani wapewe nafasi ya kwanza ndipo wapatiwe wa kutoka mikoa ya nje nafasi kama zita kuwepo.
Aidha Pinda ameipongeza serikali ya Korea Kusini kwa kutoa fedha na vifaa katika ujenzi wa chuo hicho,  Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi  na pia uongozi wa Bodi ya VETA  kwa jitihada zao za kuendesha vyuo hivyo nchini
Mhe. Pinda aliwaambia wanafunzi wa chuo hicho wakitunze,wasianze kupiga mawe kukiwa na maatizo na kama yakitokea waende kuomba ushauri kwenye uongozi wa wilaya,ikishindwa Mkoa na hata  kwa Mbunge wao.

KANUMBA AZIKWA MAKABURI YA KINONDONI ,WENGINE WAZIRAI NA UMATI WASHINDWA KUAGA MWILI WAKE KUTOKANA NA ENEO LA KUAGA MWILI KUWA DOGO

 Mwili wa Marehemu Kanumba ukisindikizwa na umati wa watu kuelekea makaburi ya kinondoni Jijini Dar es Salaam kwa mazishi,Waliwahi kuaga mwili wa marehemu ni viongozi wa Kitaifa tu wananchi wengine hawakupata nafasi ya kuuaga mwili.ambapo baadhi ya familia waliaga Katika makaburi ya Kinondoni.
 Baba wa Marehemu kanumba Bw.Charles Kanumba.
 Mama wa Kanumba
 Marehemu kanumba
 Mwili wa marehemu kanumba ukiagwa
 Mmoja wa wacheza filamu na Marehemu Kanumba wakimnyamazishi wakati akihojiwa.
 Mwenyekiti wa kamati ya mazishi Bwana Gabriel Mtitu akielezea taratibu za uagaji wa mwili na mazishi Jijini Dar es Salaam leo
Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Mhe.Dkt Emannuel Nchimbi alisema kazi ya usanii si rahisi,lakini marehemu Kanumba waliweza kufanya kazi hiyo hadi kifo chake ambapo aliandaa Filamu 40.Aidha alisema serikali imetoa ubani shilingi milioni 10.

Monday, April 9, 2012

MOUNT KILIMANJARO TEND TO LOST IT’S ICE SLOWLY

Now my friend  you have any comment on the photo of mount Kilimanjaro ( By Christian Sikapundwa ).And that is the ice  remain on the peak ,I am talking about.What do you respect on the year  2025 ?.


Mount Kilimanjaro in Tanzania is the tallest mountain  in Africa is now going to lost it’s ice slowly, there for the government should do something immediately in order to stop the disappearance of ice, which attract more than 20,000 tourists a year.
     The smelting of  the ice field will affect drinking water supply, agriculture and  hydroelectric production ,also more than one million villagers live at the foot of the mountain and depend on it’s spring for irrigation and other domestic uses.
    The melting of ice is a real threat and the government should take action to the honey collectors, farmers used to clear land by burning forest which affect thousands of hectares natural forest of the mountain to be destroyed by fire.
     This is my observations when I was in Kilimanjaro last year for specially duty  for one week. Do you have any comment on that ?   and take a look on a photo of mount Kilimanjaro


Sunday, April 8, 2012

KIKWETE KWENDA KUTIA SAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO KWA MAREHEMU MAHUNDI NA STIVE KANUMBA LEO JIJINI DAR ES SALAAM

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete leo ametia saini kwa familia ya marehemu Mahundi na Kanumba.
Aidha Rais amesema kuwa Kanumba alikuwa ameanza kuchipukia na kufahamika kwa kazi zake nzuri katika nchi za jirani za Kongo,Kenya na nyingine,lakini kazi ya Mungu haizuiliki,alikwisha zungumza naye akiwa na wasanii wenzake Ikulu,na aliwa ahidi kuwasaidia kwa fedha na vifaa.

 Rais akisalimiana na mmoja ya Mtoto katika familia ya Marehemu Mahundi Jijini Dar es salaam leo alipokwenda kutoa pole kwa wafiwa.
i
 Huyo ni MMoja kati ya wacheza film wa Nigeria ambao walifika Tanzania wakacheza na Marehemu Kanumba katika mchezo wa ' My Sister'
Marehemu Kanumba msanii aliyeanza kung'a Tanzania na nchi yenye magwiji wa kucheza film ya Nigeria,lakini Maskini Kanumba Rafiki 'mkia wa fisi inama ukufilisi' sasa 'Kanumba the great has no longer in this World because of Love' Uktakumbukwa daima kutokana na kazi zako.Mungu ailaze roho ya Marehemu Kanumba peponi Aman.

Malori yameanza kupita katika barabara ya Newala Mtwara baada ya kufungwa kwa magogo na wananchi wenye hasira ya kutokulipwa malipo yao ya korosho Tarafa ya Nanyamba

 Barabara ya Newala kwenda Mtwara ilikuwa imefungwa kwa magogo makubwa na wananchi ,wakulima wanaodai malipo ya pili ya zao la korosho Nanyamba mkoani Mtwara.Leo imefunguliwa baada ya uongozi wa wilaya kwenda kuzungumza na wakulima wa zao hilo na kufikia mwafaka wa kutoa magogo hayo barabarani , magari yameanza kupita.
Hao ni baadhi ya wakulima ambao wanalalamikia uongozi wa wilaya kwa kuchalewesha malipo ya pili ya zao la korosho,ambapo madereva wa malori hayo nao wanasema wawo kufungiwa barabara ni kuwakosea haki maana wao hawahusiki na malipo hayo.

BLOG YA KUSINI INAUNGANA NA WATANZANIA WENGINE AMBAO WAMEGUSWA NA KIFO CHA MSANII MAARUFU NCHINI MAREHEMU KANUMBA

Ni pengo kubwa ambalo si rahisi kusimulia kwakuwa usanii ni 'talent' ya mtu aliyepewa na Muumba wake,alivyokuwa akifanya Kanumba siyo rahisi kufanya mwengine ingawa vitafanana.
Aidha tunatoa pole kwa wazazi wake ambao wamepata mshtuko kwani kijana wao hakuugua,lakini yote ni ya Mungu kazi yake mara zote haina makaosa,ni pamoja na wasanii wenzake wa ndani na nje ya nchi.
Roho ya marehemu Kanumba Mungu aiweke mahali pema peponi, Amin.

Saturday, April 7, 2012

NAWATAKIA PASAKA NJEMA,WAUMINI WA MANISPAA YA SONGEA WANAUNGANA NA WAUMINI WENZAO DUNIANI KATIKA MKESHA WA PASAKA

Leo duniani waumini wanamkesha wa Pasaka,nawatakia sikukuu njema,iwe yenye amani na upendo kwa wanadamu woteambao wamekata tamaa ya maisha,ambapo wanakabiliwa na changamoto za maisha lukuki,zikiwemo njaa,vita vya wenyewe kwa wenyewe,unyanyasaji wa kijinsia na mambo kadhaa yanayomkabili,hivyo tumuombe kristu mfufuka ,atuepushe na shida zote za dunia hii.

RIS JAKAYA KIKWETE JANA ATANGAZA TUME ITAKAYOSHUGHULIKIWA MASUALA YA KATIBA 15 TOKA TANZANIA BARA NA 15 TANZANIA VISIWANI

 Rais Kikwete alisema kila mmoja mwenye maoni yake kuhusu kuboresha Katiba ionane na kamati hiyo,kamati ambayo inawakilisha wananchi wote ,ambayo ina wajumbe kutoka Tanzania Bara 15 na Tanzania Visiwani 15.Alisema haikuwa rahisi namna ya kuwapata lakini busara imetumika wamepatikana.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akisoma majina ya wajumbe waliyoteuliwa kwenye Tume hiyo Jijini Dar es Salaam jana.

MANISPAA YA SONGEA YABORESHA BARABARA ZAKE WAKIANZIA NA MITARO NA MAKARAVATI

 Kamera yetu iliwanasa wafanyakazi wa utengenezaji wa barabara za manispaa ya Songea wakiwa wakichimba barabara iendayo polisi na majimaji kwa ajili ya kuweka karavati,eneo ambalo ni korofi hasa nyakati za mvua.
Upande wa pili ni mitaro iliyo kandokando ya maduka ambayo inabomolewa ili ijengwe upya,ili maji ya mvua yeweze kupitisha uchafu na vitu vingine ambavyo husombwa na maji ya mvua yakiwa mengi.

WEMBEMBE WA DARAJA LA MATARAWE LA SABABISHA GARI DOGO KUJERUHI OMBAOMBA MANISPAA YA SONGEA HIVI KARIBUNI

 Gari hilo lenye namba ya usajili T.699 AFM  mwenye mali hakujulikana baada ya dereva aliyekuwa akiendesha kukimbia baada ya  kusababisha ajali hiyo.Gari hilo lilikuwa limebeba mbao,alipoteremka mlima mbao zilielemea upande mmoja na kumshinda na kuelekea aliko kaa mwombaji huyo, ni mtu mzima ilikuwa ni kawaida yake kuomba eneo hiyo lanye hatari,aligongwa na kutupwa kwenye mtaro ,na alikimbizwa Hospitali ya mkoa ya Songea kwa matibabu.
Askari wa Uasama barabarani  Mkoani Ruruma akionyesha namba ya usajili ya gari hilo ambayo ilikuwa mbele ya gari na nyuma hakukuwa na namba yoyote,hi ni hatari kwa wenye kumiliki magari,pia kwa waendesha magari hayo.

Sunday, April 1, 2012

LEO NDIYO LEO KINYANG'ANYIRO CHA UDIWANI KATA YA LIZABONI MANISPAA YA SONGEA

Watu wanasubiri kusikia nani kwa Diwani wa Kata hiyo ya Lizaboni Manispaa ya Songea Ruvuma,kufuatia aliyekuwa Diwani wa Kata hiyo Ally Manya  ( CCM ) kufariki dunia mwaka uliyo pita.Ni vyama viwili vilivyoingia ulingoni kwa hiyo CCM au CHADEMA tunasubiri kusikia.

USAFIRISHAJI WA MABINDI BADO KAZI NZITO KUTOKA RUVUMA KWENDA NJE YA MKOA HUO

Hilo ni moja ya lori lililojaza mzigo wa magunia ya mahidi kutoka Ghala la chakula la Taifa Ruhuwiko Manispaa ya Songea.Lakini bado kuna foleni ndefu kwelikweli ya malori yakisubili kujaza mzigo,kazi bado ni nzito ya kuyamaliza mahindi hayo kwenye ghala.

NAWATAKIA JUMAPILI NJEMA YA MATAWI WADU WANGU WA BLOG HII

Pia na maandalizi mema ya Pasaka,Tuombe amani na utulivu siku hiyo.

KIJANA THADEO PETER MPELASOKA WA MINZIRO BUKOBA SASA SONGEA JANA KAZINDUA KAMATI YAKE YA KUPOKEA BAADA YA KUFUNGA CINGU ZA MAISHA KWAO TAREHE 29/6/2012

 Bwana Harusi mtarajiwa Bw.Thadeo Peter Mpelasoka akiwa katika ukumbi wa USHIRIKA wawazi na kamati yake aliyoiunda kwa ajili ya mapokezi yeye na Mpendwa wake au Mrs Pelasoka kwa lengo la makaribisho na utambulisho.
 Familia ya marehemu Mzee Peter Segawa Mpelesoka wa Minziro Bukoba wamezindua kikao cha kwanza cha maandalizi ya Harusi ya kijana wao Thadeo Mpelasoka kama anavyopendeza hapo kwenye picha anatarajia kufunga ndoa tarehe 29/6/2012 huko Bukoba.
 Mmoja ya wanakamati akichangia hoja namna ya kuboresha sherehe hizo siku hiyo,Hapo juu mwenye miwani ndiye aliyechaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati hiyo hapo jana.

 Hiyo ni meza ya upande wa wazazi wa Bw.Mpelasoka .
Hao nao ni kati ya wanakamati waliyo alikwa kufika kumuunga mkono Bw.Thadeo Mpelasoka wengine hawapo kwenye picha.