Monday, January 14, 2013

WAKINA MAMA WA UWT MKOA WA RUVUMA WAMPONGEZA MHE. TEREZYA HUVISA LUOGA KWA KUPELEKA VIFAA TIBA KATIKA HOSPITALI YA MKOA SONGEA NA WILAYA

 Baadhi ya kina mama wa UWT mkoa wakiongea na Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais ( Mazingira ) Mhe.Terezya Huvisa Luoga picha ya chini wa kwanza kushoto na wapili ni Mwenye kiti wa UWT mkoa wa Ruvuma Bibi Kuluthum Mhagama,katika ukumbi wa CCM mkoa.
Akina mama hao wanampongeza Mhe.Terezya Huvisa Luoga kwa moyo wake wakuwaonea huruma wananchi wanateseka kwa magonjwa mbalimbali katika mkoa wake,akaweka nyuma ubinafsi akajala maisha wa watu.
Menyekiti wa UWT Mkoa Bibi Kuluthumu Mhagama alisema ,ni moyo wa pekee ambao ameuonyesha kwa wanaruvuma na Taifa kwa ujumla.kwani angeweza kuanzisha hospitali yake ambapo akanufaika na vifaa tiba vivyo.Bibi Mhagama ametoa wito kwatanzania wengine ambao wamejaliwa kuwa na marafiki katika mashirika yasiyo ya kiserikali kutafuta misaada kwa manufaa ya maeneo yao hata na taifa kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment