Monday, January 28, 2013

UELEWA MDOGO KWA WAKAZI WA MTWARA KUHUSU GESI KUMEZUSHA TAFLANI MKOANI HUMO

UELEWA mdogo kwa baazi ya wananchi wa Mtwara kuhusu gesi inayopatikana mkoani humo kumezusha vurugu na kusababisha hasara iliyowakumba wananchi wasiyo na hatia.
Naibu Waziri wa Nishati na madini Mhe.George Simbachawene,amesema wananchi wa mkoa huo lazima wajiandae na mafanikio ya gesi hiyo,Ingawa si wote watapata ajira kutokana na bomba la kusafirisha gesi kwenda Dar es Salaam,lakini wanao uwezo wa kujiajiri wenyewe,kwa kufanya biashara za bidhaa ambazo wafanya kazi wa uchimbaji wa gesi na bomba wakahitaji.
Mhe.Simbachawene alisema vikao kadhaaa vilisha fanyika kuanzia ngazi ya Mkoa,Wilaya vya kuwaelimisha wakazi hao umuhimu wa gesi katika kutoa nishati kwa Jamii.
Alisema gesi hiyo si kwa manufaa ya Chama fulni au ya kikundi cha watau fulani,la sivyo alisema gesi hiyo ni kwa manufaa ya Taifa kwa ujumla.
Amewaomba wana Mtwara kuelewa manufaa ya gesi ambayo itakuza uchumi wa nchi kwani maeneo 68 yamefanyiwa              Upembuzi yakinifu na kugundua kuwa na gesi.alisema wananchi hao wajiandae kwa mabadiliko ya uchumi wa Taifa hili.        

No comments:

Post a Comment