Monday, January 14, 2013

DOKTA TEREZYA HUVISA LUOGA ATEMBELEA HOSPITALI YA MKOA SONGEA NA WILAYA YA MJI MWEMA KISHA KUONGEA NA WALINA MAMA WA UWT KUANZISHA MIRADI

 Mheshimiwa Dkt Terezya Huvisa Luoha wa kwanza kulia wakitoka kuona baadhi ya vifaa tiba  alivyo vileta katika Hospital ya mkoa na wilaya hivi karibuni.
 Dkta Huvisa akizungumza na uongozi wa hospitali ya mji mwema hawapo kichani alipotembelea hospitali hiyo leo.
 Dkt Huvisa Luoga akitoka ofisi ya Mganga mkuu akiwa na Dkt Ngaiza wa hospitali hiyo mwenye shati la buluu pamoja na wanahabari kuelekea mawordini.
Dkt Huvisa na Dkt Daniel Malekela mganga mkuu wa hospitali ya mkoa Songea wakionyesha moja ya matandiko yaliyo pelekwa Mji mwema  Kutoka Shirika lisilo la kiserikali Tanzania Ecology Serving Foundatin la nchini Denmark ,ambavyo Mhe Huvisa alivileta kupitia shirika hilo.
 Dkt huvisa akimweleza Mganga Mkuu wa Mkoa kuwa ili kutatua upungufu wa wauguzi katika hospitali hiyo,aweke bajeti kwa mwaka wa fedha wa 2013/2014 ili kutengewa mishahara yao.
 Akina mama wa UWT wakimsikiliza Dkt Hovisa katika ukumbi wa ccm Mkoa leo
 Akina mama hao walikuwa wakicheza ngoma walipo kuwa wakimkaribisha Mhe. Mbunge Huvisa katika ukumbi wa CCM mkoa leo.
Na yeye kuonyesha kuwa ni mtoto wa Ruvuma ,pamoja na nyazifa alizo nazo hayuko mbali katika kusakata ngoma za jadi.
Dkt huvisa akionyeshwa moja ya kitanda kati vitanda vilivyo pelekwa Mji mwema.


AKINA MAMA WA UKUUZA MBOGA ZAOWT MKOA WA RUVUMA WATAFUTIWA SOKO LA UHAKIKA LA 

WAZIRI Ofisi ya Makamu wa Rais ( Mazingira )  Mhe.Dkt  Terezya Huvisa Luoga amewaambia akina mama wa UWT Mkoa wa Ruvuma kuwa waanzishe miradi ya Bustani za mboga,mtu binafsi  au katika vikundi  kuzalisha mboga nyingi ambazo watauza kwenye makampuni ya uchimbaji wa Ureniam yatakayo anza katika wilaya ya Namtumbo.
Amesema kuwa njia moja wapo ya kumkwamua mwanamke kiuchumi ni pamoja na kufanya kazi kwa bidii,kwa hiyari yao na siyo kulazimishwa.Mhe. Huvisa alisema soko la uhakika limepatikana la mboga  wilayani Namtumbo ambapo kutakuwa na watu wengi ambao watahitaji mboga.
Aidha alisema walime mboga za kabeji,hoho,chaina ziwe na ubora kutokana na maandalizi mazuri,pia alisema wajihusishe na ufugaji wa kuku wa mayai ,ambapo mayai yatahitajika sana na makampuni hayo  ya uchimbaji wa Urenium.
Kuhusu utunzaji wa fedha ,Dkt Huvisa alisema CRDB kuna akaunti iitwayo Malaika ambayo mteja ataweka fedha zake ,baada ya mwaka mmoja atapata faida ya asilimia 4 ya fedha yake alizoweka kwa mwaka mzima na anaweza kupata mkopo.
Ameshauri kufanya mradi kila mmoja peke yake,kwa kuwa miradi katika vikundi haidumu kwani kuna vikundi vingi vilivyo anzishwa leo havipo kwa kuto elewana  au kukosa imani kasa katika masuala ya fedha.
Amewa haidi kuwapa mbegu wale ambao wataanza mradi wa bustani za mboga,Dkt Huvisa Jana amefanya mazungumzo na akina mama wa Wilaya ya Namtumbo ambako aliahidi kutoa mbegu za mboga za bustani kwa mtu mmoja na vikundi.
Dkt Teresya Huvisa Luoga yuko mkoani Ruvuma akihamasisha akina mama kujikwamua kiuchumi kwa kuanzisha Bustani na ufugaji wa kuku wa mayai.leo ametembelea Hospitali ya Mkoa Songea na Hospitali ya Mji mwema kuangalia vifaa tiba ambavyo alivileta kupitia Shirika lisilo la Kiserikali Tanzania Ecology Serving Foundation la Denmark.Kisha akaongea na akina mama wa UWT katika ukumbi wa CCM mkoa katika Manispaa ya Songea.

No comments:

Post a Comment