Saturday, January 12, 2013

MWENDESHA WA YEBO YEBO NUSURA KUPATA MKONG'OTO KWA UZEMBE WA KUTOJUA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

Mwendesha pikipiki al maarufu Yebo yebo wa Manispaa ya Songea jina lake limehifadhiwa nusura apokee mkong'oto kwa Kiongozi ambaye alikuwa akirudi rivasi na huku akionyesha alikokuwa akielekea jina lake halikupatikana maramoja,alijikuwa kijana huyo kutaka kumwingia na pikipiki yake akiwa na abiria.
Badala ya kijana huyo kuomba msamaha kwa kuingia na kutaka kugonga sehemu siyo yake,kijana alimpolomoshea matusi ya nguoni kiongozi huyo.
Kwa kawida mtu mzima kutukanwa na mtoto mdogo anayefanana na watoto zake,alipandwa na hasira na kutaka kuchukua sheria mkononi ya kumpa mkong'oto na kisha kumpeleka kituo cha polisi atukane huko,na kunayamkini kijana huyo hata leseni hana.Waendesha vyombo vya moto iwapo ukigundua ulitaka kusababisha ajali kwa uvunjifu wa sheria za barabarani ni bora kuomba radhi kuliko kuporomosha matusi.na vijana wetu wakumbuke wana wazazi wao au watu waliyo wazidi umri kuwa na nidhamu kwa watu waliyo wazidi umri.

No comments:

Post a Comment