Thursday, January 31, 2013

UCHOCHEZI WA WANASIASA MKOANI MTWARA HAKUTASIDIA KITU KWA WANANCHI WA MKOA HUO - PINDA

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe.Mizengo Pinda ametatua mgogoro wa Gesi asilia Mkoani Mtwara,pale aliposema kiwanda cha gesi kitajengwa Mtwara.
Alisema kuwa mgogoro huo umesababisha baadhi ya wawekezaji kusita kuanza kuwekeza katika mkoa huo,lakini tatizo ni baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa kushabikia kwa wananchi wa mkoa huo kufanya uhalifu mbalimbali na kusababisha hasara kadhaa.kwa ajili ya kujijengea umaarufu wa kisiasa.Waziri Mkuu alisema ushabiki wao hausaidii bali unarudisha nyuma kasi za maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment