Thursday, January 31, 2013

MWENYE MACHO HAMBIWI TAZAMA,UPANUSI WA BARABARA JIJINI DAR ES SALAAM UNAVYO KWENDA KASI

Hilo ni Jiji la Dar es Salaam ambalo lina msongamano wa magari,kiasi kwamba waenda kazini huchelewa kufika mapema eneo la kazi na wanafunzi halikadhalika.
Serikali imeamua kupanua miundombinu ya barabara zake ili msongomano wa mgari upungue,Sambamba na hilo kumeanziswa na Train ambalo nalo lita saidia kwa kiasi kikubwa kupeleka watu kazini wakati wa asubuhi na kuwarudisha wakati wa jioni.

BEAKING NEWSSSS! MWENYEKITI WA SOKO KUU JIJINI MWANZA AKUTWA NA JENEZA/SANDUKU LISILO NA MAITI KATIKA ENEO LAKE LA KAZI

MWENYE kiti wa soko Jijini Mwanza Bwana Amadi Njola amewashangaza wafanya biashara wenzake baada ya kukuta sanduku la kuhifadha maiti likiwa tupu katikati ya magunia katika eneo lake la kazi.
Alipoulizwa alisema kuwa yeye ni mfanya kiashara kama wenzake,kwa hiyo hawakuwa na haja ya kuuliza kitu ambacho kipo katika biashara zake.
Tukio hilo lina sadikiwa kuwa liana kwenda sambamba na imani za kishirikina.Sawa ni ushirikina wa aina gani huo wa kuweka sanduku katikati ya magunia? je aliliweka kwa ajili yake ili anapo fariki jamaa zake wasipate shida ya kuchonga sanduku? na kama ndiyo kwa nini asiliweke nyumbani kwake? Tuwaachie wenyewe wahusika.

UCHOCHEZI WA WANASIASA MKOANI MTWARA HAKUTASIDIA KITU KWA WANANCHI WA MKOA HUO - PINDA

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe.Mizengo Pinda ametatua mgogoro wa Gesi asilia Mkoani Mtwara,pale aliposema kiwanda cha gesi kitajengwa Mtwara.
Alisema kuwa mgogoro huo umesababisha baadhi ya wawekezaji kusita kuanza kuwekeza katika mkoa huo,lakini tatizo ni baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa kushabikia kwa wananchi wa mkoa huo kufanya uhalifu mbalimbali na kusababisha hasara kadhaa.kwa ajili ya kujijengea umaarufu wa kisiasa.Waziri Mkuu alisema ushabiki wao hausaidii bali unarudisha nyuma kasi za maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.

UBABE WA WAFUGAJI WA KIMASAI UNAENDELA PALE WALIPO MSHAMBULIA MKULIMA WA KIJIJI CHA KIMAMBA KILOSA KWA FIMBO NA KUMJERUHI MIKONO YAKE ALIPOULIZA KWA NINI NG'OMBE WANAKULA MAHINDI YAKE

Mkulima mmoja wa kijiji cha kimamba kilosa Mkoani Morogoro Mzee Ally Mkakari jana amepata kipigo kutoka kwa wafugaji wa Kimasai ambao waliwaingiza ng'ombe wao kulisha shamba lake.
Mzee Ally alisha peleka malalamiko yake kuhusu shamba lake kushambuliwa na wanyama.lakini hakupata jibu lolote kutoka Kituo kidogo cha Polisi Kimamba.Kiukweli wamasi ni wababe wanaingiza ng'mbe kwenye mashamba ya wakulima kwa makusudi,mkulima akiuliza anapata mkong'oto hata kutotolewa uhai wake na wafugaji hao.Na uongozi wa Wilaya na Mkoa unangalia tu,hivyo kwanini wakulima wanakuwa wanyonge kwa wafugaji hao? Je wanatoa kitugani kwa uongozi wa wilaya na Mkoa? hali hiyo itaendelea hadi lini?
Kwanini wasitengewe maeneo yao wafugaji hao ,ili kunusuru uhai wa wakulima na mali zao.

MAELFU YA WAKAZI WA MANISPAA YA SONGEA LEO WAMEFUTIKA KATIKA MAZISHI YA MWENYE KITI MSTAAFU WA CCM SONGEA MJINI BWANA YASINI DIZUMBA NYUMBANI KWAKE RUHIRA SEKO

Bwana Dizumba alikuwa maarufu sana katika maisha yake,katika manispaa ya Songea na Dar es Salaam pia ambako alikozaliwa na kupata elimu yake.
Katika uhai wake amewahi kufanya shughuli mbalimbali  zikiwemo za michezo, za ulazishaji mali mapoja na shughuli za Chama mpaka anaiga dunia hapo juzi katika hospitali ya Peramiho alikuwa Mwenye kiti wa CCM mstaafu.
Aidha alikuwa kiongozi wa Timu ya majmaji na ikapanda daraja,hivyo watu wengi wanamkumbuka Dizumba kutokana na umarufu wake kwa kuwa alikuwa ni mtu wa watu.
Bw.Dizumba amezikwa nyumbani kwake Ruhira Seko ( Songea Boys ) katika Manispaa ya Songea leo na maelfu ya watu waliofurika katika mazishi yake.Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Amina.

Monday, January 28, 2013

UELEWA MDOGO KWA WAKAZI WA MTWARA KUHUSU GESI KUMEZUSHA TAFLANI MKOANI HUMO

UELEWA mdogo kwa baazi ya wananchi wa Mtwara kuhusu gesi inayopatikana mkoani humo kumezusha vurugu na kusababisha hasara iliyowakumba wananchi wasiyo na hatia.
Naibu Waziri wa Nishati na madini Mhe.George Simbachawene,amesema wananchi wa mkoa huo lazima wajiandae na mafanikio ya gesi hiyo,Ingawa si wote watapata ajira kutokana na bomba la kusafirisha gesi kwenda Dar es Salaam,lakini wanao uwezo wa kujiajiri wenyewe,kwa kufanya biashara za bidhaa ambazo wafanya kazi wa uchimbaji wa gesi na bomba wakahitaji.
Mhe.Simbachawene alisema vikao kadhaaa vilisha fanyika kuanzia ngazi ya Mkoa,Wilaya vya kuwaelimisha wakazi hao umuhimu wa gesi katika kutoa nishati kwa Jamii.
Alisema gesi hiyo si kwa manufaa ya Chama fulni au ya kikundi cha watau fulani,la sivyo alisema gesi hiyo ni kwa manufaa ya Taifa kwa ujumla.
Amewaomba wana Mtwara kuelewa manufaa ya gesi ambayo itakuza uchumi wa nchi kwani maeneo 68 yamefanyiwa              Upembuzi yakinifu na kugundua kuwa na gesi.alisema wananchi hao wajiandae kwa mabadiliko ya uchumi wa Taifa hili.        

Wednesday, January 23, 2013

BIASHARA NDOGO NDOGO KWA WANAFUNZI KATIKA MIKOA YA LINDINA MTWARA NDIYO CHANZO CHA UTORO WA WANAFUNZI KATIKA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI

Hiyo ni moja ya biashara ndogo ndogo zinazofanywa na watoto ambao ni wanafunzi wa shule za msingi na sekindari katika mashamba ya chumvi Mkoani Lindi.
Biashara hizo hufanya wanafunzi kuwa watoro wa  shule,na kufanya matokeo yao kuwa mabaya na kupolomoka kwa kiwango cha taaluma.

VIFAA VYA UJENZI MANISPAA YA SONGEA KWA BEI POA VINAPATIKANA KATIKA DUKA LA VIFAA HIVYO KATIKA JENGO LA KAURU MKABALA NA KANISA KUU LA SONGEA LA MBUNGA HARD WARE

 Bwana Ngerengera mwenye shati leupe lenye mikono mifupi mwenye duka hilo akiwa na wateja wake.
 Bw,Ngerangera akimtolea vitasa vya mlango mteja wake alivyo vinunua katika duka hilo.
Kila aina ya vifaa vya ujenzi vinapatikana dukani humo.kwa bei ya manunuzi

HALMASHURI YA MANISPAA YA SONGEA ILIVYO LEO

 Mwandishi wa Blog hii leo amepita mitaa ya Manispaa ya Songea ambapo ameshuhudia pilika pilika za wananchi waki hanagika na maisha.yao ya kila siku ya ujenzi wa taifa.
Barabara nyingi ambazo hazijajengwa katika viwango huishia kuharibika baada ya muda mfupi kutokana na malori makubwa kama hayo ambayo yana shehena kubwa kupita kiwango kinacho takiwa  kubebwa na malori hayo. kwenye barabara hizo.

WAKULIMA WA KOROSHO WANAPATA KOROSHO NYINGI KUTOKANA NA KUPALILIA MASHAMBA YAO NA KUPULIZIA DAWA

 Pamoja na wakulima wa korosho mikoa ya Mtwara,Lindi na Ruvuma kupalilia na kupulizia dawa mikorosho yao na kuvuna korosho nyingi,bado wakulima hao wanakabiliwa na tatizo la kuuza korosho zao kwa walanguzi kwa bei ya chini.
Lakini kwenye vyama vya Ushirika nako wanakopwa korosho zao,kutokana na mazingira hayo wananchi wa mikoa hiyo hawanufaiki na zao hilo.

Monday, January 14, 2013

WAKINA MAMA WA UWT MKOA WA RUVUMA WAMPONGEZA MHE. TEREZYA HUVISA LUOGA KWA KUPELEKA VIFAA TIBA KATIKA HOSPITALI YA MKOA SONGEA NA WILAYA

 Baadhi ya kina mama wa UWT mkoa wakiongea na Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais ( Mazingira ) Mhe.Terezya Huvisa Luoga picha ya chini wa kwanza kushoto na wapili ni Mwenye kiti wa UWT mkoa wa Ruvuma Bibi Kuluthum Mhagama,katika ukumbi wa CCM mkoa.
Akina mama hao wanampongeza Mhe.Terezya Huvisa Luoga kwa moyo wake wakuwaonea huruma wananchi wanateseka kwa magonjwa mbalimbali katika mkoa wake,akaweka nyuma ubinafsi akajala maisha wa watu.
Menyekiti wa UWT Mkoa Bibi Kuluthumu Mhagama alisema ,ni moyo wa pekee ambao ameuonyesha kwa wanaruvuma na Taifa kwa ujumla.kwani angeweza kuanzisha hospitali yake ambapo akanufaika na vifaa tiba vivyo.Bibi Mhagama ametoa wito kwatanzania wengine ambao wamejaliwa kuwa na marafiki katika mashirika yasiyo ya kiserikali kutafuta misaada kwa manufaa ya maeneo yao hata na taifa kwa ujumla.

MHE.DKT TEREZYA HUVISA LUOGA AKISHIKA MASHINE YA KUMSHITUA MOYO MTU ANAYETAKA KUFA

 Mhe.Huvisa Luoga ameshika mashine inayo weza kushitua moyo wa mtua anayetaka kufa.
 Hizo ndizo mashine tiba za moyo
Hiyo ni Utrasound iliyo letwa na Dkta Huvisa ambapo iliyo kuwepo iliharibikwa na kulazimu huduma hiyo itolewe na Hospitali ya Peramiho.

DOKTA TEREZYA HUVISA LUOGA ATEMBELEA HOSPITALI YA MKOA SONGEA NA WILAYA YA MJI MWEMA KISHA KUONGEA NA WALINA MAMA WA UWT KUANZISHA MIRADI

 Mheshimiwa Dkt Terezya Huvisa Luoha wa kwanza kulia wakitoka kuona baadhi ya vifaa tiba  alivyo vileta katika Hospital ya mkoa na wilaya hivi karibuni.
 Dkta Huvisa akizungumza na uongozi wa hospitali ya mji mwema hawapo kichani alipotembelea hospitali hiyo leo.
 Dkt Huvisa Luoga akitoka ofisi ya Mganga mkuu akiwa na Dkt Ngaiza wa hospitali hiyo mwenye shati la buluu pamoja na wanahabari kuelekea mawordini.
Dkt Huvisa na Dkt Daniel Malekela mganga mkuu wa hospitali ya mkoa Songea wakionyesha moja ya matandiko yaliyo pelekwa Mji mwema  Kutoka Shirika lisilo la kiserikali Tanzania Ecology Serving Foundatin la nchini Denmark ,ambavyo Mhe Huvisa alivileta kupitia shirika hilo.
 Dkt huvisa akimweleza Mganga Mkuu wa Mkoa kuwa ili kutatua upungufu wa wauguzi katika hospitali hiyo,aweke bajeti kwa mwaka wa fedha wa 2013/2014 ili kutengewa mishahara yao.
 Akina mama wa UWT wakimsikiliza Dkt Hovisa katika ukumbi wa ccm Mkoa leo
 Akina mama hao walikuwa wakicheza ngoma walipo kuwa wakimkaribisha Mhe. Mbunge Huvisa katika ukumbi wa CCM mkoa leo.
Na yeye kuonyesha kuwa ni mtoto wa Ruvuma ,pamoja na nyazifa alizo nazo hayuko mbali katika kusakata ngoma za jadi.
Dkt huvisa akionyeshwa moja ya kitanda kati vitanda vilivyo pelekwa Mji mwema.


AKINA MAMA WA UKUUZA MBOGA ZAOWT MKOA WA RUVUMA WATAFUTIWA SOKO LA UHAKIKA LA 

WAZIRI Ofisi ya Makamu wa Rais ( Mazingira )  Mhe.Dkt  Terezya Huvisa Luoga amewaambia akina mama wa UWT Mkoa wa Ruvuma kuwa waanzishe miradi ya Bustani za mboga,mtu binafsi  au katika vikundi  kuzalisha mboga nyingi ambazo watauza kwenye makampuni ya uchimbaji wa Ureniam yatakayo anza katika wilaya ya Namtumbo.
Amesema kuwa njia moja wapo ya kumkwamua mwanamke kiuchumi ni pamoja na kufanya kazi kwa bidii,kwa hiyari yao na siyo kulazimishwa.Mhe. Huvisa alisema soko la uhakika limepatikana la mboga  wilayani Namtumbo ambapo kutakuwa na watu wengi ambao watahitaji mboga.
Aidha alisema walime mboga za kabeji,hoho,chaina ziwe na ubora kutokana na maandalizi mazuri,pia alisema wajihusishe na ufugaji wa kuku wa mayai ,ambapo mayai yatahitajika sana na makampuni hayo  ya uchimbaji wa Urenium.
Kuhusu utunzaji wa fedha ,Dkt Huvisa alisema CRDB kuna akaunti iitwayo Malaika ambayo mteja ataweka fedha zake ,baada ya mwaka mmoja atapata faida ya asilimia 4 ya fedha yake alizoweka kwa mwaka mzima na anaweza kupata mkopo.
Ameshauri kufanya mradi kila mmoja peke yake,kwa kuwa miradi katika vikundi haidumu kwani kuna vikundi vingi vilivyo anzishwa leo havipo kwa kuto elewana  au kukosa imani kasa katika masuala ya fedha.
Amewa haidi kuwapa mbegu wale ambao wataanza mradi wa bustani za mboga,Dkt Huvisa Jana amefanya mazungumzo na akina mama wa Wilaya ya Namtumbo ambako aliahidi kutoa mbegu za mboga za bustani kwa mtu mmoja na vikundi.
Dkt Teresya Huvisa Luoga yuko mkoani Ruvuma akihamasisha akina mama kujikwamua kiuchumi kwa kuanzisha Bustani na ufugaji wa kuku wa mayai.leo ametembelea Hospitali ya Mkoa Songea na Hospitali ya Mji mwema kuangalia vifaa tiba ambavyo alivileta kupitia Shirika lisilo la Kiserikali Tanzania Ecology Serving Foundation la Denmark.Kisha akaongea na akina mama wa UWT katika ukumbi wa CCM mkoa katika Manispaa ya Songea.

Saturday, January 12, 2013

MWENDESHA WA YEBO YEBO NUSURA KUPATA MKONG'OTO KWA UZEMBE WA KUTOJUA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

Mwendesha pikipiki al maarufu Yebo yebo wa Manispaa ya Songea jina lake limehifadhiwa nusura apokee mkong'oto kwa Kiongozi ambaye alikuwa akirudi rivasi na huku akionyesha alikokuwa akielekea jina lake halikupatikana maramoja,alijikuwa kijana huyo kutaka kumwingia na pikipiki yake akiwa na abiria.
Badala ya kijana huyo kuomba msamaha kwa kuingia na kutaka kugonga sehemu siyo yake,kijana alimpolomoshea matusi ya nguoni kiongozi huyo.
Kwa kawida mtu mzima kutukanwa na mtoto mdogo anayefanana na watoto zake,alipandwa na hasira na kutaka kuchukua sheria mkononi ya kumpa mkong'oto na kisha kumpeleka kituo cha polisi atukane huko,na kunayamkini kijana huyo hata leseni hana.Waendesha vyombo vya moto iwapo ukigundua ulitaka kusababisha ajali kwa uvunjifu wa sheria za barabarani ni bora kuomba radhi kuliko kuporomosha matusi.na vijana wetu wakumbuke wana wazazi wao au watu waliyo wazidi umri kuwa na nidhamu kwa watu waliyo wazidi umri.

NI DALILI NZURI KWA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA MKOANI RUVUMA MWAKA HUU

Wakulima wa mkoa wa Ruvuma hususan wakulima wa mahindi wameisifia mvua ambayo inaendelea kunyesha kuwa ni mvua nzuri kwani inanyesha, na kutulia ambapo inaipa mimea kukua kwa haraka.
Mkoa huu iwapo bei za mbolea nzingekuwa na unafuu wa kununua kwa kila mkulima wa mkoa huu,mazao yangekuwa mengi mmno.
Kutokana na wakulima kuwa na uwezo mdogo wa kipato hivyo inawalazimu kulima kishamba kidogo ambacho hakina tija wala faida kwa kushindwa kununua mbolea nyingi na alime shamba kubwa.

MIAKA 49 YA MAPINDUZI ZANZIBAR DKT. MOHAMED ALL SHEIN AHUTUBIA WANANCHI

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt All Mohamed Shein asema Serikali yake haita mvumilia mtu atakayelenga kuvuruga amani iliyopo hivi sasa nchini.
 Sherehe hizo lilipambwa na majeshi ya ulinzi na usalama,ambapo Rais aliyakagua kabla ya kupita kutoa heshima kwa mwendo wa haraka na pole.
Wakipita mbele ya Jukwaa mwendo wa pole wakitoa hashima.

Friday, January 4, 2013

TUNAKUOMBEA KILA LA KHERI (SAJUKI) MUNGU ILAZE ROHO YAKE PEPONI,WATANZANIA TUNAZIDI KUPOTEZA WASANII AMBAO BADO TUNAWAHITAJI

Msanii Sadick  Juma Kilowoko ( SAJUKI) akiwa katika safari yake ya mwisho hapa duniani.Kazi ya Mungu  haina makosa.
Ila wimbi la kupoteza wasanii wetu Tanzania limezidi kuwakumba wasanii, mmoja hadi mwingine hebu tujiulize tatizo liko wapi.
Wasanii wachanga kabisa ambao walianza kujulikana ndani na nje ya nchi tunawapoteza,tumuombe Mungu aepushe vifo vya wasanii wetu ambao ndiyo kwanza wanaanza kujulikana.
Pamoja na yote hayo wasanii wetu ambao ni kioo cha nchi yetu katika kutoa mafundisho kuburudisha na kuhimiza jamii kujirekebisha kutokana na mafundisho yanayotolewa na wasanii hao.