Thursday, October 29, 2015

SHAMRASHAMRA KUMPONGEZA DKT JOHN POMBE MAGUFULI ZILITANZA KATIKA MJI WA MAKAO MAKUU YA CCM MJINI DODOMA ,MAGARI, PIKIPIKI ZIKIWA NA BENDERA ZA KIJANI,WAKIKSEMA HAPA NI KAZI TU.

Magari na pikipiki yakisimama kwa ghafla kupisha au kuruhusu vijana ,watu wazima ,akina mama na watoto wakiwa kwenye furaha za kupongeza ushidhi baada ya kutangazwa na Tume ya Uchaguzi .
Furaha zao zilifanywa kwa Amani na Utulivu,ambapo magari ya polisi katika mji huo yalionekana yakipita pita kuhakikisha amani inakuwepo kwa waliyo furahia matokeo na wale ambao upepo umewaendea kombo lakini wote ni watanzania na watabaki kuwa watanzania

TANZANIA IMEINGIA KATIKA HISTORIA YA KUTANGAZA MATOKEO YA URAIS KWA DKT JOHN POMBE MAGUFULI NA MGOMBEA MWENZA WAKE SAMIA HASSAN SULUHU KWA KURA 8,882,935. NA KUIWEKA TANZANIA KATIKA HISTORIA YA KUWA NA MAKAMU WA RAIS MWANAMKE,WATANZANIA WANATEGEMEA MABADILIKO KAMA WALIVYO ELEZA KWENYE SERA ZAO

 Rais Mteule  Dkt.John Pombe Magufuli leo ametangazwa rasmi  kuwa Rais  wa awamu ya Tano baada ya kushinda kwa kura 8,882,935 akifuatiwa na Mhe. Edward Lowassa kwa kura 6,072,848.

Kutokana na matokeo hayo Mgombea mwenza Mhe. Samia Hassan Suluhu anakuwa makamu wa Rais wa kwanza  mwanamke Tanzania,Hongera zao.Na kwamba kesho kuanzia saa 4. watatunukiwa Hati au Cheti cha hushindi.
Mhe.Samia Hassan Suluhu Mgombea mwenza wa Dkt Magufuli  kutokana na Sera zao wameibuka kuwa washindi kwa kura 8,882,935,kesho watatunukiwa hati ya ushindi katika ukumbi Diamond Jubelee Jijini Dar es Salam saa 4 asubuhi.Hongereni sana watanzania wanasubiri mabadiliko.

Monday, October 26, 2015

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YATANGAZA MATOKEO YA URAIS KUPITIA VYOMBO VYA HABARI ,NA KUTOA ANGALIZO

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva ameanza kutangaza matokeo ya Urais ambapo Kupitia CCM Dr. Joseph Pombe Magufuli anaonekana kuongoza akifuatiwa na wa CHADEMA Edward Lowassa.Jaji Lubuva amewaambia wandishi wa habari kuwa  kesho saa tatu asubuhi. ataendelea kutangza matokeo mengine yatakayo pokelewa kutoka  kwenye Majimbo ya uchaguzi nchini.

Aidha alisema kuwa mwenye mamlaka ya kutangaza matokeo ya Urai ni Tume ya Uchaguzi ya Taifa peke yake, mtu mwingine atakapo tangaza yatakuwa siyo matokeo rasmi.Na kwamba aliwaonyesha waandishi wa habari makaratasi yaliyo sainiwa na mawakala wa vyama vyao.na kutumwa Tume ili yatangazwe.

Saturday, October 24, 2015

KITUO CHA KUPIGIA KURA CHA OFISI ZA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA DODOMA SAA MOJA KAMILI WANANCHI WALIANZA KUPIGA KURA,KWA AMANI NA UTULIVU MKUBWA

  • Kuona jinsi wananchi walivyo hamasika wengi wamejitokeza kwa wingi kwenda kutimiza haki zao za msingi  cha chagua viongozi wanao wataka.
  • Mabasi yakutoka na kuingia kwenye stendi ya mabasi Mkoa wa Dodoma  hayapo wasafiri nao hawapo stendi imetulia kama vile watu hawapo.
  • Kwenye Zahanati ya Mkole nako hata wagonjwa nao hawapo pametulia.
  • Barabara na mitaa ya Mji wa Dodoma kumetulia .ukweli hali ni shwari.
  • Kituo hicho hali nishwari kabisa ,wanamama,wazee,na vijana wamejitokeza na wameelekezwa vya kutosha.

 Foleni ya wapiga kura katika kituo cha ofisi za Shirika la Nyumba na Taifa wakiwa katika kusubiri zamu zao  za kupiga kura zifike
  • Hii barabara ya kutoka Bungeni kuelekea mjini iko tupu
Foleni ya wapiga kura pamoja wa waandishi wa habari wako sambamba kufuatilia mwenendo mzima wa kupiga kura,akiwemo wa ITV na vymombo vingine li kuhabarisha Taifa na Dunia kwa ujumla kuonyesha jinsi Tanzania ilivyo kuwa na Ukomavu wa Vyama vingi na kuzingatia Democrasia ya kweli..


Hiki ni kituo cha Zahanati cha Makole kumekuwa na utulivu kama vile wagonjwa hawapo,lakini yote ni kwenda kupiga kura.

TUNAMSHUKURU MUNGU KWA KUANZA NA KUMALIZA KAMPENI KWA AMANI NA UTULIVU, HIVYO WATANZANIA KESHO WAKATIMIZE WAJIBU WAO ,KWA AMANI NA UTULIVU ULIOKUWEPO WAKATI WA KAMPENI

Viongozi wa wametumiza wajibu wao wa kunadi Sera zao wakati wa Kampeni kwa Amani ,Utulivu,Busara zilizotumika katika kuonyesha ukomavu wa Demokrasia wa Vyama vingi.

Hivyo ukomavu huo wananchi wautumie kumpata kiongozi ambaye atatimiza ndoto za watanzania.Ni imani yetu uchaguzi utaenda salama hapo kesho kwa kuwa uchaguzi unapita,baada ya hapo majukumu yetu yataendelea kama kawaida.

Tunaipenda Tanzania yenyebamani na n chi ya mfano wa kuigwa hivyo tuulinde mfano huo,Mungu ataepusha machafuko amabayo yanatokea kwenye nchi zisizo na Amani.Tujitokeze  kuanzia saamoja asubuhi tupige kura turudi nyumbani tusubiri matokeo.

Wednesday, October 21, 2015

WAKATI ZIMEBAKIA SIKU TATU WATANZANIA WATUMIE HAKI YAO YA KUCHAGUA VIONGOZI WANAO WATAKA MKURUGENZI WA HUDUMA ZA SHERIA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI BWANA EMANNUEL KAVISHE ASEMA MWENYE KUTANGAZA MATOKEO NI TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

Aidha Bw. Kavishe amesema Viongozi wa Vyama na wananchi wanatakiwa kupiga kura zao kwa amani na utulivu na kwamba ,baada ya kupiga kura watu warudi walikotoka na kusubili matokeo ambayo yatangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Amesema Mtu atayepata kura nyingi atatangazwa kutoka kwenye chama chochote ambacho mgombea amepata kura nyingi.
kuhusu idadi kamili ya wapiga kura tarehe 25 mwezi huu ,amesema kuwa ni watu milioni 22..7 ambao wanatarajiwa katika upigaji kura siku hiyo,nakwamba kila mtu atapiga  kura kwenye kituo alichojiandikisha,na kama yuko nje ya kituo chake basi mtu huyo atakuwa amekosa haki yake ya kumchagua kiongozi anaye mtaka.
Pia kasema ili kuepusha vurugu zisizo na sababu wananchi wafuate maelekezo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi,na kuheshimu Katiba.Na madai ya kubaki kwenye vituo baada ya kupiga kura, inamaana mawakala waliyowekwa na vyama vyao hawaviamini.maana waele ndiyo watao hakikisha mgombea wake amepata kura ngapi.

Saturday, October 17, 2015

WANAFUNZI 177 WA CHUO CHA UHASIBU CBM DODOMA KILICHOJULIKANA KAMA ASEK WAMEHITIMU KATIKA NGAZI YA STASHAHADA NA CHETI











Wahitimu hao wa 177 wakiwemo 102  wa Stashahada  na 75 wa Cheti katika fani za Procurement and Supply,Marketing,Banking and Financial and Accountancy  katika Chuo hicho jana 

Saturday, October 10, 2015

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA JAKAYA KIKWETE AZINDUA KIWANDA CHA KUCHAKATA GESI MADIMBA MTWARA LEO

Nakwamba Rais amezindua viwanda vingine  vya Mtwara kikiwemo cha saruji,kiwanda kikubwa ambacho kitawanufaisha wananchi wa Kusini na majirani zao.

Tuesday, October 6, 2015

BLOG YA TUJIFUNZE KUSINI INATOA POLE KWA FAMILIA YA MWANASIASA MKONGWE MCHUNGAJI CHRISTOPHER MTIKILA ,PAMOJA NA WANASIASA KWA KUFUATIA KIFO CHA MWANA SIASA HUYO AMBAPO MCHANGO WAKE UILIKUWA BADO UNAHITAJIKA

Tukio la mwana siasa huyo limemshitua kila mmoja wetu , lakini hatuna uwezo zaidi wa kuamua lini na wapi na muda gani binadamu atatoweka duniani  na kwa mtindo gani,yote tumuachie Mungu kwani yeye ndiye mwenye kujua nani anamuhitaji kumchukua.
Hivyo Familia na wale wote wenye mapenzi mema kwa marehemu Mtikila kuwa na subira hasa kwa kipindi chote cha msiba huu,kwani Bwana alitoa na Bwana alichukua.Roho ya Marehemu Mungu ailaze mahali pema peponi Amina.

WAKATI ZIMEBAKI SIKU CHAHCE KUELEKEA UCHAGUZI MKUU WA MADIWANI,WAGUNGE NA URAIS,WATANZANIA WAMETAKIWA KUWA KUTUNZA SHAHADA ZAO ZAKUPIGIA KURA

Baadhi ya wananchi wenye kuipenda amani utulivu,pamoja na utulivu, upendo kwa atanzania wote kuacha kuwahadaa watu  wenye shahada zao za kupigia kura kuzifanya ziwe bidhaa kwa mafaniko yao katika kuchaguzi ujao.

 Aidha wanaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kusikiliza Sera za wagombea mbalimbali wa vyama vyote ,ili wajue na wachambue mbivu na mbicha tarehe 25 mwezi huu.

Lakini sanasana cha muhimu ni kuaandaa mazingira ya Amani ,utulivu siku hiyo ya kupiga kura.Hasa kila mmoja amalizapo kufanya kitendo cha haki yake ya kumchagua Diwani,Mbunge na Rais tarehe 25, arudi nyumbani kwakwe kusubili matokeo.

Wale ambao wanatarajia kubakia vituoni kusubiri kuona aliyemchagua kashinda,waache kwani kufanya hivyo kutasababisha uvunjifu wa Amani.Nini maada ya mawakala wa vyama na Tume ya Uchaguzi,Kazi ya kutangaza matokeo ni Tume ya Uchaguzi wengine Turudi majumbani mwetu.

Inajulikana kuwa kura ni siri ya mpiga kura,sasa wewe mwingine kushabikia fulani lazima ashinde je wewe ulikuwa na wapigakura wote nchini ukaona wamemchagua huyo unaye sisitita kuwa kashinda ,jamani tuwaachie wenyewe watakao hesabu kura na kutoa matangazo.

Blogu hii imesikiliza maoni ya baadhi ya Wananchi wa Dodoma wakielezea mtazamo wao katika mwelekeo wa Uchaguzi mkuu tarehe 25 mwezi huu,na kwamba iwapo wananchi watafuata maelekezo ya Tume ya Uchaguzi na Vyombo vya Ulinzi na Usalama ,Uchaguzi siku hiyo utakuwa wa  Amani na Utulivu kwani Tanzania ni Kisiwa cha Amani.Hivyo tumuombe Mungu aifanye siku hiyo iwe ya Amani na Utulivu na Atuongoze katika kuwapata viongozi ambao ni chaguo lake.

Saturday, September 19, 2015

WASHABIKI ACHENI TABIA ZA KUCHANA MABANGO YA WAGOMBEA NAFASI MBALIMBALI ZA UONGOZI KATIKA UCHAGUZI MKUU UJAO HIVI PUNDE MWAKA HUU

Blogu hii imekuta baadhi ya wananchi katika Manispaa ya Dodoma wakilaani vikali kitendo cha kuchaniwa bango la mgombea ubunge wa Jimbo la Dodoma mjini kupitia CCM hivi karibuni nyakati za usiku,na kwamba kitendo hicho hakikuwapendezesha watu wenye hekima na busara zao mjini hapa.
.
Wanasema vitendo hivyo havina tija wala faida kwao na pengine watu hao hawajui thamani za vitu.Wanajiuliza walikuwa na tatizo gani na bango mpaka kulichana, wamesema mambo ya uchaguzi ni ya mpito tu baada ya hapo hali itaendelea kama kawaida,sasa aliyefanya kitendo hicho anapokutana na mgombea huyo atakuwa na amani moyoni mwake.

Aidha walisema vitendo hivyo havifai kama ndiyo ushabiki wa aina hiyo basi haufai kwakuwa ni vitendo vinavyo ashiria uvunjifu wa amani na upendo. katika Jamii ya Kitanzania na Duniani kote

Kufuatia kauli ya viongozi wa ngazi ya juu wa ulinzi na usalama wa mkoa huu,kwamba la kumtaka kila mwananchi akisha piga kura siku hiyo arudi nyumbani kwake kusubili matokeo,Kauli hiyo kwa watu kama hao inaweza kugonga mwamba kwa kutaka kubakia vituoni kusubiri matokeo.

Alisema watu  watakao kiuka agizo hilo asishangae kuona vyombo vya usalama vitapo mshughulikia kikamilifu maana atakuwa ameyataka mwenyewe kwa sababu ya ushabiki,hawajui ushabiki una weza kusababisha machafuko ya kupigwa na hata vifo vya kujitakia.Hivyo wenye tabia kama hizo waziache maana zita waletea wananchi kukosa amani kwa ajili ya watu wachache wasiye taka kusikia.

Tuesday, September 1, 2015

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA JAKAYA MRISHO KIKWETE AAGWA NA VYOMBO VYA ULINZI NA USALMA KATIKA UKUMBI WA DIAMOND JUBILEE JIJINI DAR ES SALAM


Ameagwa na vyombo vya ulinzi na Usalama Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam na kupewa zawadi ya Trector na majembe yake ambapo Mama Salma Kikwete  amepewa zawadi ya ng’ombe wa maziwa.
Katika hotuba yake na vyombo hivo amewashukuru sana,kasha akasema anaondoka ikiwa watu bado wanampenda.
Aidha alisema anauhakika kuwa vyombo vya Ulinzi na usalama vipo katika hali nzuri, vikiwa na zana za kivita  imara, kujenga  Air Force imengwa,nyumba 10000 zinajengwa  ikiwa nyumba 6,000 ni Askari wa kawaida ambapo nyumba 4,000 ni za Mofisa wa ngazi za juu ,wakati na chini.
Jesha la polisi wanaletewa magari ambapo mipango imesha fanyika Nchini India,magari hayo muda wowote yatawafikia Jeshi la Polisi.
Magereza wao bado kupanga mapendekezo yao,amewaambia wafanye haraka kabla hajaondoka aidhinishe ili atakaye mpokea amkabidhi.
Alisema alichofarijika nalo ni la Umoja wa vyombo vya Ulinzi na Usalama,Kuboresha maslahi ya watumishi wa Umma na Vyombo vya Usalama.
Usipo wekeza kwenye vyombo vya ulinzi na Usalama ,Unaweka rehani maisha ya wananchi,pamoja na ughali wake lazima kuwekeza kwenye vyombo vya Ulinzi na usalama kwa usalama wa ulinzi wan chi na watu wake.
Kama vyomba ulinzi na usalama ni dhaifu mali zote zitahujumiwa bila kujua.Meli mbili zimeanza kulinda kwenye bahari yenye kina kirefu.
Uimara wa uchumi wan chi lazima ulindwe na Jeshi lake na uchumi ule lazima ulindwe kwa upanga.msipowekeza kwenye ulinzi na usalama ,mabenki yote yataibiwa kila siku.
Alisema Dunia sasa inabadilika kwa Sayansi na Teknolojia,lazima na majeshi yetu yafikie huko,Mf moi kumenunuliwa mashine yenye thamani ya Dollar milioni 2, ili kuokoq mqisha ya wananchi ,ukiogopa aghali huwezi kuokoa maisha ya wanachi.
Aidha alisema mwaka huu kuna uchaguzi,vyombo vya ulinzi na usalama hasa Polisi,kuhakikisha upigwaji kura unakuwa wa usalama ,hategemei kuwa kutakuwa na matukio ya kulishinda jeshi la Polisi.
Anastaafu atarudi  kuwa raia maarufu, Hawezi kwenda kuomba atoe ushauri kwa Rais,maana Rais washauri wake. Akitaka ushauri ataenda kuomba ushauri wa kulima mananasi yake,alisema Duniani hapa amefanya kazi kubwa ya Urais.siwezi kuomba kazi,kwa manufaa ya nchi yake kama ataombwa ushauri nitakuwa tayari.
Amesema kuwa walikuwa ndiyo nguzo yake,mhimili wake,kama walivyo msaidia na kumshauri atakaye atayeshika madaraka.kama walivyomshauri na nchi iko shwari.

Monday, August 31, 2015


MGOMBEA URAIS KUPITIA CHAMA CHA ACT WAZALENDO BIBI ANNA MGHWIRA AHAIDI KUUNDA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA AKIJUMUISHA VYAMA VYOTE NA MAKUNDI YA KIJAMII

 Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha ACT Bibi Anna Mghwira  akitaja misingi ya Utu,Uadilifu na Uzalendo katika Chama chake,Jana katika Viwanja vya Mbagala Jijini Dar es Salaam  katika Uzinduzi wa Kampeni ambapo amesema ataunda serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa kujumuisha Vyama vyote mradi wawe na Utu,uadilifu na Uzalendo.
Baadhi ya wananchama waliyo hudhuria katika mkutano huo wa uzinduzi wa Kampeni ya ACT katika Viwanja vya Mbagala Jijini Dar es Salaam jana

 
Mgombea Urais huyo alisema hayo wakati  akizungumza na wanachama wa chama hicho katika viwanja vya Mbagala Jijini Dar es Salaam leo.
Amesema kuwa iwapo atapa ridhaa ya kuwa Rais wa awamu ya Tano ataunda serikali ya umoja wa Kitaifa kutoka vyama vyote,wananchi na Sekta mbalimbali kwa msingi wa kujali Utu,Uadilifu na Uzalendo.
Ametaja vipaumbele vyake ni pamoja na Hifadhi ya Jamii,Tatizo la ajira kutokana na  uwekezaji katika kilimo,Kuimarisha Makao makuu ya Dodoma kuwa ya Serikali,siyo ya Chama.kwani Dodoma ni katikati ya nchi makao makuu ya chama yatatafutiwa sehemu nyingine.
Vingine ni pamoja na hifadhi ya jamii,viwanda vya mazao ya kilimo,uvuvi utalii na michezo,nakwamba maliasili zote zitakuwa za wananchi na sio za Katiba,pamoja na kuboresha Elimu kwani watoto wanamaliza Elimu ya Msingi hawawezi kusoma na wale waliomaliza Elimu ya sekondari hawawezi kusoma barua ambapo wanaomaliza vyuo vikuu hawawezi kujieleza katika ofisi wanazofanyia kazi.
Aidha amesema kuwa watoto wengi wenye vipaji  wako mitaani wanaitwa watoto wa mitaani, serikali yake watoto wote hao watapata elimu.
Alisema iwapo atapata ridhaa hiyo ya kuwa Rais Mwenye kiti wa Chama hicho Bwana   Zitto Kabwe atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Awali Kampeni Meneja wa Chama hicho,ni mkakamavu na shujaa anayesema mambo asiyo na uhakika nayo yanayo sababisa kuingilia Utu wa mtu,lakini katika Sera zao wanajali utu,Uadilifi na Uzalindo katika Ilani yao ya Uchaguzi, kutokana na kauli ile ya kudhalilisha utu wa mtu vinaendana na wanayoyanadi.Kitu kile hakipendezeshi watu.Anatakiwa kunadi Ilani na Sera ya Chama chake siyo kukosoa kwani wana uhakika gani kama wakipata ridhaa kutawala watateleza ahadi zote kwa wananchi. Walizo zisema..
Kwa Stahili ile Chama cha Mapinduzi CCM kitaendelea kutawala  kwa muda mrefu kwa kuwa vyama vya Upinzani badala ya kusaidiana katika kunadi Sera zao wanazarauliana wao kwa wao.
Lakini kwanini  wanashambuliana wao kwa wao wakati wanadai kuleta mabadiliko katika Siasa,wakidai CCM imekaa madarakani kwa muda mrefu bila mabadiliko.Nimeamini kuwa vita vya panzi furaha ya kunguru.
Ukweli ndoto ya Ukawa kwenda Ikulu kwa Stahili ya msemaji wa ACT Wazalendo  ambaye ni Kampeni meneja haipo,kwani itawachanganya hata wananchi ambao nao walikuwa na ndoto ya madiliko wakachagua kuendelea na CCM hiyohiyo.kwa inaonyesha kuwa vyama hivyo kila kiongozi anataka madaraka ya juu.
Ila Mgombea wao anajua kutetea Sera na Ilani ya Chama chake,amepanga vipaumbele vyake kwa ufasaha na hakuwa na haja ya kuwalaumu wenzake au viongozi wailiyo shika madaraka ya juu.






Friday, August 21, 2015

WAGOMBEA UBUNGE KWA TIKETI YA CCM NA CHADEMA MJINI DODOMA UMEPAMBA MOTO KAMERA YATU IMEPATA MSAFARA WA MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA DODOMA MJINI WA CHADEMA AKIENDA KUCHUKUA FOMU KWENYE OFISI ZAO

 Baadhi ya gari lenye wapambe waliokuwa wakimsindikiza mgombea Ubonge kwa tiketi ya CHADEMA Jimbo la Dodoma Mjini kwenda kuchukua fomu kwenye Ofisi yao.
Sasa kimeeleweka maagizo ya kuacha ushabiki wa mbwembwe katika kusindikiza wagombea umeeleweka,


PAMOJA NA USHABIKI KWA WAKEREKETWA ,CHA MSINGI HAPA NI KUWA NA SHAHADA YA KUPIGIA KURA

Ushabiki wa kusindikiza viongozi kwenda kuchukua Fomu na kurudisha Fomu,uwe wa amani na nidhamu bila kujali Itikadi za vyama vyao.

Kinachao takiwa kutolewe elimu kwa mashabiki hao, siku ya kupiga kura wasijae kwenye vituo vya kupigia kura na kudai wanamtaka nani,kelele kibao waache. wawaachie mawakala wafanye kazi yao.

Maana mkono wa Dola ni mrefu kupita kawaida,watapigwa bila faida yoyote kwani huyo watakaye mtaka kuwa Diwani, Mbunge au Rais  akichaguliwa au hakuchaguliwa watapa faida gani au hasara gani.

Ushabiki usio na tija hauta saidia,Wananchi wengi wanaomba kwa Mungu kuwepo na Upigaji kura wa Amani,Ili Tanzania Ibakie kuwa kisiwa cha Amani.

Wengine wanasema hata viongozi nao waache lugha za kashfa wakati wa Kampeni zao,Matusi,lugha za kejeli,Ubabe na umwamba kwenye Kampeni hazisidii wananchi,Wananchi wanacho hitaji ni maisha nafuu, kumtoa mtanzania mwenye kipato cha chini na kumpeleka kwenye kipato walau hata cha kati na sio wimbo uliyozoeleka kila Awamu.

Tunawatakia Amani,Utulivu,Upendo na kuhasehimiana wakati wa Kampeni zao kwa kila Chama kilichoingia kwenye  kinyang'anyilo cha Udiwani,Ubonge na Urais

Sunday, July 12, 2015

NITUMENI NITAWATUMIKIA,KWA NGUVU ZOTE,MOYO WOTE - DKT JOHN POMBE MAGUFULI

 Hotuba yake Magufuli baada ya kutangazwa
Wajumbe wa Mkutano huo


Dkt John Pombe Magufuli alisema hayo baada ya kutangazwa kuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania.
Aidha alisema kuwa yuko tayari kunadi Ilani ya CCM, na kwamba wenzake 38 atakuwa nao pamoja katika kuinadi Ilani ya Chama hadi ushindi unapatikana. Kwani Chama kwanza,CCM kwanza na Tanzania kwanza,ni lazima kuwa kitu kimoja.
Baadaye kamtangaza Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea mwenza,na kuweka Hitoria katika Ramani ya Dunia kuwa na Mwanamke  wa kwanza Tanzania kuwa mgombea mwenza mwanamke.
Hatimaye saa 10 jioni leo Dkt Magufuli atanadiwa katika uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma na Juma nne Dar es Salaam.

HATIMAYE DKT JOHN POMBE MAGUFULI ASHINDA KWA KURA 2,104 NA KUPONGEZWA NA DKT ASHA ROSE MIGIRO BAADA YA KISHINDO CHA USHINDI

Dkt John Pombe Magufuli  ndiye aliyepata nafasi kupitia Tiketi Chama chake kuwa mgombea Urais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,kwa kupigiwa kura na wajumbe wa Mkutano mkuu wa CCM,kwa kupata kura 2,104,ambapo Balozi Amina Said Ally kwa kura 253 na Dkt Asha Rose Migiro kwa kura59.

Wote wapo tayari kambi zao kuwa bega kwa bega na Dkt John Pombe Magufuli kuhakikisha ushindi unapatikana kwa Dkt Magufuli wa kupeperusha Bendera ya CCM.Na mwenye kiti wa Chama hicho.

Wednesday, June 17, 2015

NG,OMBE 94 NA MBUZI 75 WA MFUGAJI MMOJA JINA LAKE HALIJAPATIKANA KATIKA MANISPAA YA DODOMA WAMESHIKWA WAKIWA SAZURULA KATIKA MANISPAA HIYO KUTOKANA NA KUKIUKA AGIZO LA SERIKALI LA KUHAMISHA MIFUGO YOTE KWENDA NJE YA MANISPAA

Uongozi wa Manispaa ya Dodoma ilishatoa agizo kuwa kila mfugaji ahamishe mifugo yake kupeleke nje ya Manispaa,na atakayekiuka agizo hilo ng,ombe akikamatwa atapaswa kumlipia shilingi 20,000 na mbuzi shilingi 10,000.kila mmoja.
Kwa hiyo mfugaji huyo anang,ombe 94 kila mmoja shilingi 20,000 sawa na shilingi 1,880,000 na mbuzi 75 ikiwamo mmoja shilingi 10,000 ,mfugaji huyo italazimu kulipa shilingi 2,630,000 kwa sababu ya kiburi na ujeuri wa kupingana na maagizo yanayotolewa na Serikali.
Mmoja anayeshughulikia mifugo inayo zurula hovyo katika Manispaa hii alisema,mara nyingi wenye mifugo wamelekezwa nini cha kufanya,lakini wanakiuka,nakwamba mjini kuwepo na mifugo inayochungwa haileti picha nzuri ni vyema watoe ushirikiano na mamlaka husika ,kuhamisha mifugo mbali na Mji.

JAJI MKUU MSTAAFU AGUSTINO STIVIN RAURENCE RAMADHANI ASEMA ANAUWEZO WA KUWA RAIS IWAPO CHAMA CHAKE KITAMPA RIDHAA YA KUONGOZA


Jaji Ramadhani aliwahikuwa askari kwa cheo cha Luteni Usu mwaka 1971 na hatimaye Brigedia Jenerali,vita vya Uganda naye alikuwemo.akaongeza kuwa mwaka 1978 alikuwa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar.


Alisema kuwa baadaye aliteuliwa kuwa Jaji Mkuu Zanzibar na hatimaye Tanzania Bara hadi kustafu kwake,na kwamba hadi sasa ni Jaji Mkuu wa Afrika na ni Mtanzania wa kwanza kushika nafasi hiyo, hivyo kutokana nafasi yake aliyokuwa nayo anasema anauzoefu na anauwezo na sifa za kuwa Rais wa Nchi hii.Pia ni msafi hana tuhuma za rushwa.

Kuhusu mauaji ya wenye ulemavu wa ngozi ,amesema yeye akiwa Rais atahakikisha kunatolewa elimu kwa wananchi kuondoa imani potofu ya kuwa viungo vya Albino vinampa mtu utajiri au cheo nasio mwili mzima.na kwamba serikali iliyoko madarakani imeshaanza kuchukua hatua kali kwa wale waliobainika wamefanya mauaji kwa walemavu wa ngozi hao.

Aidha akiwajibu waandishi wa habari kuhusu kuwa na wafuasi wengi wakati wa kuchukua fomu, alisema .sipendi makeke wakati wa kuchukua fomu,asema kibaya chajitembeza na kizuri chajiuza.

Jaji Ramadhan amekabidhiwa fomu kadhaa zikiwemo za kupeleka mikoani kuomba wadhamini,na kisha kuzirudisha kwenye ofisi za Chama hicho Mjini hapa.