Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha ACT Bibi Anna Mghwira akitaja misingi ya Utu,Uadilifu na Uzalendo katika Chama chake,Jana katika Viwanja vya Mbagala Jijini Dar es Salaam katika Uzinduzi wa Kampeni ambapo amesema ataunda serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa kujumuisha Vyama vyote mradi wawe na Utu,uadilifu na Uzalendo.
Baadhi ya wananchama waliyo hudhuria katika mkutano huo wa uzinduzi wa Kampeni ya ACT katika Viwanja vya Mbagala Jijini Dar es Salaam jana
Baadhi ya wananchama waliyo hudhuria katika mkutano huo wa uzinduzi wa Kampeni ya ACT katika Viwanja vya Mbagala Jijini Dar es Salaam jana
Mgombea
Urais huyo alisema hayo wakati
akizungumza na wanachama wa chama hicho katika viwanja vya Mbagala
Jijini Dar es Salaam leo.
Amesema
kuwa iwapo atapa ridhaa ya kuwa Rais wa awamu ya Tano ataunda serikali ya umoja
wa Kitaifa kutoka vyama vyote,wananchi na Sekta mbalimbali kwa msingi wa kujali
Utu,Uadilifu na Uzalendo.
Ametaja
vipaumbele vyake ni pamoja na Hifadhi ya Jamii,Tatizo la ajira kutokana na uwekezaji katika kilimo,Kuimarisha Makao
makuu ya Dodoma kuwa ya Serikali,siyo ya Chama.kwani Dodoma ni katikati ya nchi
makao makuu ya chama yatatafutiwa sehemu nyingine.
Vingine
ni pamoja na hifadhi ya jamii,viwanda vya mazao ya kilimo,uvuvi utalii na
michezo,nakwamba maliasili zote zitakuwa za wananchi na sio za Katiba,pamoja na
kuboresha Elimu kwani watoto wanamaliza Elimu ya Msingi hawawezi kusoma na wale
waliomaliza Elimu ya sekondari hawawezi kusoma barua ambapo wanaomaliza vyuo
vikuu hawawezi kujieleza katika ofisi wanazofanyia kazi.
Aidha
amesema kuwa watoto wengi wenye vipaji
wako mitaani wanaitwa watoto wa mitaani, serikali yake watoto wote hao
watapata elimu.
Alisema
iwapo atapata ridhaa hiyo ya kuwa Rais Mwenye kiti wa Chama hicho Bwana Zitto
Kabwe atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Awali
Kampeni Meneja wa Chama hicho,ni mkakamavu na shujaa anayesema mambo asiyo na
uhakika nayo yanayo sababisa kuingilia Utu wa mtu,lakini katika Sera zao
wanajali utu,Uadilifi na Uzalindo katika Ilani yao ya Uchaguzi, kutokana na
kauli ile ya kudhalilisha utu wa mtu vinaendana na wanayoyanadi.Kitu kile
hakipendezeshi watu.Anatakiwa kunadi Ilani na Sera ya Chama chake siyo kukosoa kwani
wana uhakika gani kama wakipata ridhaa kutawala watateleza ahadi zote kwa
wananchi. Walizo zisema..
Kwa
Stahili ile Chama cha Mapinduzi CCM kitaendelea kutawala kwa muda mrefu kwa kuwa vyama vya Upinzani
badala ya kusaidiana katika kunadi Sera zao wanazarauliana wao kwa wao.
Lakini
kwanini wanashambuliana wao kwa wao
wakati wanadai kuleta mabadiliko katika Siasa,wakidai CCM imekaa madarakani kwa
muda mrefu bila mabadiliko.Nimeamini kuwa vita vya panzi furaha ya kunguru.
Ukweli
ndoto ya Ukawa kwenda Ikulu kwa Stahili ya msemaji wa ACT Wazalendo ambaye ni Kampeni meneja haipo,kwani
itawachanganya hata wananchi ambao nao walikuwa na ndoto ya madiliko wakachagua
kuendelea na CCM hiyohiyo.kwa inaonyesha kuwa vyama hivyo kila kiongozi anataka
madaraka ya juu.
Ila
Mgombea wao anajua kutetea Sera na Ilani ya Chama chake,amepanga vipaumbele
vyake kwa ufasaha na hakuwa na haja ya kuwalaumu wenzake au viongozi wailiyo
shika madaraka ya juu.
No comments:
Post a Comment