Ameagwa na vyombo vya ulinzi na
Usalama Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam na kupewa zawadi ya Trector na majembe yake ambapo
Mama Salma Kikwete amepewa zawadi ya
ng’ombe wa maziwa.
Katika hotuba yake na vyombo hivo
amewashukuru sana,kasha akasema anaondoka ikiwa watu bado wanampenda.
Aidha alisema anauhakika kuwa
vyombo vya Ulinzi na usalama vipo katika hali nzuri, vikiwa na zana za
kivita imara, kujenga Air Force imengwa,nyumba 10000 zinajengwa ikiwa nyumba 6,000 ni Askari wa kawaida
ambapo nyumba 4,000 ni za Mofisa wa ngazi za juu ,wakati na chini.
Jesha la polisi wanaletewa magari
ambapo mipango imesha fanyika Nchini India,magari hayo muda wowote yatawafikia
Jeshi la Polisi.
Magereza wao bado kupanga
mapendekezo yao,amewaambia wafanye haraka kabla hajaondoka aidhinishe ili
atakaye mpokea amkabidhi.
Alisema alichofarijika nalo ni la
Umoja wa vyombo vya Ulinzi na Usalama,Kuboresha maslahi ya watumishi wa Umma na
Vyombo vya Usalama.
Usipo wekeza kwenye vyombo vya
ulinzi na Usalama ,Unaweka rehani maisha ya wananchi,pamoja na ughali wake
lazima kuwekeza kwenye vyombo vya Ulinzi na usalama kwa usalama wa ulinzi wan
chi na watu wake.
Kama vyomba ulinzi na usalama ni
dhaifu mali zote zitahujumiwa bila kujua.Meli mbili zimeanza kulinda kwenye
bahari yenye kina kirefu.
Uimara wa uchumi wan chi lazima
ulindwe na Jeshi lake na uchumi ule lazima ulindwe kwa upanga.msipowekeza
kwenye ulinzi na usalama ,mabenki yote yataibiwa kila siku.
Alisema Dunia sasa inabadilika
kwa Sayansi na Teknolojia,lazima na majeshi yetu yafikie huko,Mf moi
kumenunuliwa mashine yenye thamani ya Dollar milioni 2, ili kuokoq mqisha ya
wananchi ,ukiogopa aghali huwezi kuokoa maisha ya wanachi.
Aidha alisema mwaka huu kuna
uchaguzi,vyombo vya ulinzi na usalama hasa Polisi,kuhakikisha upigwaji kura
unakuwa wa usalama ,hategemei kuwa kutakuwa na matukio ya kulishinda jeshi la
Polisi.
Anastaafu atarudi kuwa raia maarufu, Hawezi kwenda kuomba atoe
ushauri kwa Rais,maana Rais washauri wake. Akitaka ushauri ataenda kuomba
ushauri wa kulima mananasi yake,alisema Duniani hapa amefanya kazi kubwa ya
Urais.siwezi kuomba kazi,kwa manufaa ya nchi yake kama ataombwa ushauri
nitakuwa tayari.
Amesema kuwa walikuwa ndiyo nguzo
yake,mhimili wake,kama walivyo msaidia na kumshauri atakaye atayeshika
madaraka.kama walivyomshauri na nchi iko shwari.
No comments:
Post a Comment