Saturday, September 19, 2015

WASHABIKI ACHENI TABIA ZA KUCHANA MABANGO YA WAGOMBEA NAFASI MBALIMBALI ZA UONGOZI KATIKA UCHAGUZI MKUU UJAO HIVI PUNDE MWAKA HUU

Blogu hii imekuta baadhi ya wananchi katika Manispaa ya Dodoma wakilaani vikali kitendo cha kuchaniwa bango la mgombea ubunge wa Jimbo la Dodoma mjini kupitia CCM hivi karibuni nyakati za usiku,na kwamba kitendo hicho hakikuwapendezesha watu wenye hekima na busara zao mjini hapa.
.
Wanasema vitendo hivyo havina tija wala faida kwao na pengine watu hao hawajui thamani za vitu.Wanajiuliza walikuwa na tatizo gani na bango mpaka kulichana, wamesema mambo ya uchaguzi ni ya mpito tu baada ya hapo hali itaendelea kama kawaida,sasa aliyefanya kitendo hicho anapokutana na mgombea huyo atakuwa na amani moyoni mwake.

Aidha walisema vitendo hivyo havifai kama ndiyo ushabiki wa aina hiyo basi haufai kwakuwa ni vitendo vinavyo ashiria uvunjifu wa amani na upendo. katika Jamii ya Kitanzania na Duniani kote

Kufuatia kauli ya viongozi wa ngazi ya juu wa ulinzi na usalama wa mkoa huu,kwamba la kumtaka kila mwananchi akisha piga kura siku hiyo arudi nyumbani kwake kusubili matokeo,Kauli hiyo kwa watu kama hao inaweza kugonga mwamba kwa kutaka kubakia vituoni kusubiri matokeo.

Alisema watu  watakao kiuka agizo hilo asishangae kuona vyombo vya usalama vitapo mshughulikia kikamilifu maana atakuwa ameyataka mwenyewe kwa sababu ya ushabiki,hawajui ushabiki una weza kusababisha machafuko ya kupigwa na hata vifo vya kujitakia.Hivyo wenye tabia kama hizo waziache maana zita waletea wananchi kukosa amani kwa ajili ya watu wachache wasiye taka kusikia.

1 comment:

  1. Nimesoma malalamiko kutoka sehemu zingine za nchi kuhusu uharamia huo. Mabango ya vyama mbali mbali yanachanwa, sio ya CCM tu, sio ya UKAWA tu. Ni utovu wa ustaarabu, utovu wa kuheshimu uhuru na haki za wengine.

    Kila binadamu ana haki na uhuru wa kuwa na maoni yake, haki na uhuru wa kujieleza, iwe ni kwa maandishi, mazungumzo, hotuba, au mabango. Jamii yetu inapaswa kuona aibu kwa hujuma zinazofanyika.

    ReplyDelete