Tuesday, November 6, 2012

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI – MAMLAKA YA MAPATO MKOA WA RUVUMA. • Yafanya Maadhimisho ya sita ( 6 ) ya siku,wiki ya Mlipa kodi tarehe 7/11/2013 Mkoani Ruvuma ( Kauli Mbiu ni “ ULIPAJI KODI WA HIARI KWA TAIFA LENYE MAFANIKIO.”) • Mlipa kodi anao mchango kubwa katika mafanikio ya TRA.

 Meneja wa TRA Mkoa wa Ruvuma Bwana Apili Mbaruku akitoa taarifa ya Mamlaka ya TRA Mkoa wa Ruvuma leo kwenye ofisi yake kwa waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kuhusu maadhimisho ya siku ya mlipa kodi yatakayo fanyika kesho.katika Manispaa ya Songea.
 Afisa Elimu kwa Mlipa kodi Bw.Mefti Jackson wa Mamlaka ya TRA Mkoa wa Ruvuma ,ambapo kwa ushirikiano na Timu nzima ya Mamlaka ya TRA mkoani humo ,wameweza kuwapatia leseni za udereva waendesha yeboyebo na madereva wa magali.
 Waandishi wa habari wakimsikiliza Meneja wa TRA Mkoa wa Ruvuma Bw.Apili Mbaruku,ofisini kwake
Watumishi wa TRA .
 Waandishi wa TBC na Channel Ten
Bwana.Juma Nyumayo wa kwanza mwenye kitabu akielezea jins Mamlaka hiyo ilivyo fanikiwa katika utoaji wa leseni kwa Yebo yebo.


MAMLAKA ya mapato Tanzania inatambua na kuwapongeza walipa kodi wote kwa mchango wao mkubwa katika mapato ya Serikali kwa mafanikio ya Taifa,ambapo lengo la Mamlaka ni kuimarisha utendaji wa kazi katika kuongeza makusanyo ya kodi na kuboresha huduma kwa walipa kodi wote.

MENEJA wa TRA Mkoa wa Ruvuma Bwana Apili Mbaruku, akisema hayo wakati akiongea na  waandishi wa vyombo mbalimbali wa Mkoa wa Ruvuma ofisini kwake leo,na kwamba katika maadhimisho hayo kutatolewa mafunzo ya kodi kwa walipa kodi kwa mtindo wa kuuliza maswali na majibu kwa wadau wao.

Mamlaka ya TRA inategemea kutoa msaada wa magodoro 12   kwenye Ward ya watoto katika Hospitali ya Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma yenye thamani ya shilingi laki nane ( sh.800,000/= ).

Aidha Bw. Mbaruku alisema kuwa Mamlaka ya TRA Mkoani Ruvuma, katika mwaka wa fedha wa 2011/2012,ilikusanya kodi kwa kiwango cha asilimia 109.5 % kwa kodi za ndani na asilimia 96 % kwa kodi ya Forodha.

Kuhusu kodi za ndani ililenga kukusanya shilingi bilioni 5.001/=,badala yake ikavuka malengo kwa kusanya shilingi bilioni 5.476/=,ambapo kodi ya Forodha ilifikia malengo kwa kukusanya shilingi bilioni 223.8/= kama ilivyolengwa kukusanya na kwamba makusanyo halisi yalikuwa zaidi kwa asilimia 31 % ya makusanyo halisi ya mwaka wa fedha wa 2010/2011.

Alisema kuwa katika kuboresha wa ukusanyaji kodi kwa njia ya vitalu,Mamlaka ya TRA mkoani Ruvuma imeweza kuandikisha walipa kodi zaidi ya 1,094 kwa mwaka wa 2011/2012 ,ni pamoja na utekelezaji wa Mpango Mkakati wa tatu ulioanza mwaka 2008/2009 na kuendelea mwaka 2012/2013.

Kama mpango huo ulivyoanishwa,mkoa wa Ruvuma umewekewa mtandao wa leseni za udereva uliyowezesha makusanyio ya shilingi milioni 424.2/= na leseni zaidi ya 8,500 zilizotolewa mpya au kubadilishwa.

No comments:

Post a Comment