Friday, November 2, 2012

HUDUMA YA MAFUTA AINA YA PETROLI NA DIZELI KATIKA MANISPAA YA SONGEA BADO INAENDELEA KUWA MBAYA ZAIDI KAMA UTAKAVYOONA FOLENI YA MAGARI NA PIKIPIKI KUELEKEA KWENYE KITUO CHA KISUMA PAI FILLING STATION

LEO katika Manispaa ya Songea pamoja na kuwa na foleni kubwa/ndefu ya magari na pikipiki kuelekea kwenye kituo cha Kisumapai Filling Station kupata huduma ya mafuta,lakini pia kulikuwa na mvua,lakini watu hawakujali hiyo mvua ili mradi wapate huduma hiyo.

 Hiyo ni foleni ya magari kuelekea kwa Kisuma Pai Filling Station,kituo peke yake katika Manispaa ya Songea ndiyo kinatoa huduma hiyo adimu kwa wenye vyombo vya usafiri.
 Hiyo nayo ni foleni ya pikipiki ambayo imeanzia mbali ikiwa ni foleni ya pikipiki na magari kuelekea Kisuma Pai filling Station kupata petroli na dizeli Leo katika Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.
Manispaa ya Songea ina vituovingi vinavyouza mafuta lakini ni kimoja tu ndicho kinacho uza mafuta,cha Kisuma pai Filling Station,kwa hivyo foleni ya magari na pikipiki zinakuwa ndefu kwenye kituo hicho cha kuuzia mafuta mjini hapa.

No comments:

Post a Comment