Thursday, June 28, 2012

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA ASIKITISHWA KITENDO CHA KINYAMA KILICHO FANYWA NA WATU WALIYEMSHAMBULIA DAKTARI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda ameliambia Bunge wakati akijibu maswali ya papo kwa papo kutoka kwa waheshimiwa wabunge leo ,kuwa serikali imesikitishwa na kitendo cha watu waliyehusika katika kumshambulia Daktari hadi kumsababishia maumivu katika mwili wake.
Amesema anamuombea Mungu  ili aendelee vizuri na kwamba uchunguzi unaendelea wa kupata watu waliyehusika na tukio hilo.
Kuhusu mgomo wa madaktari Pinda amesema kuwa serikali iko katika harakati za kutafuta waganga kutoka katika taasisi mbalimbali ili kuokoa maisha ya wagonjwa walioko katika hospitali ambazo madaktari wake wako katika mgomo mkiwemo Madaktari maaskari pamoja na wale waliostaafu ,wakati serikali ikifanya taratibu za suluhu kufuatia mgomo wa madaktari.

No comments:

Post a Comment