Tuesday, June 26, 2012

OPERESHENI ya polisi Ruvuma yashika silaha 17,Risasi,madwa ya kulevya na pombe haramu.

RPC Ruvuma kamishina Msaidizi Deusdedit Nsimeki akiwaeleza waandishi wa habari mafanikio ya Operesheni iliyoendeshwa na Polisi ambayo silaha 17 zimekamatwa,risasi,pombe haramu madawa ya kulevya pamoja na wizi na unyang'anyi wa kutumia silaha na wizi.
 Kamanda akijibu hoja na mwaswali kutoka kwa waandishi.
Baadhi ya waandishi wakitafakali jinsi Operesheni kamata silaha ilivyofanikiwa.
Kamanda,Gerson Msigwa TBC katikati na Mosesi Konara kulia wakisikiliza maoni na usahuri kutoka kwa waandishi hao leo.


KAMANDA wa Polisi Mkoa Ruvuma Kamishina Msaidizi Deusdedit Nsimeki ameaambia waandishi wa habari katika ukumbi wa Polisi mkoa leo kuwa,silaha 17  zimekamatwa zikiwemo short gun  3,na  Rifle 3 magobole 11, pamoja na risasi na kesi 7 za watuhumiwa ziko mahakamani.
  Aidha Kamanda Nsimeki alisema katika Operesheni hiyo,kesi 10 zilizohusisha bangi ziko mahakamani ,pamoja na kesi za pombe haramu ya gongo lita 60.5 zilizokamatwa zilizowahusisha watuhumiwa wauzaji na wanywaji wa pombe hiyo.
    Nyingine na unyang’anyi wa kutumia nguvu kesi moja na unyang’anyi wa kutumia silaha watuhumiwa 12, kati yao 6 wapo mahakamani ,pamoja na wizi wa diseli,nondo 147  za kutengenezea madaraja, zilizosadikiwa kuibwa kwenye kampuni ujenzi wa barabara, Pia wizi wa mbuzi 7 na kesi yake ipo mahakamani ikiwa ni pamoja na uzururaji mitaani bila kazi maalumu
    Kamanda Nsimeki ametoa wito kwa wananchi wa mipakani kuacha kutumia silaha wanazozimiliki kisheria  kuazimisha kwa watu ambao hawajui matumizi yake kama ni ya uahalifu au la.Alisema zoezi la kusaka silaha zinazotumiwa kinyume cha sheria linaendelea ikiwa ni zoezi endelevu.

No comments:

Post a Comment