Wednesday, June 27, 2012

MADAKTARI WAMRUDIE MUNGU WAO WAACHE MGOMO MAANA WANAO ATHIRIKA NA WANANCHI WASIO NA HATIA WALA UWEZO WA KUWATIMIZIA MADAI YAO.

Wakati Daktari Jijini Dar es Salaam yuko ICU kwa kupigwa na watu wasiyejulikana, Madaktari wa hospitali ya Mkoa Songea nao wako katika mgomo baridi wagonjwa wamefurika  hosipitalini hapo bila msaada.
   Lakini hawa walikula kiapo kuwa watalitumikia taifa kwa uwezo wao wote, ambao wamechukua dhamana ya maisha ya wananchi wa nchi hii, Lakini wamesahau kuwa walikula kiapo cha utii kwa taifa.
  Pia Serikali nayo ifikie mahali iwatekelezee madaktari hao na watumishi wengine wa kada mbalimbali wanao dai maslahi yao ili kuepusha dhahama zinazotokea kwenye migomo, halafu haipendezi ni aibu kwa nchi yenye serikali sikivu  ifike mahali serikali isema sasa migomo basi,  na inawezekana.

No comments:

Post a Comment