Thursday, June 21, 2012

Serikali mkoani Ruvuma inampango wa kuwakopesha wakulima ili waachane na jembe la mkono

Bwana Mwambungu amewaambia waandishi wa habari kuwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma ni wazalishaji wazuri wa zao la mahindi kwa kutumia jembe la mkono,na kama watatumia Matrekta na kuliacha jembe la mkono wazalisha mara dufu.
Kwa hiyo Serikali ya Mkoa huo itawapelekea wananchi matrekta ya kukopesha wakulima,maana msimu huu mahindi ni mengi yatauzwa na kubakia na ziada kwa chakula chao ,mkoa umetimiza kaulimbiu ya kilimo kwanza kwa vitendo.

No comments:

Post a Comment