Thursday, June 14, 2012

VIONGOZI NA WATENDAJI WAWAJIBIKE KIKAMILIFU KWA WANANCHI –MKUU WA WILAYA YA SONGEA

 Mkuu wa Wilaya ya Songea Bwana Joeph Joseph Mkirikiti akizungumza na waandhi wa habari ofisni kwake leo.Mjini Songea.
 Bwana Mkirikiti akiwaonyesha waandishi wa habari daftari la wakulima wa Manispaa ya Songe Mjini Magharibi lililo andaliwa na Mkuu wa Wilaya aliyestaafu Bw.Thomas Sabaya.na yeye anaanda dafutari la wafanya biashara wa manispaa ya Songea.
Waandishi wa habari wakiwa ofisini kwa mkuu wa Wilaya wakimsikiliza mikakati aliyoiweka ya viongozi na waendaji kuwajibika,maana uwajibikaji ni ngao ya maendeleo ya wananchi.
Waandishi wako makini kumsikiliza mkuu huyo leo ofisini kwake.





MKUU wa Wilaya ya Songea Bwana Joseph Joseph Mkirikiti ametoa rai kwa viongozi na Watendaji wa Serikali kuwajibika kikamilifu kwa wananchi ambao wao wanawalipia mishahara,na kwamba waache kufanya kazi kwa mazoea.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ambao leo kuwa  rai hiyo ameshaitoa kwa watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea na Halmashauri ya Songea Vijijini na hatimaye ataongea na waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri zote mbili za Halmashauri ya Manispaa ya Songea na Halmashauri ya Wilaya ya Songea Vijijini..
         Bw.Mkirikiti alisema kuwa  wananchi wa Manispaa,Songea Vijijini na Mkoa mzima kwa jumla watumie fursa zilizopo katika kuwaondolea umasikini wa kipato kwani kutokana na takwimu za mkoa mwaka 2006 ,kipato cha mwananchi wa Songea ni Tshs, 156,000/= kwa mwaka.ambacho hakitoshelezi mahitaji ya mwanachi huyo.
        Aidha alisema wakitumia fursa hizo watazalisha zaidi watauza mazao yao ambapo watapata fedha zitakazo inua misha yao.Na kwamba yote hayo hayawezi kufanikiwa iwapo uwajibikaji utakuwa haufanyiki kikamilifu.
       Kutokana na hilo mkuu huyo amewsihi  watendaji hao wawajibike kwa wananchi katika kujibia kero zao  mbalimbali zikiwemo zinazohusiana na ardhi na wala wasigeuke kuwa madalali wa ardhi.
    Kuhusu changamoto zilizopo katika Wilaya zake, alisema zimeshaanza kushughulikiwa zikiwemo za umeme, ambao ulikuwa haueleweki vizuri lakini sasa upo katika hali nzuri,lakini alichokiona kuwa ni tatizo la uwajibikaji kwa watendaji wa “Tanesco” wa kufanya kazi kwa mazoea.
     Ametoa wito kwa vijana kutumia fursa ya Boda ya Msumbiji kwa kufanya biashara za mipakani,na kufanya bishara zao ndogondogo katika maeneo yaliyoruhusiwa badala ya kupanga barabarani na kuwa kero katika Manispaa.


No comments:

Post a Comment