Tuesday, October 19, 2010

WAKAZI WA MJI WA SONGEA HAWAPO NYUMA KWA KUJICHANA KWA VINYWAJI BARIDI,KUNA USEMI USEMA UKITAKA KUJUA NGUVU ZA MLEVI UMWAGE POMBE YAKE,SASA UKITAKA KUZIJUA NGUVU ZA MNYWA SODA UFANYE NINI?

Jumanne ya leo nilipo shuhudia Lori lililojazwa makasha matupu ya vinywaji baridi aina ya Coca Cola ,liloshambuliwa na wauzaji wa vinywaji hivyo katika mji wa Songea,karibu na baa za vinywaji vikali maarufu kwa jina la bia maeneo ya Standi ya mabasi yaendayo nje ya mkoa wa Ruvuma ,vijana wakitupia na makasha hayo kama mpira wa kikapu bila kuangusha.

Ilikuwa inafurahisha lakini wao ni ajira wala siyo mchezo,mwingine kajaribu kama hukupata kesi na mwenye kampuni ya soda au utozwe faini.Kazi ni kazi bwana usidharau kazi za watu ndizo zinazo wapa umaarufu.Hata hao wanao dai kuwa wakichaguliwa watatoa ajira,hazitakuwa tofauti sana na hizo.kwa hiyo tuheshimu ajira za watu.

Lakini kando kulikuweko na wateja wengine wakijiburudisha kwa soda,kutokana na jua kali liwakalo katika mji wa Songea lakini hautoki jasho,matokeo yake unazidi kuwa mweusi,lakini Dar,joto na jasho mtindo mmoja, mambo haya jamani yanafurahisha kweli.

No comments:

Post a Comment