Rais Jakaya Kikwete kaendelea na kampeni za kuwania kuendelea Ikulu kwa kutoa ahadi kuwa ndani ya miaka mitano ijayo :-
- Barabara ya Njombe Songea itafanyiwa ukarabati wa hali ya juu kwa kuwa barabara hiyo imeanza kuchoka.
- Kujenga chuo cha waganga Mjini Songea mipango imesha andaliwa.
- Kuunganisha barabara kwa kiwango cha lami Mtwara hadi Mbamba – Bay.
- Kuboresha kilimo kwa kuongeza pembejeo.
- Kuleta vitabu vya masomo ya Fizikia,Kemia na Biology katika shule za sekondari nchini.
- Kuboresha huduma za afya.
Alisema Iani ya CCM ya mwaka 2005 imetekelezwa kwa kiwango cha juu katika sekta zote,kwani CCM ni chama dume tena dume la mbegu.alisema Ukarabati mkubwa umefanyika katika hospitali ya Mkoa.mahindi ya wakulima yatanunuliwa fedha zipo,pia wameruhusiwa kuuza mahindi nje ya nchi ila waweke akiba, yote hayo ni mchakato wa Ilani ya CCM ilivyo utekelezwa katika miaka mitano ya uongozi wa Dk Jakaya Kikwete.
Alisema tatizo la marelia vyandalua vyenye dawa vipo kwa kina mama,hivyo waume zao watanufaika na vyandarua hivyo.Hata hivyo alisema tatizo la UKIMWI bado ni kuwa kwani hakuna chandalua cha kuuzuia.Dawa ni kuacha au kutumia kinga.Tanzania bila UKIMWI inawezekana kama mtafuata maagizo ya viongozi wa Dini ,viongozi wa siasa na kufuata ushauri wa wataalamu wa afya.
Aidha alimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Songea mjini Dk Emanueli Nchimbi,ambaye kama mbunge wa jimbo hilo,amejenga shule ya sekondari Mkuzo ya kidato cha tano na sita,ameezeka bati shule za manispaa ya songea,amejenga barabara tatu kwa kiwango cha lami na manispaa na ya nne ni kutoka Makambi hadi mjini.
Dk Emanuel Nchimbi akielezea mafanikio ya ilani Ya CCM ya mwaka 2005 kwa mambo mengi ya maendeleo aliyoyafanya katika manispaa ya Songea zikiwemo barabara tatu za lami na ya nne inatarajiwa kumalizika hivi karibuni,kuboresha majengo ya shule za msingi na kujenga shule ya sekondari ya Mkuzo.ya kidato cha tano na sita.
No comments:
Post a Comment