Leo ni kumbukumbu ya miaka 11 tangu Baba wa Taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere kututoka,kwa niaba ya Kurugenzi ya Elimu ya Watu Wazima na Nje ya Mfumo Rasmi kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,kutanamkumbuka Baba wa Taifa kwa kuanzisha kisomo chenye manufaa.kwa lengo la kupambana na maadui ujinga,maradhi na umasikini.
Mwaka 1965 Tanzania ilikuwa na madarasa 7,257 yakiwa na watu wazima 541,562 mkiwemo wanaume 206,214 na wanawake 335,345,pia kulikuwa na madarasa ya kujifuza kiingereza na hesabu 14,043,vikundi 1,914 vya wanawake 112,739 waliyojishughulisha na mapishi,ushonaji,ufumaji na utunzaji wa watoto.
Katika miaka ya mwanzoni baada ya Uhuru Baba ya taifa alianzisha Eilumu ya Watu Wazima,chini ya Wizara ya Elimu ya Taifa na kuunda idara ya Elimu ya Watu Wazima nakuteuliwa Mkurugenzi Masaidizi wa Elimu ya Watu Wazima Novemba 1969.
Pamoja na mambo mengine Mwalimu Nyerere aliyazungumzia sana masuala ya Umoja wa nchi za Kiafrika,uongozi bora,uchumi,rushwa,Jumuiya ya Afrika Mashariki na Vijana ambao ndiyo nguvukazi ya taifa.
Kituo cha Mradi wa Magazeti vijijini Kanda ya Kusini TUJIFUNZE na wafanya kazi wote wanamkumbuka Mwalimu Nyerere siku ya leo,wakiwemo ndani ya Kurugenzi ya Elimu ya Watu Wazima na Nje ya Mfumo Rasmi na Mkurugenzi wake Bwana Salum Mnjagila katika Serikali ya awamu ya nne ikiongozwa na Rais Jakaya Kiwete ambaye ameirudisha Kurugenzi hiyo.
Kurugenzi ya Elimu ya Watu Wazima imekuwa kitengo kwa muda mrefu chini ya Afisa elimu kiongozi na kuwa na Mkurugenzi Msaidizi Bwana Salum Mnjagila.Kwa kumuenzi Baba wa taifa Tunamshumuru Rais Jakaya Kikwete kwa kuyaendeleza yale mazuli aliyoyaanzisha Mwalimu Nyerere na Waziri wa Elimu Prf.Jumanne Maghembe,Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima na nje ya Mfumo Rasmi Bw.Salum Mnjagila katika harakati za kupambana katika kufuta ujinga nchini.
Aidha kwa niaba ya vituo 7 vya Kanda vya magezeti vijijini tunamombea Baba wa Taifa aendelee kuwa mwenye Heri na Mungu ailaze Roho yake mahali pema peponi.Kutokana na kampeni ya elimu ya watu wazima ndipo vituo hivi viliaanza.
Mwaka 1974 Januari toleo la kwanza la Gazeti la Kanda ELIMU HAINA MWISHO la kisomo lilitolewa,mwaka 1979 magazeti mawili ya kisomo ya Kanda ya TUJIELIMISHE Kanda ya Kaskazini na TUJIENDELEZE Kanda ya mashariki.
Mengine ni magazeti matatu ya kisomo ya TUJIFUNZE Kanda ya Kusini,NURU YETU Nyanda za Juu Kusini,na ELIMU YETU Kanda ya Kati yalianzishwa Julai mwaka 1980.Dhamira ilikuwa kutoa elimu kwa kujali makundi yote yakiwamo ya watu wazima ambao walikuwa wengi hawajui kusoma,kuandika na kuhesabu baada ya Uhuru.
Lakini leo nchini kuna zaidi ya asilimia 30 ya watu wazima hawajui kusoma,kuandika na kuhesabu si ajabu kwa kuwa wengi waliodhani wamejua na wakasahau kama kuna kusoma vitabu wamerudia tena hali ya kutijua kusoma.
Tena vijana wengi walioacha shule kwa sababu tofauti zikiwemo za ufataki,wakuhonga pipi na chipsi watoto wa wenzao,wanawake wakubwa wanawakimbia wakiwaangalia walivyo jipangilia wanaona ghali na kukimbilia rahisi,kumbe ubahili wao ni hasara kwa taifa letu.kwa hiyo elimu ya watu wazima itaendelea,bado kuna wanaoingia kidato cha kwanza hawajui kusoma,hawa watakuwa wapi?.
Kila mtu anahitaji elimu ya watu wazima hata awe na shahada kibao,hawezi kujua kila jambo,sasa siku akitaka kujua jambo ambalo halijui kwa mtu mwingine,basi hiyo ni elimu ya watu wazima.Hivyo ni kweli kwamba wasomi wote wanajua kuitumia Computer sawasawa ? au wasomi wote wanayajua masomo yote?,basi kama hapana,siku akitaka kujifunza chochote asicho kijua wakati akiwa shuleni basi huyo atakuwa kwenye elimu ya watu wazima.
No comments:
Post a Comment