Tuesday, October 19, 2010

DKT.NCHIMBI AENDELEA KUNADI SERA ZA CCM MISUFINI LEO KATIKA MANISPAA YA SONGEA,,KUWA TAREHE 31 MWEZI HUU SIKU CHACHE KUANZIA SASA WANANCHI WACHAGUE MAENDELEO, WACHAGUE VIONGOZI WATAKAO WALETEA MAENDELEO, NA KATIKA KATA YA MISUFINI WAMCHAGUE ELIZA NGONGI KUWA DIWANI WAO NA SIO MFA MAJI MAANA MFA MAJI HAACHI KUTAPATAPA.

 Dkta Emanuel Nchimbi anayetetea kiti chake cha ubunge jimbo la Songea Mjini kwa Tiketi ya CCM amemnadi mgombea uduwani wa kata ya Misufini Songea mjini Bibi Eliza Ngongi ambaye alikuwa naibu Meya wa Halmashuri ya Manispaa ya Songea,Nanatetea nafasi yake ya udiwani ambapo anagombea nafasi hiyo na mgombea kwa tiketi ya CHADEMA Bwana Mfamaji.Bibi Ngongi ni  msomi wa Shahada ya biashara amea ahidi mambo kadhaa.
 Ameyataja mambo hayo kuwa ni pamoja na kuboresha miundo mbinu ya barabara,Soko la manzese,maji safi na salama,bishara ndogondogo kwa akona mama.(Source Christian Sikapundwa)
 Dkt Nchimbi Mbunge na Eliza Ngongi waliye inamiana wakitetajambo kabla ya kwenda kusalimia wananchi waliye kwenda kwenye kampeni ya ubunge na Udiwani leo Katika manispaa ya Songea kata ya misufini.
Naibu Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea anaye wania Udiwani katika kata ya Misufini akimsikiliza kwa makini Mhe.Dkt Emanueli Nchimbi hayupo kwenye picha.Wakati akimsifia mgombea wa udiwani katika kata hiyo Bw.Mfamaji kuwa ni mtu mpole,mwenye unyenyekevu,msikivu na mwenye kuelewa watu wanahitajinini kutoka kwake.

Alisema Bw.Mfamaji yeye anajua hawezi kushinda udiwani katika kata hiyo,hivyo uchaguzi ujao atahamia kata nyingine,sifa hiyo kwake imemjenge sifa ya kuhama hama kata baada ya kushindwa katika chaguzi za udiwani.Lakini majina mengine yanaweza kuashiria jambo kuwa zuri kwake au baya kwake.Sasa mfa maji jamani haachi kutapatapa.ndiyo maana uhama kata hii kwenda kata nyingine baada ya kushindwa.( Source Christian Sikapundwa)

No comments:

Post a Comment