Monday, October 11, 2010

MAFIGA MATATU SI NENO GENI MASIKIONI KWA WENGI JE HAYO...

MAFIGA MATAU UNAYAJUA ? WAULIZE WAENDESHA KAMPENI

Wakati kampeni za Urais ,Ubunge Udiwani na Viti maalu zikiendela majimboni,utapata semi kemkem moja wapo ni  ya mafiga matatu,mafiga ni mawe,tofali au udongo uliyotengenezwa kwa shughuli mahususi za upishi kuinjika sufuria la wali au ugali,chungu cha mboga wali au ugali,lakini wataalamu wa lahaja za Kiswahili watakueleza vizuri.

Katika harakati za kuwini chochote lugha kadhaa zitaibuka ili ushindi upatikane,basi usemi huo ulidhirishwa pale Mgombea Urais Dk Jakaya Kikwete alipo onyeshwa hayo mafiga matatu na sufurika kubwa ikiwa juu yake kama unavyoiona kwenye picha hiyo hapo chini, kabla hajahutubia wananchi katika uwanja wa majimaji mjini Songea kunadi Sera za CCM hapo jana.

Ujumbe wa mafiga matatu kwa hapa katika jimbo la Songea mjini ! figa moja ni la Dk Kikwete,figa la pili ni la Dk Nchimbi na latatu ni Ngongi,hii ninamaana tarehe 31 mwaka huu. Watu wachague mafiga matatu  ya CCM.

Ni kwamba figa la kwanza wamchague Rais Kikwete,figa la pili wachague wabunge wao wa CCM na la tatu wachague Madiwani  wa CCM.Habari ndiyo hiyo.lakini mafiga hayo kwenye picha yametengenezwa na mchwa yapo katika urefu unaofanana na unene unaofanana.

No comments:

Post a Comment