Wednesday, October 20, 2010

VIJANA BAADA YA KUGUNDUA KUWA AJIRA IMEKUWA NI MAZUNGUMZO MAJUKWAANI KARIBU NCHI NYINGI DUNIANI,KUNA BAADHI YA VIJANA WAGUNDUA AJIRA YA CHAPCHAP HUKO NCHINI KENYE AJIRA GANI HIYO ENDELEA NA ‘FILER’ HAPO CHINI

BAADHI ya vijana nchini Kenya wamebuni ajira ya harakaharaka baada ya kuona ajira imekuwa wimbo wa majukwaani hasa kipindi cha chaguzi mbalimbali za uongozi duniani.

Kwa taarifa ya Wanyama Kibusire wa Kenya zinasema amekutana na vijana hao wakiwa katika ajira hiyo ambayo wanasema inawapa Dollar 7 za Kimarekani baada ya kumaliza kazi ambayo wamepangiwa na mwajiri wao,Siku hiyo hiyo.

Alisema vijana hao na wananchi wa Kenya wamoena njia rahisi ya kuemboleza msiba ndugu yao akifariki na kuajiri vijana kufika kuwalilia kuanzia chumba cha maiti,hadi nyumbani kwa mfiwa,walilia vijana hao wa ufundi mkubwa wakati wengine wakiomboleza kwa nyimbo za sala kama watakuwapo.

Ingawa baadhi ya madhehebu ya dini yamekipinga sana kitendo hicho,lakini vijana hao walisema ajira hakuna,kama kuna watu ambao hawana uwezo wa kuomboleza kwa kulia kwanini wao wasifanye kazi hiyo ambayo inawapa ujira.

Lakini kama kuna ajira ya kutengeneza masanduku ya kuzikia watu ambapo watu wenyewe hawajulikani watakufa lini  na kifo kipi na wapi wameruhusiwa kufanya hivyo sasa kwanini vjiana mabingwa wa kulia kwenye msiba wasiajiriwe?.Kazi ni kazi tusije tukadharau kazi za watu tutakuwa hatuwatendei haki.

No comments:

Post a Comment