Monday, October 18, 2010

MKULIMA BADO HANUFAIKI NA KILIMO CHAKE ANAYE NUFAIKA NI MAFANYA BIASHARA ANAYEFUATA MAZAO VIJIJINI KWA WAKULIMA

 Hiyo ni shehena ya mahindi inayosafirishwa nje ya mkoa wa Ruvuma yaliyo nunuliwa na wafanya biashara kwa bei ya hasara,ukilinganisha na gharama walizotumia katika kilimo.Je mkulima huyu atakuja fanikiwa siku moja?.Anauza kwa bei ya hasara siyo kwa kupenda,kutokana na matatizo yakiwemo ya usafiri kufikisha mazo yake kwenye soko.Shehena ambayo ilitaka kukuta nyaya za umeme wakati likipita  lori hilo leo mjini Songea. ( picha na Christian Sikapundwa)

 Ruvuma inavuma kwa mazao mbalimbali,ya chakula na biashara yakiwemo kahawa,tumbaku,na korosho,kwenye chakula ni mahindi ,mpunga lakini kuna magarage ambayo unayaona yamerundikana chini yakingojea wa laji,aliyeumia hapo ni mkulima anae uza kwa hasara kwa wafanya biashara,wangekuwa na soko la uhakika wangenufaika na wao.
Magunia unayoyaona ni mahindi na maharage katika soko la SODEKO katika manispaa ya Songea wanasubiri kwenda kuya uza katika ghala la serikali Ruhuwiko kwa bei ya sh.300/=  kwa kilo wakati wao kwa wakulima wameyenunua kwa sh.150 /= kwa kilo.Je nani mjanja kati ya mkulima na mfanya biashara ?. ( Picha na Christian Sikapundwa)

No comments:

Post a Comment