Wednesday, November 2, 2011

WANANCHI WAKISHIRIKI KWENYE KISOMO WATALETA UKOMBOZI KATIKA USAFI WA MANISPAA YA SONGEA – MEYA

 Mstahiki Meya Charles Mhagama  akikagua kazi za wanavikundi
 Akikagua moduli za masomo kutoka Taasisi ya elimu ya watu wazima Kituo cha Songea
 Mheshimwa Mhagama wa kwanza mwenye makaratasi  akisikiliza shauri
 Kazi za mikono za wnakikundi cha Majengo
 Asha Tembo na Annamary Komba wakisoma shairi wanakisomo wa kujiendeleza kutoka majengo
Afisa eilu ya watu wazima Manispaa ya Songea Bwana Nathaniel Yonas akisoma taarifa ya elimu ya watu wazima ya manispaa ya Songea.

MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Songea Mhe. Charles Mhagama  amesema kuwa wananchi wa Manispaa ya Songea wakishiriki kikamilifu kwenye vikundi vya kisomo vya MUKEJA  na VICOBA watakuwa ukombozi wa mabadiliko ya usafi katika Manispaa yake.
Mheshimiwa Mhagama alisema hayo kwenye hotuba yake ya wiki la elimu ya watu wazima kiwilaya iliyomwa kwa niaba yake na Mheshimiwa Iddi Abdalah Diwani wa majengo, baada ya kukagua maonyesho kadhaa yaliyo wekwa na vikundi mbalimbali ya kisomo na uzalishaji mali katika viwanja vya shule ya msingi Majengo Manispaa ya Songea.

Sherehe huzo ziliandamana na Risala,Ngojera,michezo ya kuigiza na ngoma ya Lizombe ya kikundi cha Jakaya Mrisho Kikwete cha Lizaboni kinachoongozwa na Mzee kajogolo.



No comments:

Post a Comment