Friday, November 25, 2011

Maandamano ya siku 16 za kupinga ukatili duniani,ukatili wa jijinsia dhidi wanawake kanda ya Kusini na Nyanda za Juu Kusini

 Hayo ni maandamano ya kupinga ukatili duniani, maadhimisho hayo yatakuwa kwa siku 16 kuanzia leo ,ambapo leo wananchi,wanafunzi Katika Manispaa ya Songea wameandamana kuzuia ukatili wa kijinsia na dhidi ya wanawake Kanda ya Kusini na Nyanda za Juu kusini katika Manispaa ya Songea.
 Maandamano hayo yalianzia Ofisi ya CCM Mjini ,Kauru,Polisi,yakapandisha hadi Makumbusho ya Taifa ya Majimaji yaliyoko maeneo ya Mahenge Manispaa ya Songea.
 Maandamano hayo  yaliongozwa na bendi ya shule ya msingi,mabango mbalimbali ya kupinga ukatili wa kijinsia.
 Hayo ni baadhi ya maandamano yaliyoanza kuwasili katika uwanna wa Makumbusho ya taifa ya majimaji mjini Songea leo.
 maandamano katikati ya miji wa Songea leo.
Maandamano ya wanafunzi yaliyo karibia katika Makumbusho ya Majimaji leo.

No comments:

Post a Comment