Friday, December 31, 2010

Sunday, December 26, 2010

JUMAPILI YA FAMILIA TAKATIFU ILIKUWA KAMA HIVI LEO KETU

 Mr & Mrs Christian Sikapundwa baada ya kutoka kwenye ibada ya Christmas nyumbani kwao Dodoma
 Familia ya Sikapundwa wakiwa nyumbani kwao wakipata chakula ikiwa ni ukamilishaji wa sikukuu ya Christmas
 Kaka yake Mkubwa Bw.Sikapundwa Mzee Ally wa Kimamba Kilosa wakiwa katika kusheherekea Christmas.
 waumini wa Kanisa la makole Manispaa ya Dodoma wakiangalia pango alipozaliwa Yesu Kristu katika zizi la wanyama.
Familia ya Sikapundwa baada ya chakula cha Christmas nyumbani kwao Uhindini,karibu na Makole Mjini Dodoma.

HERI YA CHRISTMAS NA MWAKA MPYA KWA WATU WOTE ,PAMOJA NA FAMILIA TAKATIFU LEO

 Hilo pango ni kiwakilishi cha eneo la zizi la wanyama ambapo Yesu Kristu alizaliwa mahali duni,ili kutimaza ahadi ya kumkomboa mwanadamu
 Baaada ya ibada ya mkesha wa Christma,waumini wakionekana wakitoka katika ibada ya kwanza katika kanisa la Parokia ya Makole katika manispaa ya Dodoma.
Hiyo ni kwaya ya ibada ya asubuhi iliyo imba katika misa  hiyo Christmas katika kanisa la Parokia ya Makole Mjini Dodoma.

Saturday, December 25, 2010

MERRY CHRISTMAS AND HAPPY NEW YEAR OF 2011

The Rural Press staff wishes the all Bolger's readers  merry Christmas and  a happy beginning of new year 2011.And God will bless you and your family.

Thursday, December 23, 2010

MHESHIMIWA DIWANI MFAMAJI KUPITIA CHADEMA KATA YA MISUFINI AMEPATA SINTAFAHAMU PALE OFISI YAKE ILIPO CHOMWA MOTO NA WATU WASIOJULIKANA

Diwani wa kata ya Misufini katika Manispaa ya Songea Bw. Mfamaji amejikuta katika hali ya sintafahamu  pale alipo kuta ofisi yake ikiteketea kwa moto,pamoja na nyaraka zake muhimu za kufasnyia kazi.

kwa mujibu wa watu walioshuhudia ofisi hiyo ikiteketea kwa moto na kujaribu kuisalimisha na kushindikana,walisema chanzo cha moto huo bado hakijajulikana,bali watu wasiojulikana ndio waliosababisha moto huo.labda kwa chuki zao zilizo wafanya kutimiza tendo hiho la fedhea,katika jamii yenye watu wenye akili wanaokubali ushindani ni kitugani.

Tuesday, December 21, 2010

POLISI WATEMBEZA MKONG'OTO NA MABOMU YA MACHOZI WA WASOMI WA CHUO KIKUU CHA DODOMA ( UNIVERSITY OF DODOMA ) UDOM KWA MADAI YA FEDHA ZA FIELD

 hayo ni baadhi ya majengo yaliyojengwa ya Chuo Kikuu cha Dodoma kulingana vitivo mbalimbali
 Uzuri wa majengo pekee haumtoshelezi mwanafunzi kufanya vyema katika masomo yake ya miaka mitatu au mnne na zaidi iwapo hatapatiwa mahitaji muhimu ya kufanikisha maendeleo ya masomo yake ikiwepo,research,pamoja na field  mbalimbali .Iwapo  hatapata mahitaji hayo wakati akiwa katika  harakati za kutafuta  shahada yake ndipo uzalendo unaondolewa na migomo inatawala ndani ya vyuo vyetu
Majengo ya Kitivo cha Social Science ambapo wanafunzi wa kitivo hicho jana walipata mkong'oto na kumwagiwa mabomu ya machozi,baada ya kugoma,wakiwa na madai ya fedha za Field zao,baadhi yao wamejeruhiwa na kulazwa hospitali ya Mkoa,hata hivyo wanadai kupeleka malalamiko yao kwa Waziri Mkuu.

Saturday, December 18, 2010

JUMAMOSI YA LEO NAKULETEA MUENDELEZO WA MAKAO MAKUU DODOMA,NIKIANZAIA NA ROUND ABOUT TAMISEMI STAND YA DALADALA NA MAENEO MUHIMU KATIKA MANISPAA YA DODOMA

 Round about ( TAMISEMI) katika Manispaa ya Dodoma
 Stand ya daladala Jamatin ziendazo na zitokazo Mnadani ,Kuhungu,maili mbili
 Jengo la NMB Dodoma pamoja na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDO),mtaa ambao ni maarufu sana uendao katika makao makuu ya CCM Mjini hapa.
Nyerere Square ambapo watu hupenda kupigia picha kwa ajili ya kumbukumbu kama alivyo mwanachuo wa CBE Bwana Joseph Sikapundwa katika bustani hiyo hivi karibuni.

Thursday, December 16, 2010

Je unaijua Nyerere Square ,Manispaa ya Dodoma? Au Makao Makuu .

 Nyerere square ni bustani iliyopo katika Manispaa ya Dodoma,imejengwa hapo kwa ajili ya kumbukumbu ya Baba  wa  taifa Mwalimu Julius Kambalage Nyerere katika makao Makuu ya Nchi.
 Eneo hili watu hufika kupiga picha za kumbukumbu mbalimbali .
Pia kuna miti ya kivuli watu hupumzika na kujipatia vivywaji baridi,siku za kazi lakini siku za Juma mosi na Jumapili mgahawa huo haufanyi kazi,kumbe siku kama hizo ndiyo za kutangeneza fedha.Lakini usijali hayo karibu katika eneo hili la ukumbusho.

Sunday, December 12, 2010

KIPINDUPINDU CHA LIPUKA NKUUNGU NA MAJENGO MANISPAA YA DODOMA

 I meripotiwa kuwa wagonjwa 14 wa kipindupindu kulazwa katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa kipindu pindu katika Manispaa ya Dodoma katika maeneo ya Nkuungu na majengo.

Kufuatia mvua zilizonyesha katika maeneo kadhaa mkoani hapo,uchafu na maji machafu na matunda yanayouzwa na kuliwa bila kuyaosha na kunawa mikono kwa sabuni baada ya kutoka kujisaidia kumeletea mlipuko huo.

Taadhari limetolewa na uongozi wa mkoa,kuwa wananchi wanashuriwa kuepuka kula vitu vya baridi,kuondoa uchafu kwani kipindupindu kinatoletwa na kula kinyesi kinacho sambazwa na inzi,kila mmoja anashauriwa kunawa mikono kwa sabuni baada ya kutoka chooni.

Saturday, December 11, 2010

Do you know the use of ubuyu fruit this Saturday?

The mibuyu trees situated at Ruwaha Mbuyuni,at  Morogoro and Iringa Region tanzania,such trees are available at Chamwino Dodoma Tanzania ( source Christian Sikapundwa )


Ubuyu is a fruit from Mbuyu tree, mbuyu is a big tree are available in central Zone especial Dodoma,Singida, very few in Southern Zone in Lindi, Region, Morogoro and Iringa Tanzania Ruwaha Mbuyuni Area.

Ubuyu fruit is very popular this time due to the struggling of life. Most people in town they use ubuyu to produce Ice – cream ubuyu, and others produce Ubuyu juice. There for the area where ubuyu fruit is found please use those fruit to make money.

Not only Ice cream, and juice from ubuyu, but also you can mix  different colours ,and sugar with ubuyu so that you can produce good mixture which is very sweet ubuyu seed and then put them into the plastic bags and sell them to the children and Adults . (See pictures of mbuyu trees}

Thursday, December 9, 2010

UHURU MIAKA 49,TUDUMISHE UZALENDO...WATOTO 700 WA HALAIKI,200 KUTOKA VISIWAVI NA 500 TANZANIA BARA WABURUDISHA WANANCHI

 Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete akipokea heshima kutoka kwenye gwaride la vikosi vya majeshi ya Ulinzi,Polisi ,magereza na JKT katika uwanja wa Taifa siku ya maazimisho ya miaka 49 ya Uhuru jijini Dar es salaam.
 Rais Jakaya Kikwete akipungia wananchi katika uwanja wa Taifa leo siku ya kuazimisha miaka 49 ya Uhuru
Baadhi ya watoto 700 wa halaiki wakionyesha michezo ya sarakasi siku ya maazimisho ya miaka 49 ya uhuru.( MOTO: MIAKA 49 YA UHURU.TUDUMISHE UZALENDO.Jijini Dar es salaam.

Monday, December 6, 2010

kipindupindu chaua wanne,watatu wa familia moja Manispaa ya Morogoro

Ugongwa wa kipindupindu sasa cha hamia manispaa ya Morogoro baada ya kuibuka katika Wilaya ya Mvomero,imeripotiwa kuwa  wagonjwa 10 wamelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro,na  watu wanne wamefariki,kati yao watatu kutoka katika familia moja.

FURAHA YA WAZAZI NI KIJANA WAO KUPATA FAMILIA YAKE,MAMA WA MICAHEIL SIKAPUNDWA WAKIWA NA MJUKUU WAKE VERONICA

Mtoto Vero anapenda kurushwa rushwa,aona anavyo furahia kurushwa na Bibi yake Bibi Editha Sikapundwa mara baada ya kukaribishwa nyumbani kwao baada ya kutoka Dodoma, ambako alizaliwa tarehe 12/10/2010 katika Hospitali ya Mkoa huo,wakiwa kama wazazi wa Mikael na mkewe wanaungana nao katika kumshukuru Mungu katika kufanikisha maisha yao na hatimaye kupata mtoto.Walisema asante Mungu kwa yote mema yaliyopatikana.

SHUKURANI KWA MUNGU

Familia ya Bwana na Bibi Michael Sikapundwa wanamshukuru Mungu kwa ajili ya Mtoto wao mpendwa Baby Veronica Michael leo kutimiza mwezi mmoja na siku 26 tangu azaliwe tarehe 12/10/2010 katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma,ambapo sasa wapo nyumbani kwao Morogoro.

Saturday, December 4, 2010

RUVUMA YA FAULISHA KWA ASILIMIA 47.98 NA KUSHUKA KWA ASILIMIA 8.02 YA MWAKA JANA

Mshauri wa Elimu Mkoa wa Ruvuma Bibi Paulina Mkonongo akisoma taarifa ya maendeleo ya Elimu katika kikao cha Ushauri RCC katika ukumbi wa Songea Club hivi karibuni.


MKOA wa Ruvuma imefaulisha kwa asilimia 47.98,ya wanafunzi watakaoingia kidato cha kwanza mwaka huu,ikiwa imeshuka kwa asilimia 8.02 kwa matokeo ya mtihani wa taifa uliyofanyika  mwaka 2009.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mshauri wa Elimu wa Mkoa wa Ruvuma Bibi Paulina Mkonongo,mbele ya Kaimu katibu Tawala wa Mkoa huo,alisema  wanafunzi 30,829 mkiwemo wavulana 14,986 na wasichana 15,843 waliofanya mtihani huo mwaka huu,kati yao 14,792 mkiwemo wavulana 7,537 na wasichana 7,255 ndio walio faulu sawa na asilimia 47.98. Ambao wataingia kidato cha kwanza mwakani.

Aidha alisema kuwa waliochaguliwa bweni ni wanafunzi ni 103,ambapo wenye vipaji ni 31 wavulana 17 na wasichana 14,wanaokwenda ufundi ni 30 wavulana 27 na wasichana 3.Na waliochaguliwa kutwa  ni 14,689 wavulana 7,469 na wasichana 7,220.