Mkuu wa shule ya Kalembo liyoko Matogoro nje kidogo na Manispaa ya Songea Bwana Bosco Haule akielezea jinsi alivyo fanikiwa kuwapa chakula cha mchana wanafunzi wa shule yake.Ansema ili chakula kipatikane shuleni ni vyema kufanya mikutano na wazazi wakubaliane kuchanga fedha na kiasi cha kuchangisha kwa kila mzazi.
WAZAZI
wa wanafunzi wanaosoma katika shule ya sekondari Kalembo Manispaa ya Songea
Mkoani Ruvuma wanachangia sh. 30,000 kwa muhula kwa ajili ya kupatiwa chakula
cha mchana na uji wakati wa asubuhi,ingawa kiasi hicho hakitoshi.
Mkuu
wa shule ya sekondari Kalembo Bwana Bosco Haule alizungumzia umuhimu wa kutoa
chakula kwa wanafunzi wanaosoma shule za msingi na sekondari mkoani hapo na nchi nzima kwa ujumla
alipoitembelea ofisi za TUJIFUNZE leo.
Bw.Haule
alisema kuwa utaratibu wa kutoa chakula katika shule yake haukuanza hivi
karibuni,bali ulianza toka mwaka 2005,kwa kutumia Bodi ya shule
kuwahamasisha wazazi wenye watoto ambao
wanasoma katika shule hiyo kwa kuchangia sh.30,000 kwa muhula.
Alisema
mchango wa sh.30,000 kwa muhula kwa kipindi hiki akitoshi,lakini kwa kubana
matumizi wamefanikiwa kutoa uji na chakula cha mchana ,ambacho ni ugali kwa
maharage,ingawa bei ya maharge hayo iko juu ikilinganishwa na bei ya mahindi
katika mkoa wa Ruvuma.
Kuhusu
walimu Bw.Haule alisema walimu nao ili waweze kufanya kazi kwa usahii,na wao
wanapata chai na chakula cha mchana kwa kuchangia sh.10,000 kila mmoja.
Aidha
Mkuu wa Shule huyo alisema kuwa kwa wanafunzi ambao wazazi wao hawakuchangia fedha
au nafaka kwa ajili ya chakula cha watoto wao,hawapati chakula,ili wazazi wenye
watoto hao waone umuhimu wa kupata chakula kwa wanafunzi.Nakwamba kila
mwanafunzi anatumia sh.350/= kwa siku.