Sunday, November 27, 2011

WAKULIMA WA SONGEA MAHINDI YAWADODEA BAADA YA SERIKALI KUSHINDWA KUYANUNUA MAHINDI HAYO SASA WANAPELEKA SODECO KUYAUZA REJEREJA

 Wakinamama hao wanabaki hawajui nini kinachoendelea,baada ya kuambiwa serikali haina fedha za kununlia mahindi yao kwenye ghala la taifa la kuhifadhi chakula la Mkoa wa Ruvuma.
Licha ya akina mama hao kutojua nini cha kufanya ni pamoja na wakulima na wafanya biashara waliyopeleka  mahindi yao ghala la kuhifadhi chakula Songea kuamua kuyapeleka SODECO kuyauza kwa bei ya hasara.

JIONI MOJA TUKIWA UFUKWE WA MJI WA LINDI

 Tukiwa hotel ya Lindi mjini ufukweni tukichagua korosho na Bwana Juma Nyumayo Mhariri msaidizi TUJIFUNZE
 Nikiwa kwenye Bandari ya zamani ya Lindi , ambapo zamani meli za MV Lindi  na MS Mtwara zilikuwa zikitia nanga, siku hizi hazipo meli hizo.kilicho bakia mchanga umejaa meli haziwezi kusimama hapo tena kutokana na kina cha maji.kuwa kidogo.Hizo ni meli za Zanzibar ambazo mafundi wake wanazitengeneza warudi nazo kwao.Miundombinu ya barabara miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Lindi Na Mtwara  ni safi

Lami hiyo toka Masasi,Mtwara,Lindi hadi Dar es salaam .ni ndani ya miaka 50 ya Uhuru mikoa ya Kusini.


 Bwana Juma Nyumayo katika ufukwe wa Lindi Mjini akipunga upepo baada ya kazi kubwa tokea Kilwa Masoko na Kilwa Kivinje.
Jioni katika ufukwe huo watu wanakimbia,wanaogelea na wengine kuendesha baiskeli kama unavyo muona kijana huyo.
 Katika ufukwe wa Lindi baada ya kutoka Kilwa Masoko na Kivinje ,ambako wananchi wa Kilwa wanaishukuru serikali kwa kuwapatia Umeme wa uhakika  wa Gesi kutoka Songosongo.
Bw,nyumayoJioni ya mapumziko katika ufukwe wa Lindi.

Friday, November 25, 2011

MKUU WA WILAYA YA NAMTUMBO KUWA MGENI RASMI KWENYE MAANDAMANO YA KUPINGA UKATILI SONGEA LEO

 Mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Natumbo mkoani Ruvumba Bwana Saveri Maketa mwenye tai akisubiri maandamano kuyapokea katika viwanja vya makumbusho ya Taifa ya majimaji mjini Songea Leo.
 Bwana Maketa akisikiliza kwa makini mashairi yaliyosomwa na wanafunzi wa sekondari kupinga unyanya saji wa kijisnia katika jamii ya watu duniani.
 Wanafunzi wa sekondari wakiimba mashairi
wananchi wakisikiliza shaili hilo kwa makini

MKUU MKOA WA RUVUMA BWANA SAID MWAMBUNGUU AKERWA NA UNYANYASWAJI WA KIJINSIA UNAOFANYIKA DUNIANI

 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bwana Thabiti Mwambungu akiongea na wananchi leo kabla hajamkabidhi DC wa Namtumbo Bwana Saveri Maketa ugeni Rasmi..
 Wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea wakimsikiliza Mkuu wa Mkaoa.
 Baadhi ya viongozi wa Sekreterieti ya Mkoa wa Ruvuma
 Bwana Mwambungu
Wananchi katika majengo ya makumbusho ya Majimaji leo.

Maandamano ya siku 16 za kupinga ukatili duniani,ukatili wa jijinsia dhidi wanawake kanda ya Kusini na Nyanda za Juu Kusini

 Hayo ni maandamano ya kupinga ukatili duniani, maadhimisho hayo yatakuwa kwa siku 16 kuanzia leo ,ambapo leo wananchi,wanafunzi Katika Manispaa ya Songea wameandamana kuzuia ukatili wa kijinsia na dhidi ya wanawake Kanda ya Kusini na Nyanda za Juu kusini katika Manispaa ya Songea.
 Maandamano hayo yalianzia Ofisi ya CCM Mjini ,Kauru,Polisi,yakapandisha hadi Makumbusho ya Taifa ya Majimaji yaliyoko maeneo ya Mahenge Manispaa ya Songea.
 Maandamano hayo  yaliongozwa na bendi ya shule ya msingi,mabango mbalimbali ya kupinga ukatili wa kijinsia.
 Hayo ni baadhi ya maandamano yaliyoanza kuwasili katika uwanna wa Makumbusho ya taifa ya majimaji mjini Songea leo.
 maandamano katikati ya miji wa Songea leo.
Maandamano ya wanafunzi yaliyo karibia katika Makumbusho ya Majimaji leo.

Saturday, November 12, 2011

KATIKA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA MIKOA YA KUSINI IMEPIGA HATU KWA MIUNDOMBINU YA BARABARA ZA LAMI

 BARABARA YA LINDI KWENDA DAR ES SALAAM


SONGEA KWENDA NATUMBO  - TUNDURU KIPANDE CHA LAMI KILEANZA KUWEKWA



 HALMASHURI YA LINDI BARABARA ZAKE





 LINDI- MTWARA



 NANGURUKULU KWENDA LINDI
NANGURUKULU KWENDA KILWA MASOKO MKOA WA LINDI

MADAWA YA KULEVYA YAHARIBU MAISHA YA VIJANA WENGI KAMA UWAONAVYO VIJANA WA KILWA KIVINJE

mhariri msaidizi wa TUJIFUNZE  KUSINI Bwana Juma Nyumayo  aliyesimama katikati anasuluali nyeusi alikuwa akiongea na vijana wanaotumia madawa ya kulevya Kilwa Kivinje,hao wao hupaita masikani,husemekana kuwa vijana hao hawaogopi serikali wala mtu yeyote.ukiwaushi wanakuchanja na nyembe.
Bw.Nyumayo anaangalia picha ya meli iliyochorwa kwenye kitambaa na vijana hao ambao hujiita wasela,washikaji wa Kilwa Kivinje Mkoa wa Lindi ambapo Blog hii ilikuwa huko kuona maendeleo ya wananchi wa mikoa ya Mtwarana Lindi katika miaka 50 ya UHURU wa Tanzania.ambapo mafaniko yapo,na changamoto zipo nyingi zikiwepo za ukosefu wa ajira kwa vijana hao ambao ni idadi kubwa nchini,kwa kukosa cha kufanya ndipo wanatumia madawa hayo.

Friday, November 11, 2011

PAMOJA NA MAENDELEO YALIYO PATIKANA KATIKA MKOA WA MTWARA BADO WANANCHI WA MKOA HUO WANA SHIDA YA MAJI

 Akina mama na watoto wanatoka majumbani kwao saa 11 usiku kutafuata maji lakini hadi saa 10 jioni hawajapata maji hayo ambayo katika wilaya ya Masasi mkoani mtwara plastiki moja la maji ya baridi au chumvi ni sh.100.
 Na watembeza maji plastiki moja ni sh.1000 kwa maji baridi na sh.500  maji chumvi
Hiyo ni foleni ya maji ambapo akinamama wameweka ndoo zao kuanzia saa 10 lakini hadi blog hii inatia nanga Masasi saa 11 jioni bado walikuwa hawajapata maji.

SAFARI YA MIKOA YA MTWARA NA LINDI KUONA MAENDELEO YALIOFANYIKA MIAKA 50 YA UHURU KUSINI MWA TANZANIA

i
Siku ya kwanza ya kukata tiketi ya kwenda Mtwara na Lindi katika stendi ya Songea
 Bwana Juma Nyumayo Mhariri msaidizi wa TUJIFUNZE KUSINI mwenye suluali ya bluu tulikuwa nae kukata tiketi kwenye basi litokalo Songea kwenda Masasi Mkoa wa Mtwara liitwalo New Obama.
 Ndani ya Basi hilo nilikaa jirani na Mzee Mohamedi Gwasa Afisa Elimu mtaafu ,alimpokea Bwana Nyumayo walipokuwa akiripoti akiwa mwalimu katika wilaya ya Tunduru mika ya nyuma.
 Mwl Mohamedi alistaafu kazi miaka ya themanini,huyo mwenye balaghashia alikuwa akienda masasi
Mwl.Mohamedi walipiga picha ya pamoja na kijana wake Bw. Nyumayo ya ukumbusho baada ya kuwasili Mtwara.

Wednesday, November 2, 2011

ELIMU YA WATU WAZIMA KATIKA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA

 Mzee Evans  Leonard Kalonga Afisa eilimu ya Watu Wazima Mkoa mstaafu aliyetumikia taifa hili katika wadhifa huo hadi kustaafu anasema elimu ya watu wazima ilichangia kwa kiasi kikubwa kufuta ujinga kwa jamii ya watanzania baada ya uhuru.Mzee kalonga aliwahi kuwa Afisa elimu ya watu wazima Mkoa wa Rukwa na baadaye Mkoa wa Ruvuma hadi kustaafu kwake.

 Bwana Thomas Lipuka Komba yeye amestaafu akiwa Afisa Elimu Vielelezo Wilaya za Lindi na baadaye Songea vjijini yeye alikuwa Afisa Habari katika Idara ya elimu akiwa Ripota wa magazeti ya TUJIFUZNE KUSINI hadi anastaafu.
 Maafisa hao ni hazina tosha ya elimu ya watu wazima ilivyo anza kushamili hadi kupoteza umaarufu wake.
Hapa wakiaandaa MAKALA ya elimu hiyo kwa ajili ya Toleo Maalumu la TUJIFUNZE KUSINI ndani ya miaka 50 ya uhuru wa nchi hii.

NGOMA ZETU LEO NAWALETEA NGOMA YA KUSINI LIZOMBE AMA KWA JINA LINGINE KITOTO


 kikundi cha Lizombe cha Jakaya Mrisho Kikwete cha Lizaboni Manispaa ya Songea kilicho tumbuiza siku ya wiki la elimu ya watu wazima kiwilaya limefanyika Kata ya Majengo

 Bwana Rabii Mzee mwanakisomo wa Majengo akisoma risala siku ya juma la elimu ya watu wa zima Manispaa ya Songea hivi karibuni
 Waandishi wa habari akisikiliza kwa makini ujumbe unaosomwa na Bwana Rabii Mzee kutoka kwenye risala hiyo.
Baadhi ya walimu waliofika kuhudhuria wiki hilo wakiwa kama watazamaji wasiojua nini kinaendelea kuhusu elimu ya watu wazima.