Sunday, May 17, 2015

TUNATAKIWA KUMTANGULIZA MUNGU KATIKA KILAKITU,ILI KUWEPO NA MAFANIKIO ,KUMEKUWEPO NA MATUKIO MENGI MAZURI YANAYOTOKEA BUNGENI NI KWA AJILI YA MAOMBI YA WATU

Kauli hiyo imetolewa leo na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Anne Makinda,wakati akiwasalimu waumini wa Roman Catholic katika Kanisa kuu la Mjini Dodoma,kabla ya hitimisho la Ibada ya  misa ya kwanza leo.
Mhe. Makinda alisema kuwa waumini wa dhehebu hilo wasali na kuomba Mungu sana ili mafanikio ya mahitaji yao yapatikane kwa urahisi.
Alisema maombi ya waumini mbalimbali wa madhehebu ya dini,wamejitahidi sana katika maombi yao yaliyofanya mikutano inaendeshwa ndani Bunge hilo yawe ya amani na utulivu hasa kwa miaka mitano iliyopita.
Hivyo ili kanisa liweze kujiendesha ni budi waumini watoe michango yao,katika kuboresha miundombinu mbalimbali katika makanisa hayo.

3 comments:

  1. Hayo ni kweli kabisa. Nikigusia hilo suala la kutoa michango, napenda kusema kuwa nimefikia hatua ya kuamini, miaka hii ya karibuni, kwamba kadiri ninavyotoa ndivyo Mungu anavyonijalia.

    Siku nyingine ninajikuta nina hela kidogo mno, na ndiyo ya mwisho. Zamani nilikuwa ninajikuna kichwa na kupiga mahesabu na kutoa visingizio elfu, ili tu nisalimishe vijihela vyangu. Lakini, nimekuwa ninakumbana na miujiza, baada ya kutoa vile vihela kanisani. Unaweza kufika nyumbani ukakutana na mtu anakuambia amekuja kukulipa deni alilokopa miaka nenda rudi iliyopita nawe ulishasahau.

    Hata watu wakisema nimechanganyikiwa, mimi sijali. Ninajione mwenyewe miujiza hii.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sio utani unayoyazungumza ni ya kweli kabisa hayo hata mie yamenikuta hivi kavibuni.
      Mwezi uliyopita nipatwa na matatizo kibao, Nilienda kumzika baba mkwe Mbeya ,Narudi Dodoma Gari ikapasuka gurudumu la mbele kwa dereva bahati hatukupinduka dereva ambaye ni kijana wangu wa mwisho alikuwa makini na Mungu alizuia ajali ile, kama hiyo haitoshi nafika nyumbani nikaibiwa vifaa vyangu vya mawasiliano vyote , kuanzia Laptop,Camera,Modem,simu mbili nikawa lofa tu. Na ndiyo maana sikuonekana mtandaoni kwa muda.Imetokea nimenunua baadhi ,nini Mungu hutoa jibu kwa waja wake.

      Delete
  2. Mzee Sikapundwa,

    Mzee Sikapundwa, pole sana kwa matatizo. Ningemwona mtu anayekuja huko Tanzania ningetafuta kamera akuletee, uweze kuendelea na kazi ya kutuneemesha katika hii blogu. Nilijiwa na wazo la kukuletea kamera tangu kabla hujastaafu. Mungu yuko, nitatekeleza, ili niendelee kufaidi taarifa zako, na wengine wafaidi pia. Kinachonifanya niwazie hayo, pamoja na kuienzi kazi yako ya kuendesha blogu, ni hofu yangu kuwa huko nyumbani mnaweza mkauziwa bidhaa feki.

    ReplyDelete