Tuesday, May 19, 2015

RAIS PHILIP NYUSI WA MSUMBIJI AMEKUWA RAIS WA KWANZA WA NCHI HIYO KULIHUTUBIA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

 Rais Philip Nyusi akilihutubia bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mjini Dodoma leo,amesema ziara yake hapa nchini ina lengo la kukuza ushirikiano baina ya Tanzania na Msumbiji kuhusu Demokrasi,siasa na utamaduni, ushirikiano katika biashara na elimu.
Aidha ziara hiyo ni mafunzo kwake ya uongozi na kudumisha ushirikiano wa waasisi wa vyama vya nchi hizo mbili.Pia amesema wafanya biashara wanakaribishwa Msumbiji ,na Viza hakuna.
Baada ya Ziara yake bungeni amerejea nyumbani kwake nchini Msumbiji.
Baada ya Hotuba fupi alipewa zawadi ya picha ya Jengo la Bunge na Mhe. Spika Anne Makinda.

No comments:

Post a Comment