Monday, May 25, 2015

BAJETI YA WIZARA YA MAENDELEO JINSIA NA WATOTO YALETA ZOGO NDANI YA BUNGE,BAADA YA MHE.ESTER MATIKO KUTAKA KUJUA KWA NINI INGO KUFUTWA.

Akilalamikia WAMA ni ya Chama Tawala.
Waziri wa Wizra hiyo Mhe,Sophia Simba alijitahidi kuelezea kuhusu INGO na WAMA,Lakini ikawa nidhamu hakuna, sauti zinasikika kutoka kwa baadhi ya wabunge, Kaachini au simama,sasa hawaheshimu kiti cha mwenyekiti.Hebu wafika mahali wajue kuwa Bunge lile si mahala pa malumbano ya utofauti wa Vyama.Wasubili kwenye Kampeni,Ni aibu watu wengine wanavyo liona Bunge letu.

Friday, May 22, 2015

VIFAA VYA CERAGEM ,PAMOJA NA KUPONYA MAGONJWA NA UBORESHA AFYA,LAKINI PIA HUPUNGUZA MAFUTA YALIYO JAZANA MWILINI,KAMA NILIVYO VAA SLIM BELT KUPUNGUZA TUMBO

 Mkanda huu hupunguza mafuta yaliyo jazana tumboni na ufanya tumbo lipungue.CERAGEM hii ina toa huduma ya upima uzito, urefu na uwingi wa mafuta mwilini.Huyo ni mie  Blogger TUJIFUNZE KUSINI CHRISTIAN SIKAPUNDWA, Hunikosi kwenye Mazoezi Tiba ya CERAGEM kila siku,Wewe Je, Unangoja Nini.
Waati wengine wako kwenye mazoezi ,na baadhi yao hulala wenye mashine hizo kwa dakika 40,kama hiyo haitoshi, walimu wa kituo hicho wanatoa mafunzo kila siku kuhusu mwili wa binadamu ulivyo na jinsi unavyo fanya kazi, Aliye kaa ni mwalimi Bi. Lilian Mushi ili kuwasaidia wanao lala katika mashine hizo
Hilo ni jengo la Kituo cha CERAGEM Uhindini Mjini Dodoma

VIJANA TUACHE KUKAA VIJIWENI,TUJISHUGHULISHE NA BIASHARA NDOGO NDOGO KUFANYA HIVYO TUTAPATIWA MIKOPO YA KUENDESHA BIASHARA

Hayo yamesemwa na majasilia mali Bwana Mmas Iramba anayeuza viatu vya mitumba ndani ya soko la Sabasaba  katika manispaa ya Dodoma.
  Mmasi alisema kuwa vijana waachane na magenge vijiweni, bila ya kujishughulisha kwani kuna fursa nyingi zinazoweza kumtoa kijana pale alipo na kusonga mbele kwa kufanya biashara.
Amesema alianza na viatu vichache lakini baada ya kupata mkopo ameweza kununua viatu vya mitumba vingi vinavyo mpatia faida na kulipa deni alilokopa.

Thursday, May 21, 2015

USAFIRI WA MAJINI ,UWEKEWE VIFAA VYA TAHADHARI,LEO NI SIKU YA KUMBUKUMBU YA KUTIMIZA MIAKA 19 YA MELI MV BUKOBA

Hapa ni eneo la Igoma Mwanza walipozikwa wahanga 391 waliokosa ndigu zao kutokana na ajali ya kupindika na kuzama kwa meli ya MV Bukoba Mei 1996.
Basi keo waombolezaji na wananchi wlioguswa na tukio hilo waliweka maua na kufanyia usafi katika makaburi hayo.Lakini pamoja na ajali hiyo bado usafiri katika Ziwa Victoria hali ni tete,sio salama sana.Zaidi ya watu mia nane walipoteza maisha.yao ,Mungu zilaze  roho za marehemu hao mahali pema peponi Amein.

DODOMA, WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BAJETI YAKE ZAIDI YA BILIONI 200 IMEPITA BILA KUPINGWA

Waziri wa KATIBA  na SHERIA Mheshimiwa Rose Migiro amewahimiza wananchi kusoma katiba,ili waielewe wakati wa kuipigia kura katiba hiyo.
Amesema kuwa katiba 2,400,000 zimichapishwa na kusambazwa, nakala 2,000,000 ni za  maandishi ya kawaida ,Nakala 200 na  maandishi ya nundu kwa ajili ya wale wasioona  na nyingine 200 ni kwa maansidhi makubwa kwa ajili ya wenye uono hafifu ,naka 1,443,000 zimepelkwa kwenye kata zote nchini.
Aidha mahakama imepata bajeti kubwa ikilinganishwa na bajeti ya miaka iliyopita,ambapo imetengewa 40 Bilion.

Wednesday, May 20, 2015

HIVI VIONGOZI KUSHINDWA KUHAMIA MAKAO MAKUU YA NCHI DODOMA NA KUWAFANYA WABAKI DAR ES SALAAM ,NI KWA SABABU

Dodoma hakuna bahari  au Uwanja wa ndege wa Kimataifa.Au kwa sababu Dodoma kuna vumbi jingi ikilinganishwa na Dar es Salaam ,Au Mchana jua usiku Baridi kali. Au vipi  kwa hiyo Dodoma ya leo siyo ile ya miaka miwili iliyo pita. Nahii ndiyo Dodoma yenye wenyeji wakarimu sana.

 Ni moja ya majengo mapya ambalo litakuwa ofisi mbalimbali lililop mkabala na Maktaba ya Mkoa wa Dodoma, na ofisi za Fire
 Nihayo  majengo mawili amabyo yapo katika hatua za mwisho wa kukamilisha ujenzi
 Katikati ya miti hiyo ni Maktaba ya Mkoa wa Dodoma mkabala na Hospitali ya Makole na Ofisi za Manispaa ya Dodoma
Kulia kwenye mtu aliyekaa na anyetembea ni SIDO HAPA Dodoma barabara kuelekea Tenesco Dodoma

Tuesday, May 19, 2015

RAIS PHILIP NYUSI WA MSUMBIJI AMEKUWA RAIS WA KWANZA WA NCHI HIYO KULIHUTUBIA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

 Rais Philip Nyusi akilihutubia bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mjini Dodoma leo,amesema ziara yake hapa nchini ina lengo la kukuza ushirikiano baina ya Tanzania na Msumbiji kuhusu Demokrasi,siasa na utamaduni, ushirikiano katika biashara na elimu.
Aidha ziara hiyo ni mafunzo kwake ya uongozi na kudumisha ushirikiano wa waasisi wa vyama vya nchi hizo mbili.Pia amesema wafanya biashara wanakaribishwa Msumbiji ,na Viza hakuna.
Baada ya Ziara yake bungeni amerejea nyumbani kwake nchini Msumbiji.
Baada ya Hotuba fupi alipewa zawadi ya picha ya Jengo la Bunge na Mhe. Spika Anne Makinda.

TANZIA BLOG YA TUJIFUNZE KUSINI INATOA POLE KWA SHIRIKA LA UTANGAZAJI TANZANIA TBC KWA KUMPOTEZA MPENDWA WAO,MFANYAKAZI MWENZAO WA KITUO CHA KANDA YA KATI DODOMA BWANA SAMWELI CHAMLOMO

Aidha familia ya marehemu tunaitakia moyo wa uvumilivu kwa kipindi hiki kigumu walicho kuwa nacho.Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Amain

MHESHIMIWA FESTUS LIMBU MBUGE NA MKURUGENZI WA CERAGEM UHINDINI NA IRINGA ROAD DODOMA,ATOA WITO KWA WANANCHI KULINDA AFYA ZAO KWA KUFANYA MAZOEZI NA KUACHA KUTUMIA VYAKULA VYENYE MAFUTA MENGI

 Mheshimiwa Festus Limbu  Mbunge na Mkurugenzi wa CERAGEM Dodoma  Mtaa wa Uhindini na Iringa Road
 Mhe. Limbu amevaa Slimbelt kupunguza mafuta kwenye tumbo
 WanaCeragem wakifanya mazoezi kabla ya kupanda kwenye Mashine
Baada ya mazoezi wanapata elimu ya CERAGEM  kutoka kwa walimu wa kituo hicho
Hiyo ni baadhi ya bidhaa za CERAGEM zinazopatikana katika kituo hicho.


Mhe. Limbu amechukua uamuzi wa kuanzisha CERAGEM kwa lengo la kuwajengea watu afya zao , kwa kutoa huduma hiyo bure kwa kila mmoja.Ila VIP kuna malipo kidogo kwa ajili ya uendeshaji wa kituo.
 Aidha alisema watu wajenge tabia ya kufanya mazoezi, kuacha au kupunguza vyakula vyenye mafuta mengi ili kufanya miili yao kuwa imara na yenye afya
Hivyo kupitia  matumizi ya Ceragem na bidhaa zake zitawasaidia watu wenye magonjwa na wasio wagonjwa
kwa hudhuria kila siku au kununua mashine kuwa nayo nyumbani.

CERAGEM NI MOJA WAPO YA TIBA MBADALA { NI MAZOEZI TIBA } DODOMA WANAPATIKANA UHINDINI NA IRINGA ROAD}



Sumay Renatus  Meneja na Lilian Mushi Mwalimu akifaniwa Finger press
 Baada ya mazoezi wanapanda kwenye mashine Tiba kwa dakika 40
Wanafanya mazoezi ya kuondoa ganzi mgongoni hadi kiunoni



Mazoezi ya viungo vya mwili hufanyika kabla ya kupanda kwenye mashine

Mashine ya aina ya V3


Nini maana ya CERAGEM, CERAGE ni Kampuni ya Kisayansi  na ya kibiashara ya Kimataifa,inayo husika usambazaji wa vifaa vya  mazoezi tiba.

Hayo yamesemwa na Bi.Sumay  Renatus Meneja na Bi .Lilian Mushi Mwalimu wa Kituo cha Uhindini Dodoma Manispaa. Na kwamba CERAGEM Ilianzishwa wmaka 1998,baada ya kufanyiwa utafiti wa miaka 6 { sita } nakundua kuwa madini ya JADE ambayo hutoa Farinfared Radiation yakisambaa mwilini mwa mgonjwa kupitia Uti wa mgongo,mgonjwa huyo atapata tiba kutokana na ugojwa uliyokuwa ukimsumbua.

Mashine za CERAGEM huweza kuleta matokeo haraka  kukiwepo na umeme ambao hufanya mashine hizo kufanya kazi  “ Automatocally na pia hutoa Moxibution Thermoterapy”..Na hivyo ni kama njia moja wapo ya tiba mbadala.

Aidha hutumiwa na wagonjwa kwa kupata tiba kupitia mshine za Ceragem ,pia na kwa wazima ili kuweka miili yao kuwa imara na yenye afya,kwa mazoezi na kutumia mashine za CERAGEM.pia na kujikinga na maradhi.

Maneja na Mwalimu wa CERAGEM kITUO cha Uhindini Manispaa ya Dodoma Bi.Sumay Renatus ,Anaeleza kuwa,

CERAGEM ni Huduma ya vikanda Joto, Zoezi Tiba, ambayo kwa ujumla wake huitwa vikanda Joto kwa sababu hufanya kazi yake kwa kifaa kilichotengenezwa maalum kwa ajili ya kutumiwa kwa njia ya Uti wa mgongo, kilichotengenezwa kwa dini ya JADE.

Kituo hiki hutoa huduma bure ,pia na malipo kidogo kwa ajili ya kujiendesha katika upatikanaji wa umeme.Hivyo Bi Renetus afafanua kuwa kuna malipo Tshs. 40,000 kwa wiki ambapo akiongeza malipo ya kufikia Tshs. 290,000 atapata zawadi ya MINIPAD ambayo ataitumia nyumbani kwake.
Na Tshs.170,000 kwa mwezi  naye huyo iwapo ataongeza malipo kufikia Tshs.290,000 kabla ya mwezi kumalizika ,atapata zawadi ya MINIPAD
Amezitaja bidhaa za CERAGEM kuwa ni pamoja na
 Mashine ya Master V3  inapatika kwa bei ya Tsshs.6,200,000.
RLI   Tshs.4,600,000.
P390   Tshs.1,900,000.
MixPad    Tshs.520,000.
MiniPad    Tshs.290,000.
Healax,    Tshs. 590,000.
Slimbelt    Tshs. 760,000.

Makao makuu ya CERAGEM yapo Dar es Salaam Mtaa wa Lindi na Livingstone.
Pia wapo Tegeta,Mwenge,na Kigogo.
Dodoma wapo  Uhindini na Iringa Road
Mwanza,Mbeya na Arusha.

Wenye matatizo ya kiafya na wenye afya zao wanakaribishwa kwenye CERAGEM kwa huduma ya bure na kununua bidhaa za CERAGEM.

Monday, May 18, 2015

HALI YA HEWA LEO MAKAO MAKUU YA NCHI, DODOMA IMETULIA HAKUNA UPEPO,VUMBI WALA JUA KALI, JUA LINAWAKA KWA MBALI ,NA KIKUBWA ZAIDI MASHINE ZA KUANDIKISHIA DAFTARI LA WAPIGA KURA ZIMEGWANYWA KWA WATAKAO FANYA ZOEZI LA UANDIKISHAJI KATIKA MANISPAA YA DODOMA UTAKAO ANZA HIVI KARIBUNI

 Eneo la ofisi za Ujenzi na Stendi ya mabasi yaendayo Dar es Salaam katika Manispaa ya Dodoma,Barabara iendayo Bungeni ,Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,ambapo vikao ya Bajeti vinaendelea.
 Hiyo ni baadhi ya mitaa katika Manispaa hiyo.

Sunday, May 17, 2015

TUNATAKIWA KUMTANGULIZA MUNGU KATIKA KILAKITU,ILI KUWEPO NA MAFANIKIO ,KUMEKUWEPO NA MATUKIO MENGI MAZURI YANAYOTOKEA BUNGENI NI KWA AJILI YA MAOMBI YA WATU

Kauli hiyo imetolewa leo na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Anne Makinda,wakati akiwasalimu waumini wa Roman Catholic katika Kanisa kuu la Mjini Dodoma,kabla ya hitimisho la Ibada ya  misa ya kwanza leo.
Mhe. Makinda alisema kuwa waumini wa dhehebu hilo wasali na kuomba Mungu sana ili mafanikio ya mahitaji yao yapatikane kwa urahisi.
Alisema maombi ya waumini mbalimbali wa madhehebu ya dini,wamejitahidi sana katika maombi yao yaliyofanya mikutano inaendeshwa ndani Bunge hilo yawe ya amani na utulivu hasa kwa miaka mitano iliyopita.
Hivyo ili kanisa liweze kujiendesha ni budi waumini watoe michango yao,katika kuboresha miundombinu mbalimbali katika makanisa hayo.