Saturday, May 18, 2013

MIUNDOMBINU YA RELI YA KATI IKIIMARISHWA PAMOJA NA KUIMARISHA NYUMBA ZA WAFANYA KAZI WA RELI HIYO IKIWA NA KUONGEZA WAFANYA NAZI NA MISHAHARA YA KUTOSHA HALI YA USAFIRISHAJI WA MIZIGO NA ABIRIA UTAKUWA KAMA AWALI

 Railway Station Kimamba kwa sasa pamefungwa kwa muda kushoto kwako ni jengo ambalo wasafiri wanakatia tiketi na ni ofisi ya Station Master.Unaingalia kuelekea Dar es Salaam
 Hiki ni kituo kidogo cha Train cha Kimamba Kilosa ( Station ) hiyo ni Reli mbayo bado ipo imara ingawa kituo hicho hakifanyiwi usafi kwa kuwa kimefungwa kwa muda.unaitazama ikielekea Dodoma.
 Hiyo nyumba ni ya Station Master
Hilo jengo la Station ya Mkata,Kwa mujibu wa Mfanya kazi katika Shirika la Reli katika Station ya Kilosa ambaye hakupenda jina lake lijulikane, aliiambia Blog hii leo kuwa.Vituo vyote vya Train havijafungwa na hali ya Njia ya Reli ni nzuri ila inatakiwa kubadilishwa.
Alisema kuanzia eneo la Kilosa hadi Mwenyimsagali reli yake bado ni ya Pound 65 ambayo Train kipita juu inachezacheza kwa kuwa ni nyembamba na kusababisha kuacha reli na kuanguka,ni tofauti na maeneo ambayo wametandika reli ya Pound 80.
Amesema hata hiyo ya Pound 80 imeshapitwa na wakati,pamoja na kwamba Reli ya Tazara ina uzito wa Pound 80.
Aidha amesema ili kufanikisha Reli hiyo Serikali ikarabati miundombinu yake,magenge ambayo kuna wafanya kazi wanaishi  huko na yenyewe yakarabatiwe,na wafanya kazi waongezwe mishahara kwani iliyopo ni midogo kulinga na kazi wanazozifanya za kunyanyua mataruma
Alisema kwenye Yard ambapo ni Railway Station panatakiwa kuwepo na wafanya kazi 9 na fundi mmoja kwa ajili ya kushusha na kutandika reli.

Thursday, May 16, 2013

ASKOFU MKUU WA JIMBO KUU LA SONGEA MHASHAMU NOBERT MTEGA, AKUBALIWA OMBI LAKE LA KUSTAAFU KUTOKANA AFYA YAKE KUTOKA KWA BABA MTAKATIFU FRANCIS , VATCAN CITY ROMA, NAWALA HAJAJIUZURU KAMA ILIVYO TANGAZWA NA BAADHI YA VYOMBO VYA HABARI

 Askofu Mstaafu Norbet Mtega akihojiwa na Vyombo vya habari kuhusu uamuzi wa Kustaafu kazi za utume wake kabla ya miaka 75 ambayo Askofu anatakiwa kuomba kustaafu.
 Mahojiano na waandishi wa habari
 Picha ya pamoja na waandishi wa habari katika Bustani ya nyumba ya Uaskofuni Mjini Songea leo.
 Picha ya pamoja
 Picha ya pamoja na  Mhashamu Askofu Mtega
 Askofu Mtega akiwa na mtangazaji wa Radio Maria Mbinga Bw. Nilai  wa kushoto na Mwandishi wa habari mpiga picha Bw. Ndolanga na Nyuma yake Askofu ni Bibi Joyce Joliga mwandishi wa habari Gazeti la Mwananchi
Ni picha ya Pamoja ya Mwandishi wa habari wa TBC Bw.Gerson Msigwa na Askofu Mtega



Kauli hiyo ameitoa leo mbele ya vyombo vya habari alipokuwa akiongea navyo katika bustani ya nyumba ya uaskofuni katika kanisa kuu la Mtakatifu Mathias Mulumba Kalemba la Mjini Songea.
Askofu Mtega alisema ni vyema kuacha mapema kazi wakati mtu akiwa na nguvu,akili kuliko kusubili mpaka akili ichoke kwa kusahau mambo.
Alisema ameomba kustaafu kabla ya miaka ya kustaafu kwa maaskofu wa miaka 75.kutokana na matatizo ya kiafya ,mara nyingine anasumbuliwa  na BP.
Askofu Mtega amefanya utume wake kwa miaka 28 ambapo Mkoani Iringa ametumikia kwa miaka 6 na Jimbo Kuu la Songea ametumikia miaka 22, na kutoa huduma za kiroho na za kijamii zikiwemo za Elimu ,Afya pamoja na Mazingira.
Amesema kuwa yeye bado ni Askofu na atafanya kazi zote atakazo ambiwa kufanya na Askofu Mkuu atakayeteuliwa, ambapo kwa sasa anashikilia Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania, Mhashamu Ngalalimnamtwa wa Iringa.
Amewashukuru waumini wote kwa ushirikiano mwema waliouonyesha wakati wa utume wake,na  amekuwa nao kwa moyo mmoja bila kukwaruzana wala kugombana, aidha ameomba ushirikiani uimarike na kufanya kazi bila kuingiza ukabila maana masuala ya ukabila yilipitwa na wakati.

Saturday, May 11, 2013

WANACHUO SITA ( 6 ) WAHITIMU KOZI YA MIEZI 9 YA USHIRIKA NA SACCOS KATIKA CHUO CHA USHIRIKA SONGEA TAWI LA CHUO KIKUU CHA USHIRIKA MOSHI MJINI SONGEA

 Mgeni Rasmi na Afisa Ushirika wa Mkoa wa Ruvuma na Kaimu RAS Bw.Watson Nganiwa mwenye kaunda suti nyeusi akimpa cheti Mmoja wa wahitimu wa ' Professional Fanancial Cooperative Programme ( PFCMP} ya miezi 9 katika Chuo Cha Ushirika Songea Tawi La Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi Tanzania chenye matawi yake nchi nzima.
 Huyo ni Mhtimu wa Pili aliyepewa cheti ambapo waliopata vyeti ni sita wanaume watatu na wanawake watatu Mwenye suti na tai ndiye Mratibu wa Kituo cha Chuo cha Ushirika Songea Bw.Abel Raphael Ngowi
Mwenye suti nyeukundu naye ametunukiwa cheti,akiwa ni mfanyakazi katika chuo hicho Dada Lucida Chowo.
 Akina mama hawako mbele katika elimu ya Ushirika Huyo ni Bi.Tabasamu Adima Mbawala akionyesha cheti chake baada ya kukabidhiwa
 Bi fausta Kasuga mwenye nguo nyekundu ambaye ndiye Mratibu wa Mafunzo na mwalimu katika Chuo hicho na Afisa Ushirika wa Manispaa ya Songea akimpa mkono wa pongezi mwenyekiti za mafunzo hayo pia ni mhitimu Bw.Wanter Ndimbo baada ya kupewa cheti
Mwenyekiti Bw.Ndimbo akisoma risala mbele ya mgeni rasmi hayumo katika picha. Matukio mengine yataendelea kutolewa zaidi ili kukielewa vizuri chuo hiki.



WANACHUO sita wa ( course ya  Financial cooperative Programme ( PFCMP ) wakiwemo wanaume watatu na wanawake watatu wametunukiwa vyeti baada ya kusoma kwa miezi tisa katika Chuo Cha Ushirika Songea.katika Kozi ya Professional Financial Cooperative Management Programme (PFCMP)

Afisa Ushirika wa Mkoa wa Ruvuma ,pia na kaimu RAS wa mkoa wa Ruvuma Bw.Watson Nganiwa amewakabishi vyeti Bw. Kevin Ponera wa SACCOS Mshangano,Wanter Ndimbo SACCOS Walimu Vijijini, Pia mwenye kiti wa Mafunzo, Bi.Tamasamu Adimu Mbawala, Bw.Theophord Seif,Bi Lucida Chowo.

Aidha Bw. Nganiwa amesema elimu ndiyo  kila kitu katika maisha ya mwanadamu,na kwamba elimu haijali umri wa mtu.Na amweaasa wahitimu hao kuwa wawe  mabalozi wazuri huko wanakokwenda kwa kukitangaza chuo cha ushirika Songea Tawi la Chuo kikuu cha Ushirika Moshi kuwa kinatoa mafunzo kupitia elimu masafa.

Alisema wale wenye matatizo ya ada wafike kweke atazame namna ya kuwasidia ili watimize ndoto zao za kupaya elimu ya usimamizi wa Ushirika na SACCOS.katika SACCOS zao.

Awali Mratibu wa Chuo Kikuu hicho Bw. Abel Raphael Ngowi,amewapongeza wahitimu hao kwa kuweza kuhudhuria masomo kwa miezi 9 bila kutoa  kwa sababu zakushindwa kuhudhuria masomo, alisema masomo ya utu uzima siyo mchezo inatakiwa kujituma,na hivyo amewapongeza kwa kuhitimu kwao.ili wawe chachu kwa wengine wenye nia ya kusoma kupitia Elimu Masafa.

Alisema kwa kupata cheti peke yake bila kuonesha mabadiliko huko wanakokwenda itakuwa ni kazi bure, hata sifa za chuo hicho zitakuwa hazipo, alicho taka kwa wahitimu hao ni kuonyesha badaliko tofauti kabla hawajapata elimu ya Ushirika.na baada ya kupata taaluma hiyo katika SACCOS zao.

Bw.Ngowi alisema chuo hicho kinaendesha kozi za masafa ,ambapo kuna walimu wawili wanafundisha katika chuo hicho, aliwataja walimu hao kuwa ni pamoja na Bi.Fausta M. Kasuga,Mratibu wa Mafunzo pia ni Afisa Ushirika wa Manispaa ya Songea na Bw. Fredrick P. Kandosa

Ambapo Mratibu Msaidizi Bibi Benigna Nchimbi( Mrs Haule ), amewasihi wahitimu hao kuwa wakatumie vyema elimu waliyoipata, kisha kwa wale ambao watajiunga na masomo hayo, SACCOS zao zitoe ada ya kusomesha wasimamizi wa SACCOS hizo.

Friday, May 10, 2013

WANANCHI WA KATA YA MAJENGO MANISPAA YA SONGEA WAILALAMIKIA MANSIPAA HIYO KUACHA KUSOMBA TAKATAKA HIZO KWA MUDA MREFU

 Hizo ni takataka zilizo zagaa kutoka mbele kwenyeGuma lililojegwa kwa ajili ya kukusanyia takataka.
Mbele ni duka la madawa nyuma na takataka kama zinavuonekana,hapohapo kunajiwe na Bendera ya Chama Tawala,

Watoto nao hawpo nyuma katika kuokota vitu vilivyo tupwa katika maguba hayo,Lakini pamoja na ukosefu wa vitendea kazi Basi angalau hata kwa kukodi malori yaende Kata ya Majego kuzoa taka hizo
Hiyo ni barabara ya Malori ambapo takataka zimo kando kando kwa barabara hiyo.
Barabara hiyi hujulikana kwa barabara ya nitmba,kama unavoona guba la takataka lipo jirani na wauza mitumba .
Hiyo ni bara bara ya majengo maarufu kwa barabara ya mitumba Naeng,ya Majengo



WANANCHI wa Kata ya Majengo Manispaa ya Songea wanailalamikia Halmashauri hiyo kuacha kupeleka gari la kuzoa taka hizo.Na kwamba wanadai kwa kuwa Diwani wao ni wa Chama cha Upinzani ndiyo maana Halmashsuri haipeleki gari huko
.
Kwa mujibu wa baadhi ya wananchi wa Kata hiyo ,walisema kuna maguba mengi tu ambayo hayajazolewa taka kwa muda mrefu na kusababisha harufu mbaya katika maeneo hayo ambayo yamezungukwa na makazi ya watu.

 Walisema inashangaza kuwaona viongozi wanapita na magari yao na kuziona taka hizo bila ya kuchukua hatua yoyote,kiafya haipendezi kuona watoto wanaokota vitu kwenye maguba hayo.Istoshe mbele ya guba moja kuna duka la madawa lililoandikwa HATI PUNGUZO.

Wananchi hao wasiwasi wao ni kutokea kwa magonjwa ya mlipuko kutokana na uchafu uliyo kithili,wanadai kuwa wanaona taka zilizo katikati ya mji na sokoni ndiyo zinazo zolewa.na kwao zinaendelea kusambaa.

Ambapo alipo ulizwa Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Bwana Nachoa Zakaria alikiri kusema kuwa tatizo hilo linaeleweka na wala halina mahusiano na tofauti za vyama katika Manispaa yake.Bali manispaa haina magari ya kutosha.

Alisema tatizo lililopo ni la ukosefu wa vitendea kazi ambapo kwa sasa Manispaa ina malori mawili tu ambayo ni mabovu ni ya miaka 20 tangu yanunuliwe,kila siku ni gereji,na kwamba ili kusomba taka zote kunahitajika magari sita mapya ya tani 20 na kijiko.kwa ajili ya kuzolea taka,wakati sasa wanatumika vibarua kuzoe taka hizo kwa machepe.

Wednesday, May 8, 2013

BREAKING NEWS , KUUA MAASKOFU,MAPADRE AU MUFTI NA MASHEKHE NDIYO KUUMALIZA UKRISTO AU UISLAMU,NI KUJIDANGANYA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mizengo Pinda,alisema watu wasijidanganye hata kidogo,kwa kuzani kuwa wakiwaua viongozi wa dini ndiyo mwisho wa Ukristo au Uislamu.Hapana watu wataendelea na Imani zao.
Alisema kuwaua Maaskofu,Mapadre au Mufti na Mashekhe ndiyo mwisho wa Ukristo au Uislamu ni kujidaganya.kwani pale unaua Askofu ,Padre, Mufti au Shekhe basi siyo kuua Ukristo au Uislamu.

Kauli  hiyoaliitoa alipokuwa akizungumza  na wananchi wa Mkoa wa Arushu alipo kwenda kutoa pole kwa wahanga wa Bomu lililolipuliwa ndani ya Kanisa katoliki la Mt.Joseph Mfanyakazi.Na kuwataka wanachi watulie nakuwaombea majeruhi wapate nafuu mapema ili waungane na Jamaa zao.

Wakati huo huo Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Muadhama Policarp Pengo alisema Tukio lililotokea Arusha lisihusishwe na Uislamu kwa kuwa ndani ya wahalifu wanaodhaniwa kufanya uhalifu huo wamo pia na wakristo

Monday, May 6, 2013

BREAKING NEWSSS POLISI MKOANI ARUSHA YA WASHILIA WA 8 WALIOSADIKIWA KULIPUA BUMO NDANI YA KANISA

POLISI Mkoani Arusha inawashikilia watu nane ( 8 ) wanalihusika natukio la kigaidi la kulipua bomu ndani ya kanisa siku ya Jumapili.
Katika tukio hilo watu wawili wamepoteza maisha yao ambapo wa 50 wapata majeraha katika sehemu zao mbalimbali za mwili.
Kutokana na hisia za watu zisizokuwa na tafiti za kisayansi,kuwa tukio hilo halina uhusiano na imani za kidini,bali nina uhusiano na ugaidi.

Sunday, May 5, 2013

BEAKING NEWSS ,ARUSHA,MWAKILISHI WA PAPA FRANCI NCHINI TANZANIA ANUSURIKA KULIPULIWA NA BOMU MITA 10 TOKA LILIPOLIPUKA BOMU HILO LEO

Mwakilishi wa Papa Franci Nhini Tanzania amenusurika kulipuliwa na bomu lililolipuka umbali wa mita 10kutoka pale alipo, ndani ya Kanisa Katoliki la Olasite Jijini Arusha leo wakati akiendesha Ibada ya uzinduzi wa kanisa hilo.

Kwa mujibu wa Sechelela Kongola  TBC Arusha inasema watu wapatao 20 wameathirika na mlipuko huo,na majeruhi wamekimbizwa hospitalini kwa matibabu.

Aidha inasema ibada hiyo imesitishwa na waumini wameruhusiwa kurudi majumbani kwao,Mgeni ambaye ni mwakilishi wa Papa ,Askofu,Mapadre na Masista wamo ndaini ya majengo ya kanisa hilo kwa usalama na kusubili hali iwe shuwari.

Pamoja na tukio hilo hadi sasa haijajulikana kuwa bomu hilo liliwekwa na nani,na kama mtu aliweka  alikuwa na nia gani ya kutaka kupoteza maisha ya melufu ya waumini wa kanisa hilo wasio na hatia.

Serikali mkoani Arusha tayari imesha wasili katika kanisa hilo akiwemo ,Kamanda wa Polisi  wa mkoa wa Arusha  na kwamba uchunguzi unaendelea kufanyika ili kubaini chanzo cha mlipuko huo na nani aliyehusika na tukio hilo.

Huwa tunasikia tu kuwa makanisa yanachomwa moto Zazibar leo,wa- Tanzania wameshuhudia Live mlipuko wa bomu, Hivi nchi hii imeingiliwa na Ugonjwa gani kwenye vichwa vya Watanzania ? tatizo liko  wapi, kama ni tikadi za vyama mbona kila mtu ni mfuasi wa chama fulani, haiwezekani kulazimishana kuingia kwenye chama ambacho mtu hakipendi.

Na hivyo hivyokwenye Imani za kidini kila mtu anaamua kufuata Dhehebu analoona akienda huko,huwenda akafika Mbinguni au kwa Mungu, Hatuwezi wote tukaenda kwenye madhehebu ambayo hatuyapendi. E Mungu, hebu angalia viumbe wako waliko, wamefikia hatua mbaya uwashushie upendo kupitia kwa Mitume wako uliyewatuma Duniani kuja kuwakomboa kutoka kwenye Utumwa wa dhambi. Wote tuna kuomba wewe, tofauti yetu ni majina tunayo kuita sisi wanadamu kulingana na makabila uliyo yagawa wewe mwenyewe Baba.

Lakini kama ni kikundi cha wafuasi au Itikkadi fulani, hawana nia nzuri kwa Taifa letu,Wameamua kuchafua jina la nchi yetu,watu wake na viongozi wake,huwenda kwa manufaa ya watu wachache wasiyopenda Amani ,Utulivu,Mshikamano na Umoja tulionao  Wa- tanzania

Friday, May 3, 2013

Breaking news, Janet Phelan comment on how journalists facing problems to do their job frely.


Our brothers and sisters in the Third World are being arrested and worse for their acts of honest reporting. In the First World, journalism has largely been reduced to the function of a scribe---writing down what those in power say. The intimidation of journalists in the First World has become systemic and remains one of democracy's dirty little secrets. ( source by Janet Phelan )

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII ASEMA OPERESHINI YA KUPAMBANA NA MAJANGILI WA WANYAMA PORI LAZIMA IFANYIKE, JANA BUNGENI DODOMA

 Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Kagasheki,alisema kuwa operesheni ya kupambana na majangiri wanao vamia hifedhi na kuu wanyama bila kuwa na kibali  Serikali itafanya peresheni hiyo kwa kusitukiza.Balozi Kagasheli alisema hayo wakati akijibu hoja mbalimbali za waheshimiwa Wabunge katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma jana.
Katika mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo,Mhe. Kagasheki alisema tatizo la ujangiri wa wanyama pori sio la Tanzania peke yake,bali ni kilio cha nchi nyingi zenye Game Reserve na National Parks ,alisema ujangiri umekuwa wa hali ya juu kwa sababu ya mahitaji ya pembe za ndovu na kifaru katika soko la dunia.

LEO NI SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI, LAKINI UHURU HUO WA VYOMBO HIVYO UPO, NA WANAOFANYA KAZI KATIKA VYOMBO HIVYO WANAO UHURU HUO TUNAO USHUHUDIA LEO ?,BASI MIE NILIPITA MITAA YA MANISPAA YA SONGEA MKOANI RUVUMA KAMA HIVYO

 Huu ni mmoja wa mtaa maarufu sana katika Manispaa ya Songea ,ambao leo siku ya Uhuru wa vyombo vya habari,Blog hii ilipitia,lakini palitulia sana,Wasomi wa Chuo kikuu cha Misheni walikuwa wakibukua kama kawaida yao.Aidha wafanya biashara wa maduka nao walikuwa wanaendelea.Nilijiuliza mbona watu wanaendelea kama vile hakuna tukio lolote.
 Lakini baadaye nilipata jibu kuwa Siku ya Uhuru wa vyombo vya habari ni kitu wanaokifahamu wenye vyombo hivyo pengine na baadhi ya wanaofanya kazi katika vyombo hivyo.Inawezekana hata Serikali hazijui kitu hiki,wala hata viongozi hawaoni umuhimu wa kitu hicho.Inafurahisha ni sawa na baadhi ya watu wanasema hawali nyama ya mbuzi ili mchuzi wake nitajaribu kunywa.sasa ule mchuzi umetokana na kitu gani.
Tanzania tumeshuhudia waandishi wa habari wanavyofanya kazi katika mazingira magumu,wengine wanapoteza maisha yao kwa ajili ya kuisemea jamii,Ndugu yetu Mpendwa Marehemu David Mwangosi Iringa alikufa kifo kibaya hata watoto na jamaa zake wakaribu hawata kisahau.Je huo ndiyo uhuru wenyewe wa vyombo vya habari.
Kinacho shangaza Serikali na Jamii inawaona waandishi waandishi wa habari kama adui,lakini wanapotaka kufanikisha majambo yao wanawatafuta haohao maadui, wakifanikiwa hawana thamani nao tena,kwa mwenendo huo tutakuwa na uhuru wa kweli wa vyombo vya habari nchini na nje ya nchi?
Sindiyo Uhuru huo wa vyombo vya habari leo na hali ndiyo hiyo Manispaa ya Mji wa Songea kupitia Chuo kikuu cha Songea kuelekea kanisani hadi Majengo.Hiyo ndiyo siku niliyoitumia katika manispaa hii.
Ukweli vyombo vya habari bado vinakazi kubwa, mpaka vitambulike na vyenyewe kuwa vinakuwa na siku rasmi na viongozi wa wa serikali na wanachi wafike kusikia vilio vyao,na vikasikilizwa.Na siyo kama kilio cha samaki machozi yakaenda na maji.( I wish you all the best Media houses , News Organizations and my collage Journalists, to celebrate well in the media day.}