WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe.Dkt Shukuru
Kawambwa ametangaza matokeo ya darasa la
saba mwaka 2012 ofisni kwake kwa waandishi wa habari na kusema wasichana
wamefanya vizuri kuliko wavulana kwa asilimia 8.8,baada ya kuongoza kwa
asilimia 50.20 kwa kuwapita wavulana kwa asilimia 49.80.
Waziri
huyo alisema kuwa wanafunzi 560,706 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza
katika shule za serikali,na kati yao
wanafunzi 281,460 ni wasichana na 279,246 wavulana ambapo imefanya idadi ya
wanafunzi waliochaguliwa kuongezeka kwa asilimia 8.8, ikilinganishwa na
wanafunzi 515,187 ya waliyochaguliwa mwaka uliyopita.
Mhe.
Kawambwa alisema mtihani wa mwaka huu umefanyika kwa mara ya kwanza kwa kutumia
Teknolojia mpya ya ‘ optical mark reader’ ambao usahihishaji wake hutumia
compyuta,njia ambayo imeipunguzia serikali gharama ikilinganishwa na mwaka
jana.
Alisema
kuwa mwaka jana walimu 4,000 walitumika kusahihisha zaidi ya mwezi mmoja,ambapo
mwaka huu 285 ndiyo walitumika kwa siku 15 kukamilisha kazi yote.
Kuhusu
matokeo hayo amesema kuwa alama ya juu kabisa ni 234 kati ya 250 kwa wavulana
na wasichana, ambapo wanafunzi 3,087 wamepata alama daraja la ‘A’ na wanafunzi
40,683 alama daraja la ‘B’,wanafunzi 222,103 alama daraja la ‘C’ na wanafunzi
526,397 alama daraja ‘D’ ambapo waliobakia 73,264 alama daraja ‘E’
Aidha
alisema vitendo vya udaganyifu vimepungua kutoka wanafunzi 9,736 waliofutiwa
matokeo yao mwaka jana ikilinganishwa na
wanafunzi 293 waliofutiwa matokeo yao
mwaka huu.
No comments:
Post a Comment