Saturday, December 22, 2012

MINAZI NA FAIDA ZAKE KWA WAKULIMA WA ZAO HILO

 Mnazi ni zao ambalo linampa mkulima faida nyingi,Nazi kama kiungio cha mboga lakini pia kuna kilevi kiitwacho tembo,' Waswahili wana msemo usemao kukimsifia mgema Tembo hulitia maji' , dafu ni nazi ambayo haijakomaa ambayo ni laini na ina maji ya madafu,kifuu cha  nazi hutumika kama kuni,pia hutumika kwa kutengeneza mapambo.
Aidha kifuu hicho hicho hutumika kama chombo cha kuchotea maji, uji kwa jina jingine huitwa upawa,lakini machicha ya nazi hiyohiyo hutumika kama kashata.Nazi ikipelekwa kiwandani yanapatikana mafuta ya nazi ambayo ni mafuta ya nywele.
Matumizi mengine yatokanayo na zao la mnazi ni majani ya mnazi ambayo hutumika kama:-
  • Chelewa kwa fanyia usafi Mifagio
  • Chelewa hutumika kama mitego ya kutegea samaki ( migono ).
  • Majani ya minazi hujulikana kama makuti,makuti hayo hutumika kuezekea nyumba, kujengea ua wa kuoga na pia hutumika kwa kusukwa kwa ajili ya kuchukulia maembe, nazi , na vitu vingine.
  • Mti wa mnazi hutumika kwa ajili ya ujenzi wa nyumba wengine hupasua mbao na kuzifanya boriti za kuezekea nyumba.
  • Nazi inapo fuliwa yale yanayotolewa ili nazi ibakie kuwa nazi kwa ajili ya matumizi,hutumika kama kuni, na matuimizi mengine ambayo wakulima hao wanajua.
Hiyo ni minazi ya siku nyingi ambayo ni mirefu.Lakini kwa sasa kuna minazi ya muda mfupi inavunwa,inasemekana ina shambuliwa na maradhi,na nimifupi.
Hawa ni wakazi wa Pwani ya Lindi,ambao zao lao la biashara ni mnazi.

No comments:

Post a Comment