Monday, December 31, 2012
SENSA MWAKA 2012 TANZANIA ILITOA AJIRA KWA VIJANA ASEMA PINDA
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mizengo Pinda pia mwenyekiti wa Kamati kuu ya Sensa Taifa,alisema Sensa ya mwaka 2012 imetia ajira ya muda kwa vijana ambao walikuwa makarani wale wasiyo na kazi.
Aidha Mhe.Pinda alisema katika zoezi la Sensa ya mwaka huu watu wanne ( 4 ) walipoteza maisha na wengine walipata majeraha mbalimbali..
Mhe.Pinda alisema hayo siku ya uzinduzi wa matokeo ya Sensa ya awali katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam leo.Ambapo Rais Kikwete alizindua matokeo hayo.
Aidha Mhe.Pinda alisema katika zoezi la Sensa ya mwaka huu watu wanne ( 4 ) walipoteza maisha na wengine walipata majeraha mbalimbali..
Mhe.Pinda alisema hayo siku ya uzinduzi wa matokeo ya Sensa ya awali katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam leo.Ambapo Rais Kikwete alizindua matokeo hayo.
WATANZANIA TUPO WATU 44,929,002,AMBAPO TANZANIA BARA 43,625,434 NA ZANZIBAR WATU 1,303,568 ATANGAZA RAIS KIKWETE
Mhe.Dkt Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua Sensa ya watu na makazi Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam leo atangaza Kuwa Tanzania ina watu 44,929,002.Tanzania Bara watu 43,625,434 na Zanzibar watu 1,303,568.
Waziri wa Fedha Mhe, Wili
Mkamu wa Rais Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali akielezea mafanikio ya zoezi la Sensa mwaka 2012
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia mwenyekiti wa Sensa Taifa akielezea mafaniko ya sensa hiyo katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam leo.
Mariam Kan Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa akielezea jinsi Tanzania ilivyofanikisha zoezi hilo kwa malengo ya kupanga bajeti kwa maendeleo ya nchi.
Msomaji wa Utenzi Bi Amina Haji kutoka Zanzibar katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam Leo.
Waziri wa Fedha Mhe, Wili
Mkamu wa Rais Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali akielezea mafanikio ya zoezi la Sensa mwaka 2012
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia mwenyekiti wa Sensa Taifa akielezea mafaniko ya sensa hiyo katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam leo.
Mariam Kan Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa akielezea jinsi Tanzania ilivyofanikisha zoezi hilo kwa malengo ya kupanga bajeti kwa maendeleo ya nchi.
Msomaji wa Utenzi Bi Amina Haji kutoka Zanzibar katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam Leo.
RAIS KIKWETE ATANGAZA MATOKEO YA AWALI YA SENSA YA WATU NA
MAKAZI KUWA TANZANIA INA WATU 44,929,002 KATIKA
VIWANJA VYA MNAZI MMOJA LEO, TAREHE 31 DESEMBA 2012 DAR ES SALAAM
RAIS Kikwete alisema kuwa uzinduzi huu wa awali siyo kuwa
kuna matokeo mengine la bali yamekamilika isipokuwa mwezi Februari 2013
kutakuwepo na matokeo ya idadi ya watu kijinsia.kujua wanaume ni wanagapi na
wanawake ni wangapi.
Alisema kuwa katika matokeo hayo,Tanzania Bara kuna indadi
ya watu 43,625,434 na Zanzibar kuna watu 1,303,568.
Aidha alisema pamoja na changamoto kadhaa zilizojitokeza
lakini zoezi hilo
limefanikiwa kwa asilia 90.
Baadhi ya changamoto hizo ni pamoja na maandamano wakati wa
zoezi liliendelea,watu kujifungia ndani kwa kukataa kuhesabiwa.
Alisema matokeo ya idadi ya watu imeonyesha jinsi watu
wanavyoongezeka, na kwamba mwaka 2016 idadi ya Watanzania itakuwa 51,600,000,hivyo
ni mzigo mkubwa kwa Taifa na Serikali pia na jamii kwa ujumla.Hivyo serikali
itapanga mipango yake ya maendeleo ili kukabiliana na idadi kubwa ya
watu,lakini pia watanzania wafuate uzazi wa mpango kwa lengo la kuzaa watoto
ambao wataweza kuwahudumia.
Saturday, December 29, 2012
NAWATAKIENI HERI ,MAFANIKIO,AMANI,UPENDO NA MATUMAINI KWA MWAKA 2013
Naomba wasomaji wa Blogs waendelee kusoma Blogs mwaka mpya wa 2013 kama walivyosoma mwaka uliyopita wa 2012.Tumshukuru Mungu kwa kutulinda hadi kufikia mwaka mwingine,hasa kwa kushiriki katika sikukuu ya X mas,ambapo kuna watu hawakufanikiwa kushiriki siku hiyo ingawa walitamani sana.
Nikiwa katika Blog yangu nikiwatakia wasomaji wangu ,heri ya Mwaka mpya wa 2013,Asanteni sana,Tuombeane maisha mema na marefu.
Nikiwa katika Blog yangu nikiwatakia wasomaji wangu ,heri ya Mwaka mpya wa 2013,Asanteni sana,Tuombeane maisha mema na marefu.
KARIBU MWAKA 2013,KWAHERI ANOLOJIA,KARIBU DIJITALI
Wakati watu anajiandaa kuupokea mwaka 2013,Pia watu anajiandaa katika matumizi ya Dijitali,baada ya kufunga kwa matumizi ya Anolojia
Katika Manispaa ya Dodoma mistari mirefu nimekuwa ikionekana katika maduka ya STAR TIMES kununua Ving'amuzi kwa kuhofu ya kumalizika kwa vifaa hivyo katika maduka hayo.
Hiyo ni dalili nzuri kuwa watu sasa kuwa wanakwenda sambamba na matumizi ya Teknolojia ya kisasa katika matumizi ya mitandao mbalimbali kulingana na mabadiliko ya matumizi ya mitanadao mbalimbali inayo buniwa kila kukicha.
Monday, December 24, 2012
Sunday, December 23, 2012
NYAISONGA AWAPA MAADILI YA KIDINI WATOTO WA KIPEMARA DODOMA
Baba Askofu Grevasi Nyaisonga wa Jimbo la Dodoma akitoa mahubiri kwenye maazimisho ya misa Takatifu ya Kipeimara katika Parokia Ya Mt Kalori Lwanga ya Makole Katika Manispaa ya Dodoma.
Baadhi ya watoto waliyopata Kipeimara leo katika Parokia ya Makole leo.
Waumini waliohudhuria ibada hiyo ya Kipeimara leo
Ni kwa ya Mtakatifu Kalori Lwanga ya Makole ikiinjisha kwa nyimbo katika ibada iliyofanyika leo Parokiani hapo.
Askofu akitoa Kipeimara kwa kumweka Ishara ya Msalaba kwa mafuta na kofi shavuni .
Wakiwa katika mageuzi ya mkate na divai
Akionyesha kikombe cha divai kama ishara ya Damu ya Yesu,iliyo mwangika kwa ajili ya wengi kwa maondoleo ya dhambi
Askofu Nyaisonga akimpa mkono mmoja wa waumini waliyo hudhuria misa hiyo leo.
Askofu Nyaisonga akitoa Baraka kwa waumini kanisani humo baasa ya Ibada hiyo hivi leo.
Baadhi ya watoto waliyopata Kipeimara leo katika Parokia ya Makole leo.
Waumini waliohudhuria ibada hiyo ya Kipeimara leo
Ni kwa ya Mtakatifu Kalori Lwanga ya Makole ikiinjisha kwa nyimbo katika ibada iliyofanyika leo Parokiani hapo.
Askofu akitoa Kipeimara kwa kumweka Ishara ya Msalaba kwa mafuta na kofi shavuni .
Wakiwa katika mageuzi ya mkate na divai
Akionyesha kikombe cha divai kama ishara ya Damu ya Yesu,iliyo mwangika kwa ajili ya wengi kwa maondoleo ya dhambi
Askofu Nyaisonga akimpa mkono mmoja wa waumini waliyo hudhuria misa hiyo leo.
Askofu Nyaisonga akitoa Baraka kwa waumini kanisani humo baasa ya Ibada hiyo hivi leo.
WATAKIWA KUISHI KWA IMANI
KWA KUYASHINDA MAGUMU KATIKA MAISHA WATOTO WA KIPEIMARA DODOMA
ASKOFU wa Jimbo la Dodoma
Mhashamu Grevasi Nyaisonga ,amewataka watoto waliopata Kimeimara wawe mashaidi
wa Yesu Kristo kwa vitendo kwa ndani na nje,hasa katika kufuata imani ya kweli
ya upendo mbele za Mungu na watu wote.
Baba Askofu Nyaisonga
alisema kuwa kipemara kimewapa nguvu ya kuyashinda magumu katika maisha yao kwa mapenzi ya Mungu
na kuwafanya askari imara wa Mungu kwa kuwa mashuhuda wa Yesu Kristo.
Askofu Nyaisonga ametoa
Kipeimara kwa watoto 300 katika Parokia ya Mtakatifu Karoli Lwanga ya Makole
katika Manispaa ya Dodoma Mkoa wa Dodoma Leo.
Aidha amesema kuwa katika
kuchangia kwaya ya Mt.Kalori Lwanga ya Makole,waumini wanunue kanda zao zenye
nyimbi za Unjilishaji za VIDEO,Pia wanunue na Kalenda ambazo zinaweza kuingizia
Parokia mapato yake.
Wakati huohuo Mwenyekiti
wa Parokia hiyo Bwana Evarist Mnaranara
amemshukuru Baba Askofu kwa kuwapa Kipeimara watoto
hao,amewashukuru,Makatekista, na wazazi kwa kuwaandaa watoto hao katika
mafundisho ya dini hadi kufikia kupata kipemara hicho.
Pia alisema pamoja na
msimu wa mvua ,watu wafanye kazi kwa juhudi kubwa,na wakulima waende shamba
maana msimu wa kilimo umeshaanza,kwa kufanya hivyo kutapatikana chakula cha
kustosha kwa ajili ya familia zao.
Saturday, December 22, 2012
MINAZI NA FAIDA ZAKE KWA WAKULIMA WA ZAO HILO
Mnazi ni zao ambalo linampa mkulima faida nyingi,Nazi kama kiungio cha mboga lakini pia kuna kilevi kiitwacho tembo,' Waswahili wana msemo usemao kukimsifia mgema Tembo hulitia maji' , dafu ni nazi ambayo haijakomaa ambayo ni laini na ina maji ya madafu,kifuu cha nazi hutumika kama kuni,pia hutumika kwa kutengeneza mapambo.
Aidha kifuu hicho hicho hutumika kama chombo cha kuchotea maji, uji kwa jina jingine huitwa upawa,lakini machicha ya nazi hiyohiyo hutumika kama kashata.Nazi ikipelekwa kiwandani yanapatikana mafuta ya nazi ambayo ni mafuta ya nywele.
Matumizi mengine yatokanayo na zao la mnazi ni majani ya mnazi ambayo hutumika kama:-
- Chelewa kwa fanyia usafi Mifagio
- Chelewa hutumika kama mitego ya kutegea samaki ( migono ).
- Majani ya minazi hujulikana kama makuti,makuti hayo hutumika kuezekea nyumba, kujengea ua wa kuoga na pia hutumika kwa kusukwa kwa ajili ya kuchukulia maembe, nazi , na vitu vingine.
- Mti wa mnazi hutumika kwa ajili ya ujenzi wa nyumba wengine hupasua mbao na kuzifanya boriti za kuezekea nyumba.
- Nazi inapo fuliwa yale yanayotolewa ili nazi ibakie kuwa nazi kwa ajili ya matumizi,hutumika kama kuni, na matuimizi mengine ambayo wakulima hao wanajua.
Hawa ni wakazi wa Pwani ya Lindi,ambao zao lao la biashara ni mnazi.
MIKOKO NA MIMEA IOTAYO PEMBENI MWA BAHARI NI FAHARI KWA VIUMBE VYA BAHARINI,HIVYO WAKAZI WA MWAMBAO MWA BAHARI AITUNZE KUHIFADHI MAZINGIRA YAKE
Mazingira mazuri yanayovutia ya mikoko katika Bahari ya Hindi, unapoingia mkoani Lindi, utakutana na mikoko hiyo ambayo ni masikani ya viumbe vyote viishivyo Baharini.
Wananchi waishio mwambao mwa bahari hiyo ni juu yao kuhifadhi mazingira ya kandokando mwa baharihiyo ili sura ya bahari iendelee kuvutia.Friday, December 21, 2012
MATUMIZI YA MAJI YAWE SAFI NA SALAMA JE KWA WATUMIAJI WA MAJI HAYA UNAMAONI GANI?
Je unasemaje kuhusu matumizi ya maji haya ni safi na salama ?, mito maji yake ni kama hivyo wengine wanaoga na kufua juu na nyie huku chini mnayachota kwa matumizi ya kunywa,je ni salama ?
Maji yanakawaida ya kusomba kila kitu,kwa hiyo watumiaji hao wanaoga mchanganyiko huo,na kuyanywa kawa mtindo huohuo.
Maji yanakawaida ya kusomba kila kitu,kwa hiyo watumiaji hao wanaoga mchanganyiko huo,na kuyanywa kawa mtindo huohuo.
TUJIFUNZE BLOG IMETOKANA NA JINA LA GAZETI LA KUSINI LA TUJIFUNZE TOLEO Na.6 LA OKTOBA - DASEMBA 2012
Hilo ni toleo Na.6 la Oktoba - Desmba 2012 la TUJIFUNZE,Ambapo lead ni Kilio cha wakulima wa korosho nchini kilio chao kimesikika - asema katibu Mkuu wa CCM Mhe.Abdulrahamn Kinana Mtwara.
Wakati sub lead Dr.Huvisa atoa msaada wa vifaa tiba kwa hospitali za mkoa na wilaya, Mkoani Ruvuma.Front page.
Upande wa Mafunzo maalumu ,Makumbusho ya Majimaji ni kivutio kwa watalii,Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii Bi.Maimuna Tarishi.Ambapo upande wa michezo Timu ya majimaji wafunguka kwa maandalizi ya kurejea Vodacom msimu ujao.
Wakati sub lead Dr.Huvisa atoa msaada wa vifaa tiba kwa hospitali za mkoa na wilaya, Mkoani Ruvuma.Front page.
Upande wa Mafunzo maalumu ,Makumbusho ya Majimaji ni kivutio kwa watalii,Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii Bi.Maimuna Tarishi.Ambapo upande wa michezo Timu ya majimaji wafunguka kwa maandalizi ya kurejea Vodacom msimu ujao.
UPANUZI WA BARABARA JIJINI DAR ES SALAAM WAENDA SAMBAMBA NA UJENZI WA DARAJA LA JUU KIMALA KAMA LILE LA MANZESE
Hilo ni daraja la juu la Kimara Jijini Dar es Salaam kama lilivyo la Manzese,ikiwa ni upanuzi wa Barabara za Jijini Dar es Salaam ili kupunguza msongamano wa magari jijini humo.Ni juhudi za serikali za kuboresha miundombinu ya barabara zake nchini.
Ni nguzo za daraja hilo ambazo bado kuweka daraja hilo.
Ni nguzo za daraja hilo ambazo bado kuweka daraja hilo.
WASICHANA WA FANYA MAAJABU KATIKA MATOKEO YA DARASA LA SABA MWAKA 2012 KWA ASILIMIA 8.8 KWA KUWAPIKU WAVULANA
WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe.Dkt Shukuru
Kawambwa ametangaza matokeo ya darasa la
saba mwaka 2012 ofisni kwake kwa waandishi wa habari na kusema wasichana
wamefanya vizuri kuliko wavulana kwa asilimia 8.8,baada ya kuongoza kwa
asilimia 50.20 kwa kuwapita wavulana kwa asilimia 49.80.
Waziri
huyo alisema kuwa wanafunzi 560,706 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza
katika shule za serikali,na kati yao
wanafunzi 281,460 ni wasichana na 279,246 wavulana ambapo imefanya idadi ya
wanafunzi waliochaguliwa kuongezeka kwa asilimia 8.8, ikilinganishwa na
wanafunzi 515,187 ya waliyochaguliwa mwaka uliyopita.
Mhe.
Kawambwa alisema mtihani wa mwaka huu umefanyika kwa mara ya kwanza kwa kutumia
Teknolojia mpya ya ‘ optical mark reader’ ambao usahihishaji wake hutumia
compyuta,njia ambayo imeipunguzia serikali gharama ikilinganishwa na mwaka
jana.
Alisema
kuwa mwaka jana walimu 4,000 walitumika kusahihisha zaidi ya mwezi mmoja,ambapo
mwaka huu 285 ndiyo walitumika kwa siku 15 kukamilisha kazi yote.
Kuhusu
matokeo hayo amesema kuwa alama ya juu kabisa ni 234 kati ya 250 kwa wavulana
na wasichana, ambapo wanafunzi 3,087 wamepata alama daraja la ‘A’ na wanafunzi
40,683 alama daraja la ‘B’,wanafunzi 222,103 alama daraja la ‘C’ na wanafunzi
526,397 alama daraja ‘D’ ambapo waliobakia 73,264 alama daraja ‘E’
Aidha
alisema vitendo vya udaganyifu vimepungua kutoka wanafunzi 9,736 waliofutiwa
matokeo yao mwaka jana ikilinganishwa na
wanafunzi 293 waliofutiwa matokeo yao
mwaka huu.
Monday, December 17, 2012
WAKUU WA VITUO VYA KANDA SABA ZA MAGAZETI YA KISOMO WAMETAKIWA KUSIMAMA NA KUJENGA USHIRIKIANO KATIKA UTENDAJI KAZI ZAO
Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima na Nje ya Mfumo Rasmi Bwana Salumu Mnjagila akiwasomea vipengere vya fomu za PRAS Wahariri wa Magazeti vijijini wa Kanda saba katika ofisi yake Mkao Makuu ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi ya washiriki katika kikao hicho cha kazi wakimsikiliza Mkurugenzi kwa makini
Naibu Mkurugenzi Kisomo Mwanza Bibi Mary Joseph Salu
Picha ya Pamoja ya viongozi wa Idara ya Elimu ya Watu Wazima na Nje ya Mfumo Rasmi na Baadhi ya wahariri wa magazeti vjijini
Mkurugenzi Msaidizi Utawala Bw.Gange akitoa mada ya OPRAS kwa Wahariri wa Vituo vya uchapaji
Baadhi ya washiriki katika kikao hicho cha kazi wakimsikiliza Mkurugenzi kwa makini
Naibu Mkurugenzi Kisomo Mwanza Bibi Mary Joseph Salu
Picha ya Pamoja ya viongozi wa Idara ya Elimu ya Watu Wazima na Nje ya Mfumo Rasmi na Baadhi ya wahariri wa magazeti vjijini
Mkurugenzi Msaidizi Utawala Bw.Gange akitoa mada ya OPRAS kwa Wahariri wa Vituo vya uchapaji
WAKUU wa vituo wa Kanda saba
za magazeti ya kisomo
nchini,wametakiwa kusimama kwa ushirikiano na mshikamano wao katika
ufanisi wa kazi zao za kuelimisha wananchi kupitia magazeti yao ya kisomo
yanayo chapwa katika Kanda zao.
Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima na Nje ya
Mfumo Rasmi EWW/ENMRA Bwana salumu Mnjagila alisema hayo wakati wa kikao cha
kazi kilicho fanyika ofisni kwake leo Makao makuu ya Wizara ya Elimu na Mafunzo
ya Ufundi JIjini Dar es Salaam.
Bw.Mnjagila alisema kila mmoja atambue nafasi
yake kituoni ili kuleta ufanisi wa kazi bila ya kusababisha migongano baina ya viongozi
na watumishi katika vituo hivyo.
Aidha
alisema vituo hivyo vitafanya kazi za maendeleo ya kuboresha elimu nchini iwapo watafanya kazi kwa
kuelewana na kuwa wawazi katika maamuzi
ya utekelezaji wa majukumu waliyo jipangia.
Kikao
hicho kilijumuishi Msaidizi Utawala Bwana Gange na Mkurugenzi Msaidizi Ufuatiliaji
wa Taaluma Bibi Revilla na Wahariri wa
Vituo vya Uchapaji Magazeti Vijijini vya Mwanza,Tabora,Mbeya na Songea, ambao
pia ni wakuu wa vituo hivyo.
Sunday, December 2, 2012
Meya Mhagama alisema hayo katika mahafari ya shule ya Awali Charity iliyoko katika Uwanja wa sabasaba Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma jana,na kwamba katika harambee iliyofanyika katika mahafali hayo,Mstahiki Meya Mhagama aliahidi kutoa malori mawili ya mchanga yenye thamani ya shilingi laki tatu ( 300,000/= ),ambapo Yusufu Kufakunoga,kwa niaba ya Mhariri kanda ya kusini aliahidi kuchangia mifuko mitatu ( 3 ) ya sementi,Mtangazaji wa Star TV Songea Bwana Adam Nindi aliahidi kuchangia Shilingi 20,000/=.
Watoto 13 wamehitimu mafunzo ya Awali,ambapo mwakani watoto hao wataingia darasa la kwanza.Katika picha,wakwanza mwenye suti ya bluu ni mwalimu mkuu,pia ni mkurugenzi wa shule hiyo anayemfuatia mwenye kaunda suti mikono mifupi na Mstahiki Meya Charles Mhagama akimkabidhi cheti mmoja wa wahitimu.
Subscribe to:
Posts (Atom)