Shekhe Himidi Jongo akielezea umuhimu wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambapo leo ni mfungo mosi.Aidha na kuwaomba wafanya biashara nchini kuacha kupandisha bidhaa bei.
Wafanya biashara wameshauriwa kuacha kupandisha vitu bei kwa
sababu ya mfungo wa Ramadhani,Shekhe Hamidi Jongo wa Dar es Salaam alisema hayo kwenye kipindi
maalumu cha TBC jana wakati akielezea umuhimu wa kufunga kwa waumini wa Dini ya
Kiislam.
Alisema Mungu alihalalisha biashara kufanyika na
aliharamisha riba katika biashara,hivyo kufanya bishara siyo dhambi bali kupandisha vyakula wakati huu wa mwezi
Mtukufu wa ramadhani ni dhambi kwani bei ya jana kabla ya mfungo kwa
nazi,mhogo,mchele kwanini leo siku ya mfungo mosi ipande? ‘Wasifanye mwezi
Ramadhani uwe ni mwezi wa Majonzi na majuto badala ya faraja kwa wanaofunga’
alisema Shekhe Jongo.
Aidha alisema kwa mfanya biashara wa Kiislamu awe mkweli kwa
wateja wake wakifika kununua mchele au maharage asema kweli kuwa maharage yake
yanaiva haraka au yanachelewa kuliko kusema maharage yake ni maji mara moja
kumbe uongo.Mtu kama huyo asifunge maana
atakuwa anapoteza muda wake bure.
Tuungane na Shekhe
Jongo kuwahasa wafanya biashara wa mhogo,maharage,nazi,tambi,tende wauze
bidhaa hizo kwa bei ya halali,wasipandishe bidha hizo muhimu kwani kufanya
hivyo ni kuwakomoa wenzetu watakaojaliwa
kufunga,kwani mwezi huu ni mwezi Mtukufu
kwa waumini wa Kiislamu.
Kila unapofika Mwezi Mtukufu, tunasikia taarifa za huu ufisadi wa kupandisha bei. Sijui kama hao mafisadi ni wa dini gani au labda ni makafiri. Ingekuwa bora kama kungekuwa na utaratibu wa kuwataja, ili ijulikane hao wahujumu wa dini ni akina nani.
ReplyDelete