Thursday, July 5, 2012

CHUO KIKUU SAUT TAWI LA SONGEA KUONGEZA KUWA NA VITIVO VITANO KUANZIA SEPTEMBA 2012

Profesa Donatus Albert Komba akiwa Ofisini kwake katika Chuo Kikuu cha SAUT Tawi la chuo Kikuu cha SAUT Mwanza Mjini Songea.kk






\[CHUO KIKUU TAWI LA SAUT CHA SONKUANZIA SEPTEMBER 2012
MKURUGENZI  wa chuo hicho Profesa Donatus Albert Komba alisema hayo ofisini kwake leo kwa waandishi wa habari waliyotembelea chuoni hapo katika Manispaa ya Songea, kuona na kupata maelezo ya mafanikio ya chuo hicho ambacho ni tawi la chuo kikuu cha SAUT cha Jijini Mwanza.
Profesa Komba alisema kuwa chuo kinatarajia kuwa na vitivo sita kuanzia mwezi September mwaka huu,alivitaja vitivo hivyo kuwa ni pamoja na ‘Education, Law, Business Administration,Sociology, Mass Communication, and Medicine’.
Alisema kuanzia mwezi Septemba 2012 chuo kitapokea wanafunzi wanafunzi wengi ikilinganishwa na sasa wachache ambao ni 176 kati yao wavulana108 na wasichana78.na walimu 13 na wafanyakazi ambao si walimu 17.
Kuhusu ada inayolipwa katika chuo hicho ni Tshs.2,600,000 kwa wanafunzi wa Kitivo cha Medicine ambapo Bodi ya mikopo huwakopesha kiwango chote hicho kutokana na umuhimu wao.
Aidha kwa vitivo vingine ada ni Tshs.950,000 kwa mwaka ambayo hulipwa kwa awamu mbili.ambapo Bodi ya mikopo huwakopesha Tshs.475,000/= kiasi kinacho salia hulipa wenyewe.
Alisema kuwa wanfunzi 50 wa kitivo cha Medicine kitaanzia Songea wakati miundombinu ya chuo kikuu cha tiba ikikamilishwa Peramiho,ikikamilika watakwenda kuendelea na masomo yao kwa mika mitano huko Peramiho.
Hilo ni jengo la Utawala la chuo kikuu cha SAUT Songea

.

No comments:

Post a Comment