CHUO KIKUU CHA SAUT SONGEA
KUONGEZA VITIVO
MSHAURI wa wanachuo ( Dean of
Student ) Michael Sinienga alisema hayo hivi karibuni kwa waandhishi wa habari
wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi wa Kanda ya Kusini walipotembelea chuo
hicho kwa lengo la kupata taarifa za mafanikio na changamoto kadhaa tangu chuo
hicho kianze kudahili wanachuo wake.
Bwana Sinienga alitaja vitivo vitakavyo
ongezeka kuwa ni pamoja na ‘Business Administration, Law, Medicine, Mass
Communication and Education’ ambayo
ndiyo iliyoanza.
Matarajio
mengine ya chuo hicho ni kutoa kozi fupifupi za ujasiliamali, kozi za jioni
‘Evening classes’ kwa watumishi na watu
wengine wenye kutaka kusomea shahada wakiwa kazini.
Matarajio mengine ni kutoa huduma kwa shule za
sekondari ambazo zitakuwa na uhaba walimu na zikipenda kupata huduma hiyo
kutoka katika Chuo Kikuu hicho, Pia kuwaandaa vijana kujiamini na kujitambua na
maadili kuwekewa kipaumbele.
Nilipata fursa, juzi Jumamosi, ya kutembelea chuo hiki kipya. Alinitembeza mwenye kigoda wa chuo, Profesa Donatus Komba, akanieleza mengi kuhusu historia, mipango, na changamoto za chuo hiki. Niliondoka nikiwa nimefahamu mengi na pia nikiwa na ari ya kuchangia juhudi za hao wenzangu.
ReplyDelete