Sunday, July 8, 2012

Serikali kuitoa asilimia 70 ya wakulima wa Tanzania wanaotumia jembe la mkono kwenda kwenye kilimo cha kisasa cha matrekta.

 Waziri Mkuu Mizengo Pinda watatu kutoka kulia akipungia wananchi mkono  wa kwaheri jana katika uwanja wa zimanimoto Katika Manispaa ya Songea baada ya kuzindua matrekta 53 yaliyokopeshwa kwa wakulima wa Mkoa wa Ruvuma.
 Baadhi ya Matrekta yaliyo kabidhiwa jana kwa wakulima wa wilaya za Songea Manispaa,Songea Vijijini,Namtumbo ,Mbinga na Tunduru ambako wengi waliyachukua mayterkta hayo
 Mhe.Pinda akizindua trekta lililo kopwa na Mkuu wa Koa wa Ruvuma Mhe,Said Thabit Mwambungu.
 Waziri Mkuu akisalimiana na viongozi na baadhi ya wananchi waliofika kumpokea uwanjani katika uwanja wa ndege Songea Juzi alipoa anza ziar yake ya siku mbili mkoani Ruvuma juzi.
Mhe.Mizengo Pinda.


Ili kuitoa asilimia 70 ya Wa- Tanzania wanaotumia jembe la mkono kwa kilimo,
Serikali imeweka mkakati wa kuhamasisha wakulima kutumia matrekta katika kilimo chao badala jembe la mkono.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda alisema hayo jana katika uwanja wa Zimani moto katika Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma ,wakati wa kuzindua mradi wa matrekata 53 ambayo yamekopeshwa kwa wananchi na wakulima kwa lengo la kumtoa mkulima kutoka matumizi ya jembe la mkono.
Alisema serikali imeagiza zaidi ya  amatrekta 1,600 kutoka nchini India kwa mkopo ambayo yapelekwa mikoani kwa mpango wa kuyakopesha wananchi kwa bei nafuu ambayo yatalipwa ndani ya miaka mnne.
   Aidha alisema kuwa uwezo wa trekta ni kulima heka 25 hivyo mmliki wa trekta anaweza akakodisha kwa wakulima wengine nao wakaachana na jembe la mkono.
  Alisema Halmashauri na vyama vya Ushirika wachukue matrekta hayo ili wawezi kukopesha wananchi wanye kutaka kutumia trekta katika kilimo.
         Pamoja na mambo mengine Waziri Mkuu waliwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi wakati Tume ya Katiba inapofika katika mikoa yao ambapo Tume hiyo imeanza katika mikoa 8 isitosha alihimiza kwa wananchi usiku wa kumkia tarehe 25  mwezi wa 8 mwaka huu, kila mwananchi atahesabiwa ni siku ya Sensa Kitaifa ameomba wannanchi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa makarani wa sensa wanapopita katika kaya zao siku hiyo.

No comments:

Post a Comment