Thursday, July 19, 2012

NI JAMBO LA KUFURAHISHA LA KUKUTANA NA BLOGGER MKUBWA NA KUCHATI NAE INAPENDEZA KWELI SI MWINGINE PROFESA MBELE - SONGEA LEO

 Baada ya mapumziko ya safari ya basi kutoka Dar es Salaam kuja hapa Songea Profesa Mbela mwenye shati la mistari pamoja na ndugu zake picha ya pamoja katika ukumbi wa Serengeti ,maarufu sana hapo Songea kwa kupata moja baridi na moto pia,
Hapa Prf.Mbele anajikumbusha kivywaji cha nchi yake almaarufu Kili- manjaro akiwa na Dada Sia  katika ukumbi wa Serengeti Manispaa ya Songea,Prf.Mbele pamoja na kuishi nchini Marekani kikazi,lakini hukumbuka kurudi nchini kwakwe na hasa mkoani kwake na wilayani kwake Mbinga.
Profesa Mbele anaamini kuwa usomi haupungui iwapo msomi akijichanganya na watu wa kawaida,na wala akiwa akiongea na vijana wa vijiweni,Hawampunguzii Uprofesa wake,maana kazi ya Mungu ni kubwa kwa kuwa siyoyote yanayo zungumzwa na watu wa kawaida ni vya upuuzi la,ila kuna mengine yana maana huenda hata alipokuwepo chuoni hakuwahi kusikia.
Mie na mpongeza sana Profesa huyo,kwa kuwa anatambua kuwa kila mmoja na mchango wake katika jamii kulingana na kiwango chake cha elimu au cha uelewa wake kasoma au hapana,endelea hivyo profesa Mbele kwa mtindo huo utachota mambo mengi yanayoizunguka dunia hii.

2 comments:

  1. Hongera sana kwa kukutana na Prof. Mbele mie tulipishana sana mwka jana. Ni jambo nzuri sana kwa kweli kukutana hivi na kubadilisha mawazo.

    ReplyDelete
  2. Dada Yasinta, nami nakumbuka tulivyopishana mwaka jana. Haikuwa bahati yetu kukutana, ingawa nilifika hadi Ruhuwiko, kumtembelea dada yangu. Na safari hii nilienda tena hadi Ruhuwiko.

    Na nikirudi kwenye hii taarifa ya Mheshimiwa Sikapundwa, ni ukweli kuwa tulifurahi kukutana na kuongelea mambo kadha wa kadha. Nami nitaleta picha za tukio hilo katika blogu yangu.

    ReplyDelete