BADHI ya wanafunzi wa shule ya
msingi Kambarage Halmashauri ya Manispaa ya Songea wamempatia mkong’oto mwalimu
aliyejulikana
kwa jina la Kahimba kwa madai ya kuwa na kuherehere cha kufundisha wakati
walimu wengine wapo kwenye mgomo ulifanyika nchi nzima,wakidai kuwa mwalimu
huyo amewasaliti walimu wenzake na viongozi wa Chama cha Walimu Tanzania.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kambarage Bibi
Adolophine Ndunguru katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea alithibitisha
tulio hilo kuwa
lilitokea majira ya asubuhi.
Aidha Katibu wa Chama Cha Walimu Tanzania wa
Mkoa wa Ruvuma Bwana Luya Ngonyani,alisema kuwa Mgomo wa Walimu ni halali
umezingatia sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004.
Alisema kuwa hatua ya kwanza ya
Chama Cha Walimu (CWT ) imetekeleza kutangaza
mgogoro wa siku 30 kwa kujaza fomu namba 1 kwa lengo la kudai maslahi yao.
Wakati Uongozi wa Manispaa ya Halmashauri
ya Songea wakitaka kuitisha mkutano wa Waratibu Elimu Kata na Walimu wakuu wa shule
wa Manispaa hiyo leo katika shule ya msingi Mfaranyaki uligonga mwamba baadaya wa
Waratibu na walimu wakuu hao kuacha kwenda kwenye mkutano huo.
Serikali isifanyie mzaha kuhusu tukio hilo,sio suala la kusema shauri lipo mahakamani ,walimu warudi shuleni kufundisha,Sekta ya Elimu ni Sekta nyeti si ya kuichezea chazea kama wengine wanavyo dhani,Mwalimu anaweza akapindisha Mtaala wa Elimu akafanya kinyume na Sera ya nchi kwa muda mfupi sana.Lakini watu hawaoni hayo." kilio cha walimu ni kurudishiwa Teaching allowance".