Monday, December 31, 2012

NAMSHUKURU MUNGU KWA KUNIWEKA ZALAMA MWAKA MZIMA WA 2012 KATIKA KUWASILIANA NA WENZANGU KUPITIA BLOG HII,PIA NAWASHUKURU NYOTE MLIYO TEMBELEA BLOG YA TUJIFUNZE KUSINI

 Hizo ni baadhi ya kazi nilizofanya mwaka 2012 namshukuru Mungu kwa kusafiri katika Kanda ya Kusini salama.




LEO SAA SITA USIKU ,WATU TULE,TUNYWE KWA FURAKA KATIKA KUAGA MWAKA 2012 NA KUKARIBISHA MWAKA 2013.

 Karibuni tunywe wote chai saa sita usiku,kuaga mwaka 2012 na kukaribisha mwaka mpya wa 2013
Usijali kikombe kimoja ,vitaongezwa vingine tukijumuika pamoja saa sita usiku leo

SENSA MWAKA 2012 TANZANIA ILITOA AJIRA KWA VIJANA ASEMA PINDA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mizengo Pinda pia mwenyekiti wa Kamati kuu ya Sensa Taifa,alisema Sensa ya mwaka 2012 imetia ajira ya muda kwa vijana ambao walikuwa  makarani wale wasiyo na kazi.
Aidha Mhe.Pinda alisema katika zoezi la Sensa ya mwaka huu watu wanne ( 4 ) walipoteza maisha na wengine walipata majeraha mbalimbali..
Mhe.Pinda alisema hayo siku ya uzinduzi wa matokeo ya Sensa ya awali katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam leo.Ambapo Rais Kikwete alizindua matokeo hayo.

WATANZANIA TUPO WATU 44,929,002,AMBAPO TANZANIA BARA 43,625,434 NA ZANZIBAR WATU 1,303,568 ATANGAZA RAIS KIKWETE

 Mhe.Dkt Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua Sensa ya watu na makazi Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam leo atangaza  Kuwa Tanzania ina watu 44,929,002.Tanzania Bara watu 43,625,434 na Zanzibar watu 1,303,568.
 Waziri wa Fedha Mhe, Wili
Mkamu wa Rais Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali akielezea mafanikio ya zoezi la Sensa mwaka 2012
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia mwenyekiti wa Sensa Taifa akielezea mafaniko ya sensa hiyo katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam leo.
 Mariam Kan Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa akielezea jinsi Tanzania ilivyofanikisha zoezi hilo kwa malengo ya kupanga bajeti  kwa maendeleo ya nchi.
Msomaji wa Utenzi Bi Amina Haji kutoka Zanzibar katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam Leo.


RAIS  KIKWETE  ATANGAZA MATOKEO YA AWALI YA SENSA YA WATU NA MAKAZI  KUWA TANZANIA INA WATU 44,929,002 KATIKA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA LEO, TAREHE 31 DESEMBA 2012 DAR ES SALAAM

RAIS Kikwete alisema kuwa uzinduzi huu wa awali siyo kuwa kuna matokeo mengine la bali yamekamilika isipokuwa mwezi Februari 2013 kutakuwepo na matokeo ya idadi ya watu kijinsia.kujua wanaume ni wanagapi na wanawake ni wangapi.
Alisema kuwa katika matokeo hayo,Tanzania Bara kuna indadi ya watu  43,625,434 na Zanzibar kuna watu 1,303,568.
Aidha alisema pamoja na changamoto kadhaa zilizojitokeza lakini zoezi hilo limefanikiwa kwa asilia 90.
Baadhi ya changamoto hizo ni pamoja na maandamano wakati wa zoezi liliendelea,watu kujifungia ndani kwa kukataa kuhesabiwa.
Alisema matokeo ya idadi ya watu imeonyesha jinsi watu wanavyoongezeka, na kwamba mwaka 2016 idadi ya Watanzania itakuwa 51,600,000,hivyo ni mzigo mkubwa kwa Taifa na Serikali pia na jamii kwa ujumla.Hivyo serikali itapanga mipango yake ya maendeleo ili kukabiliana na idadi kubwa ya watu,lakini pia watanzania wafuate uzazi wa mpango kwa lengo la kuzaa watoto ambao wataweza kuwahudumia.

Saturday, December 29, 2012

NAWATAKIENI HERI ,MAFANIKIO,AMANI,UPENDO NA MATUMAINI KWA MWAKA 2013

 Naomba wasomaji wa Blogs waendelee kusoma Blogs mwaka mpya wa 2013 kama walivyosoma mwaka uliyopita wa 2012.Tumshukuru Mungu kwa kutulinda hadi kufikia mwaka mwingine,hasa kwa kushiriki katika sikukuu ya X mas,ambapo kuna watu hawakufanikiwa kushiriki siku hiyo ingawa walitamani sana.
Nikiwa katika Blog yangu nikiwatakia wasomaji wangu ,heri ya Mwaka mpya wa 2013,Asanteni sana,Tuombeane maisha mema na marefu.

KARIBU MWAKA 2013,KWAHERI ANOLOJIA,KARIBU DIJITALI

Wakati watu anajiandaa kuupokea mwaka 2013,Pia watu anajiandaa katika matumizi ya Dijitali,baada ya kufunga kwa  matumizi ya Anolojia
Katika Manispaa ya Dodoma mistari mirefu nimekuwa ikionekana katika maduka ya STAR TIMES kununua Ving'amuzi kwa kuhofu ya  kumalizika kwa vifaa hivyo katika maduka hayo.
Hiyo ni dalili nzuri kuwa watu sasa kuwa  wanakwenda sambamba na matumizi ya Teknolojia ya kisasa katika matumizi ya mitandao mbalimbali kulingana na mabadiliko ya matumizi ya mitanadao mbalimbali inayo buniwa kila kukicha.

Sunday, December 23, 2012

NYAISONGA AWAPA MAADILI YA KIDINI WATOTO WA KIPEMARA DODOMA

 Baba Askofu Grevasi Nyaisonga wa Jimbo la Dodoma akitoa mahubiri kwenye maazimisho ya misa Takatifu ya Kipeimara katika Parokia Ya Mt Kalori Lwanga ya Makole Katika Manispaa ya Dodoma.
 Baadhi ya watoto waliyopata Kipeimara leo katika Parokia ya Makole leo.
 Waumini waliohudhuria ibada hiyo ya Kipeimara leo
Ni kwa ya Mtakatifu Kalori Lwanga ya Makole ikiinjisha kwa nyimbo katika ibada iliyofanyika leo Parokiani hapo.
 Askofu akitoa Kipeimara kwa kumweka Ishara ya Msalaba kwa mafuta na kofi shavuni .
 Wakiwa katika mageuzi ya mkate na divai
 Akionyesha kikombe cha divai kama ishara ya Damu ya Yesu,iliyo mwangika kwa ajili ya wengi kwa maondoleo ya dhambi
a
 Askofu Nyaisonga akimpa mkono mmoja wa waumini waliyo hudhuria misa hiyo leo.
Askofu Nyaisonga akitoa Baraka kwa waumini kanisani humo baasa ya Ibada hiyo hivi leo.


WATAKIWA KUISHI KWA IMANI KWA KUYASHINDA MAGUMU KATIKA MAISHA WATOTO WA KIPEIMARA DODOMA

ASKOFU wa Jimbo la Dodoma Mhashamu Grevasi Nyaisonga ,amewataka watoto waliopata Kimeimara wawe mashaidi wa Yesu Kristo kwa vitendo kwa ndani na nje,hasa katika kufuata imani ya kweli ya upendo  mbele za Mungu na watu  wote.
Baba Askofu Nyaisonga alisema kuwa kipemara kimewapa nguvu ya kuyashinda magumu katika maisha yao kwa mapenzi ya Mungu na kuwafanya askari imara wa Mungu kwa kuwa mashuhuda wa Yesu Kristo.
Askofu Nyaisonga ametoa Kipeimara kwa watoto 300 katika Parokia ya Mtakatifu Karoli Lwanga ya Makole katika Manispaa ya Dodoma Mkoa wa Dodoma Leo.
Aidha amesema kuwa katika kuchangia kwaya ya Mt.Kalori Lwanga ya Makole,waumini wanunue kanda zao zenye nyimbi za Unjilishaji za VIDEO,Pia wanunue na Kalenda ambazo zinaweza kuingizia Parokia mapato yake.
Wakati huohuo Mwenyekiti wa Parokia hiyo Bwana Evarist Mnaranara  amemshukuru Baba Askofu kwa kuwapa Kipeimara watoto hao,amewashukuru,Makatekista, na wazazi kwa kuwaandaa watoto hao katika mafundisho ya dini hadi kufikia kupata kipemara hicho.
Pia alisema pamoja na msimu wa mvua ,watu wafanye kazi kwa juhudi kubwa,na wakulima waende shamba maana msimu wa kilimo umeshaanza,kwa kufanya hivyo kutapatikana chakula cha kustosha kwa ajili ya familia zao.

Saturday, December 22, 2012

MINAZI NA FAIDA ZAKE KWA WAKULIMA WA ZAO HILO

 Mnazi ni zao ambalo linampa mkulima faida nyingi,Nazi kama kiungio cha mboga lakini pia kuna kilevi kiitwacho tembo,' Waswahili wana msemo usemao kukimsifia mgema Tembo hulitia maji' , dafu ni nazi ambayo haijakomaa ambayo ni laini na ina maji ya madafu,kifuu cha  nazi hutumika kama kuni,pia hutumika kwa kutengeneza mapambo.
Aidha kifuu hicho hicho hutumika kama chombo cha kuchotea maji, uji kwa jina jingine huitwa upawa,lakini machicha ya nazi hiyohiyo hutumika kama kashata.Nazi ikipelekwa kiwandani yanapatikana mafuta ya nazi ambayo ni mafuta ya nywele.
Matumizi mengine yatokanayo na zao la mnazi ni majani ya mnazi ambayo hutumika kama:-
  • Chelewa kwa fanyia usafi Mifagio
  • Chelewa hutumika kama mitego ya kutegea samaki ( migono ).
  • Majani ya minazi hujulikana kama makuti,makuti hayo hutumika kuezekea nyumba, kujengea ua wa kuoga na pia hutumika kwa kusukwa kwa ajili ya kuchukulia maembe, nazi , na vitu vingine.
  • Mti wa mnazi hutumika kwa ajili ya ujenzi wa nyumba wengine hupasua mbao na kuzifanya boriti za kuezekea nyumba.
  • Nazi inapo fuliwa yale yanayotolewa ili nazi ibakie kuwa nazi kwa ajili ya matumizi,hutumika kama kuni, na matuimizi mengine ambayo wakulima hao wanajua.
Hiyo ni minazi ya siku nyingi ambayo ni mirefu.Lakini kwa sasa kuna minazi ya muda mfupi inavunwa,inasemekana ina shambuliwa na maradhi,na nimifupi.
Hawa ni wakazi wa Pwani ya Lindi,ambao zao lao la biashara ni mnazi.

MIKOKO NA MIMEA IOTAYO PEMBENI MWA BAHARI NI FAHARI KWA VIUMBE VYA BAHARINI,HIVYO WAKAZI WA MWAMBAO MWA BAHARI AITUNZE KUHIFADHI MAZINGIRA YAKE

Mazingira mazuri yanayovutia ya mikoko katika Bahari ya Hindi, unapoingia mkoani Lindi, utakutana na mikoko hiyo ambayo ni masikani ya viumbe vyote viishivyo Baharini.
Wananchi waishio mwambao mwa bahari hiyo ni juu yao kuhifadhi mazingira ya kandokando mwa baharihiyo ili sura ya bahari iendelee kuvutia.

Friday, December 21, 2012

MATUMIZI YA MAJI YAWE SAFI NA SALAMA JE KWA WATUMIAJI WA MAJI HAYA UNAMAONI GANI?

 Je unasemaje kuhusu matumizi ya maji haya ni safi na salama ?, mito maji yake ni kama hivyo wengine wanaoga na kufua juu na nyie huku chini mnayachota kwa matumizi ya kunywa,je ni salama ?
Maji yanakawaida ya kusomba kila kitu,kwa hiyo watumiaji hao wanaoga mchanganyiko huo,na kuyanywa kawa mtindo huohuo.

TUJIFUNZE BLOG IMETOKANA NA JINA LA GAZETI LA KUSINI LA TUJIFUNZE TOLEO Na.6 LA OKTOBA - DASEMBA 2012

 Hilo ni toleo Na.6 la Oktoba - Desmba 2012 la TUJIFUNZE,Ambapo lead ni Kilio cha wakulima wa korosho nchini  kilio chao kimesikika - asema katibu Mkuu wa CCM Mhe.Abdulrahamn Kinana Mtwara.
Wakati  sub lead Dr.Huvisa atoa msaada wa vifaa tiba kwa hospitali za mkoa na wilaya, Mkoani Ruvuma.Front page.
Upande wa Mafunzo maalumu ,Makumbusho ya Majimaji ni kivutio kwa watalii,Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii Bi.Maimuna Tarishi.Ambapo upande wa michezo Timu ya majimaji wafunguka kwa maandalizi ya kurejea Vodacom msimu ujao.

UPANUZI WA BARABARA JIJINI DAR ES SALAAM WAENDA SAMBAMBA NA UJENZI WA DARAJA LA JUU KIMALA KAMA LILE LA MANZESE

 Hilo ni daraja la juu  la Kimara Jijini Dar es Salaam kama lilivyo la Manzese,ikiwa ni upanuzi wa Barabara za Jijini Dar es Salaam ili kupunguza msongamano wa magari jijini humo.Ni juhudi za serikali za kuboresha miundombinu ya barabara zake nchini.
Ni nguzo za daraja hilo ambazo bado kuweka daraja hilo.

Merry Christmas and new year of 2013 for all Blogger readers

 Happy with Merry Xmas cards and coming of new year of 2013 together.



WASICHANA WA FANYA MAAJABU KATIKA MATOKEO YA DARASA LA SABA MWAKA 2012 KWA ASILIMIA 8.8 KWA KUWAPIKU WAVULANA




WAZIRI wa  Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe.Dkt Shukuru Kawambwa  ametangaza matokeo ya darasa la saba mwaka 2012 ofisni kwake kwa waandishi wa habari na kusema wasichana wamefanya vizuri kuliko wavulana kwa asilimia 8.8,baada ya kuongoza kwa asilimia 50.20 kwa kuwapita wavulana kwa asilimia 49.80.
   Waziri huyo alisema kuwa wanafunzi 560,706 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule za serikali,na kati yao wanafunzi 281,460 ni wasichana na 279,246 wavulana ambapo imefanya idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kuongezeka kwa asilimia 8.8, ikilinganishwa na wanafunzi 515,187 ya waliyochaguliwa mwaka uliyopita.
  Mhe. Kawambwa alisema mtihani wa mwaka huu umefanyika kwa mara ya kwanza kwa kutumia Teknolojia mpya ya ‘ optical mark reader’ ambao usahihishaji wake hutumia compyuta,njia ambayo imeipunguzia serikali gharama ikilinganishwa na mwaka jana.
   Alisema kuwa mwaka jana walimu 4,000 walitumika kusahihisha zaidi ya mwezi mmoja,ambapo mwaka huu 285 ndiyo walitumika kwa siku 15 kukamilisha kazi yote.
     Kuhusu matokeo hayo amesema kuwa alama ya juu kabisa ni 234 kati ya 250 kwa wavulana na wasichana, ambapo wanafunzi 3,087 wamepata alama daraja la ‘A’ na wanafunzi 40,683 alama daraja la ‘B’,wanafunzi 222,103 alama daraja la ‘C’ na wanafunzi 526,397 alama daraja ‘D’ ambapo waliobakia 73,264 alama daraja ‘E’
   Aidha alisema vitendo vya udaganyifu vimepungua kutoka wanafunzi 9,736 waliofutiwa matokeo yao mwaka jana ikilinganishwa na wanafunzi 293 waliofutiwa matokeo yao mwaka huu.

Monday, December 17, 2012

WAKUU WA VITUO VYA KANDA SABA ZA MAGAZETI YA KISOMO WAMETAKIWA KUSIMAMA NA KUJENGA USHIRIKIANO KATIKA UTENDAJI KAZI ZAO

 Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima na Nje ya Mfumo Rasmi Bwana Salumu Mnjagila akiwasomea vipengere vya fomu za PRAS   Wahariri wa Magazeti vijijini wa Kanda saba katika ofisi yake  Mkao Makuu ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Jijini Dar es Salaam jana.
 Baadhi ya washiriki katika kikao hicho cha kazi wakimsikiliza Mkurugenzi kwa makini
 Naibu Mkurugenzi Kisomo Mwanza Bibi Mary Joseph Salu
 Picha ya Pamoja ya viongozi wa Idara ya Elimu ya Watu Wazima na Nje ya Mfumo Rasmi na  Baadhi ya wahariri wa magazeti vjijini
 Mkurugenzi Msaidizi Utawala Bw.Gange akitoa mada ya OPRAS kwa Wahariri wa Vituo vya uchapaji




WAKUU  wa vituo wa Kanda  saba  za magazeti ya kisomo  nchini,wametakiwa kusimama kwa ushirikiano na mshikamano wao katika ufanisi wa kazi zao za kuelimisha wananchi kupitia magazeti yao ya kisomo yanayo chapwa katika Kanda zao.
     Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima na Nje ya Mfumo Rasmi EWW/ENMRA Bwana salumu Mnjagila alisema hayo wakati wa kikao cha kazi kilicho fanyika ofisni kwake leo Makao makuu ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi JIjini Dar es Salaam.
     Bw.Mnjagila alisema kila mmoja atambue nafasi yake kituoni ili kuleta ufanisi wa kazi bila ya kusababisha migongano baina ya viongozi na watumishi katika vituo hivyo.
Aidha alisema vituo hivyo vitafanya kazi za maendeleo ya kuboresha  elimu nchini iwapo watafanya kazi kwa kuelewana  na kuwa wawazi katika maamuzi ya utekelezaji wa majukumu waliyo jipangia.
     Kikao hicho kilijumuishi Msaidizi Utawala Bwana Gange na Mkurugenzi Msaidizi Ufuatiliaji wa Taaluma Bibi Revilla na Wahariri  wa Vituo vya Uchapaji Magazeti Vijijini vya Mwanza,Tabora,Mbeya na Songea, ambao pia ni wakuu wa vituo hivyo.


Sunday, December 2, 2012

WAZAZI WATAKIWA KUWAPELEKA WATOTO WAO WADOGO SHULE ZA AWALI


Meya wa Manispaa ya Songea  Mstaiki Charles Mhagama amewataka wananchi na wazazi wa Manispaa yake kuwapeleka watoto wao wadogo kwenye shule za Awali ,ili wajengeke na msingi mzuri wa kujifunza.
Meya Mhagama alisema hayo katika mahafari ya shule ya Awali Charity iliyoko katika Uwanja wa sabasaba Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma jana,na kwamba katika harambee iliyofanyika katika mahafali hayo,Mstahiki Meya Mhagama aliahidi kutoa malori mawili ya mchanga yenye thamani ya shilingi laki tatu ( 300,000/= ),ambapo Yusufu Kufakunoga,kwa niaba ya Mhariri kanda ya kusini aliahidi kuchangia mifuko mitatu ( 3 ) ya sementi,Mtangazaji wa Star TV Songea Bwana Adam Nindi aliahidi kuchangia Shilingi 20,000/=.
Watoto 13 wamehitimu mafunzo ya Awali,ambapo mwakani watoto hao wataingia darasa la kwanza.Katika picha,wakwanza mwenye suti ya bluu ni mwalimu mkuu,pia ni mkurugenzi wa shule hiyo anayemfuatia mwenye kaunda suti mikono mifupi na Mstahiki Meya Charles Mhagama akimkabidhi cheti mmoja wa wahitimu.