Tuesday, March 20, 2012

UZINDUZI WA MWAKA WA USHIRIKA DUNIANI MGENI RASMI JAKAYA KIKWETE MNAZI MMOJA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete awambia wana ushirika kuwa waache tabia mbaya ya kuyauza majengo yao kwa bei za hasara,alisema hayo siku ya uzinduzi wa mwaka wa vyama vya Ushirika Duniani uliofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam leo,akiwa mgeni rasmi.
Kauli mbiu ya Vyama Vya Ushirika Duniani  mwaka huu ni Ushirika hujenga Dunia iliyo Bora.Aidha Dkt Kikwete alisema ,vyama vya Ushirika vielekeze nguvu zao kwenye ubanguaji wa korosho,kwa kuwa soko la korosho iliyobanguliwa ni la wazi,kuliko korosho ya maganda katika soko la dunia.

No comments:

Post a Comment