Saturday, March 10, 2012

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI MKUU WA MKOA WA RUVUMA MHE.SAID THABIT MWAMBUNGU AMEWAELEZA WANANCHI TAARIFA YA KAMATI YA KUCHUNGUZA VURUGU ILIYOTOKEA TAREHE 22 FEBRUARI MWAKA HUU MJINI SONGEA.

 Mhe.Mwambungu amesema kamati ya watu 8 aliyoiunda ikiongozwa na Injinia Tossi kufuatia vurugu zilizotokea tarehe 22 mwezi Februari 2012 katika manispaa ya Songea na kupelekea watu watatu kupoteza maisha wakiwemo watu wawili aliyouawa kwa risasi na mmoja kwa ajali ya pikipiki kutokana na vurugu hiyo,wamebaini mambo kadhaa.
Kamati hiyo imebaina mambo ya kiutawala na mambo ya kisheria yatafanyika kutokana na vurugu zile,na kwamba katika mambo ya kiutawala juhudi zimeshachukuliwa za ulinzi shirikishi na polisi jamii kulinda katika mitaa ili kuahakikisha usalama unakuwepo.
Aidha Mkuu wa mkoa huyo amewashukuru wananchi wa mkoa huo ,kwa ushirikiano wao na uongozi wa wilaya na mkoa katika kurejesha hali ya amanai na utulivu katika Manispaa ya Songea na Mkoa kwa ujumla wake.Na pia kawashukuru waandishi wa habari kwa kusidia kuwaelimisha wananchi mambo mengi ya maendeleo na usalama kama lile lililotokea Februari mwaka huu.
Alisema wananchi wawe na amani kwani amani imepatikana,kutokana na ulinzi shirikishi wa sungusungu na polisi kwa ushirikiano wa wananchi wenyewe, unaenda vizuri,amewataka wawe na amani wafanye shughuli zao za shamba bila wasiwasi.
 Bwana Nyumayo na baadhi ya waandishi wakimsikiliza mkuu wa mkoa kwa makini.
 Baadhi ya waandishi wa habari ofisini kwa mkuu wa mkoa wakisiliza taarifa hiyo leo mjini Songea
 Afisa habari wa mkoa wa Ruvuma Bwana Revocatus akiwa makini katika kufuatilia taarifa akiwa na waandishi wa habari wa Mkoa wake katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa leo.
Mwandishi wa habari mpigapisha maarufu Bwana Mhidini Ndolanga alikuwa miongoni mwa waandishi wa habari leo.

No comments:

Post a Comment