Mheshimiwa Mkuu Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu akitoa taarifa ya kamati aliyoiunda kuchunguza vurugu zilizotokea tarehe 22 mwezi Februaru mwaka huu katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma kwa waandishiwa wa habari jana ofisini kwake.
Baadhi ya waandishi wa habari nikiwemo pamoja nao tukifuatilia taarifa hiyo hapo jana ya mkuu wa mkoa wa Ruvuma.
baadhi ya viongozi wa mkoa na Mkuu wa wilaya ya Songea Ole Thomas Sabaya na waandishi wa habari katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Ruvuma wakisikilizataarifa ya kamati hiyo.
Baadhi ya waandishi wa habari nikiwemo pamoja nao tukifuatilia taarifa hiyo hapo jana ya mkuu wa mkoa wa Ruvuma.
baadhi ya viongozi wa mkoa na Mkuu wa wilaya ya Songea Ole Thomas Sabaya na waandishi wa habari katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Ruvuma wakisikilizataarifa ya kamati hiyo.
KAMATI
iliyoiundwa kwa mazumuni ya kuangalia vurugu zilizotokea na kuleta mataizo
makubwa, tarehe 22 februari mwaka huu na
kupelekea watu watatu walipoteza maisha yao wakiwemo wawili kwa kupigwa na
risasi na mwingine kwa ajali ya pikipiki na wengine kadhaa kupata majeraha
ambao walipata matibabu na halizao zikawa
salama.Mkuu wa mkoa Mhe.Said Thabit Mwambungu amaipokea taarifa yao.
Mkuu
wa mkoa huyo aliunda Kamati ya watu 8 iliyoongozwa na Katibu Tawala msaidi
wa mkoa nayeshughulikia miundombinu Injinia
Tossi na wenzake maafisa waandamizi 7 kuangalia
chanzo cha vurugu ile kama ilikuwa vipi ili isije jirudia tena.
Alisema
nia ya serikali ni kusalifu kiundani chanzo cha vurugu ile ili serikali ifanye
kazi yake na pia wananchi waelewe kuwa serikali imepokea taarifa ile,na kubaini
mambo kadhaa, yakiwemo ya kiutawala na ya
kisheria.
Ambapo
mengine yameanza fanyiwa kazi kwa mujibu wa sheria.kwa kuwafikisha kunako
husika watuhumiwa waliyohusika na mauaji toka Mwezi Novema mwaka jana Na kesi
zao zipo katika hatua mbalimbali.
Alisema
na wale ambao walihusika na mauaji ya vijana wawili kwa risasi watafikishwa
kwenye vyombo vya sheria lili uchunguzi ufanyike na haki itendeke kwa mujibu wa
sheria.
Aliwaomba
wananchi waepukane kueneza uvumi ambao unaweza
kuzalisha maafa makubwa katika jamii na wanaposikia jambo au tetesi ya uhalifu
wapeleke taarifa kunako husika. kuliko kuchukua sheria mikononi.
Alisema
wananchi wamepata elimu ya kujilinda na kazi hiyo imeanza kwa ulinzi shirikishi
katika mitaa yote ya Mansipaa ya Songea.Baada ya wananchi kuelewa umuhimu wa
kujilinda,.na kuwa na tabia ya kufikisha malalamiko yao kunako husika kwa njia
ya halali na ya amani kwenye vyombo vya
sheria. Na kwamba sungusungu wametakiwa
kufanya kazi yao
kwa kufuata sheria na wanapompata mhalifu wasichukue sheria mikononi wamfikishe
kwenye usalama.
Pia Mhe.Mwambungu aliwashukuru wananchi na waandishi wa habari kwa ushirikiano wao
na serikali katika kuifanya manispaa ya songea kurejea katika hali ya usalama
na utulivu kwa muda mfupi sana.
Aidha
aliwataka wananchi wa nje ya mkoa huo kuwa hali ya utulivu na amani katika mkoa
wa Ruvuma na wilaya zake zipo kama mwanzo, ambapo wananchi wanafanya kazi zao
kama kawaida za kilimo na zauzalishaji mali.
No comments:
Post a Comment