Saturday, March 17, 2012

RUVUMA PRESS CLUB YAZINDUA KAMATI YA MAADILI,NIDHAMU NA USULUISHI LEO

 Kamati ya maadili,usuluhishi na nidhamu ya Press Club Ruvuma imezinduliwa leo Rasmi katika ukumbi wa SACCOS  ya walimu Vijijini katika Manispaa ya Songea,Awali Katibu Mtendajiwa Clabu hiyo Bwana Endrew Chatwanga kabla hajamkaribisha kaimu mwenyekiti Bawana Mosesi Konara alisema kamati hiyo itafanya shughuli zao kwa kufuata kanuni ya UTPC.Bw.Christian Sikapundwa wa kwanza akipokea katiba kutoka kwa Kaimu Mwenyekiti Bw.Konara.
  Naye makamu wa Mwenyekiti Bw.Mosesi Konara alisema zoeli hilo la uzinduzi wa kamati hiyo ni muhimu sana kwani utafungua ukurasa mpya ya Clabu hiyo kwa wanachama wake kufuata maadili na nidhamu ya kazi yao ili wawe mfano kwa clabu nyingine hapa nchini. Hati maye makamu wa mwenyekiti huyo aligawa Katiba ya Umoja wa waandishiwa wa habari Ruvuma.

 Mjumbe wa kamati ya Maadili Bibi Catherine Nyoni akipokea Kitabu cha Katiba ya Ruvuma Press kutoka kwa kaimu wa mwenyekiti wa Press clabu Bw.Konara.
Katibu Mtendaji wa Clabu hiyo Bw.Endrew Chatwanga kushoto na makamu wa Mwenyekiti Bw.Moses Konara baada ya uzinduzi wakiteta jambo.
Kamati hiyo ya Maadili,Nidhamu na Usuluhishi yenye wajumbe 6 Mwenyekiti wao ni Bw.Christian Sikapundwa,Zakaria NgalimanayoMjumbe na ni Katibu wa muda,Judith Mwenda Mjumbe,Revocaus Massimba Mjumbe,Catherine Nyoni Mjumbe na Augustino Mbunda mjumbe.wambao watadumu kwa muda wa miaka mitatu.

No comments:

Post a Comment