Saturday, March 24, 2012

UMOJA WA WAANDISHI WA HABARI RUVUMA UMEPATA UONGOZI WA KUDUMU • Endrew Kuchonjoma Mwenyekiti. • Leticia Nyoni Makamu Mwenyekiti • Enderw Chatwanga Katibu Mtendaji • Julis Moses Konara Makamu katibu Mtendaji

 Anayezungumza ni mwenyekiti aliyechaguliwa Bw.Endrew Kuchonjoma na wa kwanza ni Makamu mwenyekiti Bi Leticia Nyoni
 Katibu Mtendaji wa Press aliyechaguliwa Bw.Endrew Chatwanga
 Katibu na kamati tendaji ya Press
 Afisa tawala Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Songea Bw. Richardi Mbambe msimamizi wa uchaguli huo leo Ukumbi wa Emau Peramiho
 Wajumbe na baadhi ya viongozi
Bw.Mbambe anawakabidhi rasmii viongozi wa kudumu kwa miaka mitatu ijayo.

Tuesday, March 20, 2012

UZINDUZI WA MWAKA WA USHIRIKA DUNIANI MGENI RASMI JAKAYA KIKWETE MNAZI MMOJA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete awambia wana ushirika kuwa waache tabia mbaya ya kuyauza majengo yao kwa bei za hasara,alisema hayo siku ya uzinduzi wa mwaka wa vyama vya Ushirika Duniani uliofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam leo,akiwa mgeni rasmi.
Kauli mbiu ya Vyama Vya Ushirika Duniani  mwaka huu ni Ushirika hujenga Dunia iliyo Bora.Aidha Dkt Kikwete alisema ,vyama vya Ushirika vielekeze nguvu zao kwenye ubanguaji wa korosho,kwa kuwa soko la korosho iliyobanguliwa ni la wazi,kuliko korosho ya maganda katika soko la dunia.

Saturday, March 17, 2012

RUVUMA PRESS CLUB YAZINDUA KAMATI YA MAADILI,NIDHAMU NA USULUISHI LEO

 Kamati ya maadili,usuluhishi na nidhamu ya Press Club Ruvuma imezinduliwa leo Rasmi katika ukumbi wa SACCOS  ya walimu Vijijini katika Manispaa ya Songea,Awali Katibu Mtendajiwa Clabu hiyo Bwana Endrew Chatwanga kabla hajamkaribisha kaimu mwenyekiti Bawana Mosesi Konara alisema kamati hiyo itafanya shughuli zao kwa kufuata kanuni ya UTPC.Bw.Christian Sikapundwa wa kwanza akipokea katiba kutoka kwa Kaimu Mwenyekiti Bw.Konara.
  Naye makamu wa Mwenyekiti Bw.Mosesi Konara alisema zoeli hilo la uzinduzi wa kamati hiyo ni muhimu sana kwani utafungua ukurasa mpya ya Clabu hiyo kwa wanachama wake kufuata maadili na nidhamu ya kazi yao ili wawe mfano kwa clabu nyingine hapa nchini. Hati maye makamu wa mwenyekiti huyo aligawa Katiba ya Umoja wa waandishiwa wa habari Ruvuma.

 Mjumbe wa kamati ya Maadili Bibi Catherine Nyoni akipokea Kitabu cha Katiba ya Ruvuma Press kutoka kwa kaimu wa mwenyekiti wa Press clabu Bw.Konara.
Katibu Mtendaji wa Clabu hiyo Bw.Endrew Chatwanga kushoto na makamu wa Mwenyekiti Bw.Moses Konara baada ya uzinduzi wakiteta jambo.
Kamati hiyo ya Maadili,Nidhamu na Usuluhishi yenye wajumbe 6 Mwenyekiti wao ni Bw.Christian Sikapundwa,Zakaria NgalimanayoMjumbe na ni Katibu wa muda,Judith Mwenda Mjumbe,Revocaus Massimba Mjumbe,Catherine Nyoni Mjumbe na Augustino Mbunda mjumbe.wambao watadumu kwa muda wa miaka mitatu.

Tuesday, March 13, 2012

CCM WAZINDUA KAMPENI YA UDIWANI LEO KATA YA LIZABONI MANISPAA YA SONGEA KUZIBA NAFASI YA MAREHE MU ALLY MAYA

Wakati Chama Cha Mapinduzi CCM wanazindua kampeni ya Udiwani Katika  Kata ya Lizaboni Manispaa ya Songea Mkoa wa Ruvuma leo,kufuatia aliyekuwa Diwani kupitia Chama hicho kufariki mwaka jana na kuacha nafasi hiyo wazi,Wenzao wa Chama Cha Chadema wao walizindua  kampeni hiyo siku tatu zilizo pita.

Monday, March 12, 2012

USAFIRISHAJI WA MAHINDI KUTOKA GHALA LA CHAKULA LA TAIFA RUHUWIKO SONGEA RUVUMA KUPELEKA NJE YA MKOA BADO UNAENDELEA.

 Lori hilo ninashehena ya magunia ya mahindi kutoka katika ghala la taifa la chakula Ruhuwiko Songea hapo liko eneo la Lizaboni Manispaa ya Songea likielekea Barabara Songea Dar es Salaam.
Lori hilo lipo maeneo ya Stand kuu ya Songea likiingia kwenye shell ya Kisumapai kuweka mafuta ili aendelee na safari yake.Usafirishaji wa chakula kwa malori ni mzuri ila unachukua muda mrefu,iwapo kungekuwa na usafirishaji wa gari moshi. shehena iyolundikana kule ghalani ingekuwa karibu wanaimaliza.

Saturday, March 10, 2012

KAMATI YA KUCHUNGUZA VURUGU ZILIZOTOKEA TAREHE 22 FEBRUARI 2012 ILIYOUNDWA NA MKUU WA MKOA IMETOA TAARIFA YAKE RASMI JANA

 Mheshimiwa Mkuu  Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu akitoa taarifa ya kamati aliyoiunda kuchunguza vurugu zilizotokea tarehe 22 mwezi Februaru mwaka huu katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma kwa waandishiwa wa habari jana ofisini kwake.
 Baadhi ya waandishi wa habari nikiwemo pamoja nao tukifuatilia taarifa hiyo hapo jana ya mkuu wa mkoa wa Ruvuma.
baadhi ya viongozi wa mkoa na Mkuu wa wilaya ya Songea Ole Thomas Sabaya na waandishi wa habari katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Ruvuma wakisikilizataarifa ya kamati hiyo.


KAMATI iliyoiundwa kwa mazumuni ya kuangalia vurugu zilizotokea na kuleta mataizo makubwa,  tarehe 22 februari mwaka huu na kupelekea watu watatu walipoteza maisha yao wakiwemo wawili kwa kupigwa na risasi na mwingine kwa ajali ya pikipiki na wengine kadhaa kupata majeraha ambao walipata matibabu na halizao zikawa  salama.Mkuu wa mkoa Mhe.Said Thabit Mwambungu amaipokea taarifa yao.

Mkuu wa mkoa huyo aliunda  Kamati  ya watu 8 iliyoongozwa na Katibu Tawala msaidi wa mkoa  nayeshughulikia miundombinu Injinia Tossi na wenzake maafisa waandamizi  7 kuangalia chanzo cha vurugu ile kama ilikuwa vipi ili isije jirudia tena.

Alisema nia ya serikali ni kusalifu kiundani chanzo cha vurugu ile ili serikali ifanye kazi yake na pia wananchi waelewe kuwa serikali imepokea taarifa ile,na kubaini mambo kadhaa, yakiwemo ya  kiutawala   na  ya kisheria.

Ambapo mengine yameanza fanyiwa kazi kwa mujibu wa sheria.kwa kuwafikisha kunako husika watuhumiwa waliyohusika na mauaji toka Mwezi Novema mwaka jana Na kesi zao zipo katika hatua mbalimbali.

Alisema na wale ambao walihusika na mauaji ya vijana wawili kwa risasi watafikishwa kwenye vyombo vya sheria lili uchunguzi ufanyike na haki itendeke kwa mujibu wa sheria.

Aliwaomba wananchi waepukane kueneza  uvumi ambao unaweza kuzalisha maafa makubwa katika jamii na wanaposikia jambo au tetesi ya uhalifu wapeleke taarifa kunako husika. kuliko kuchukua sheria mikononi.

Alisema wananchi wamepata elimu ya kujilinda na kazi hiyo imeanza kwa ulinzi shirikishi katika mitaa yote ya Mansipaa ya Songea.Baada ya wananchi kuelewa umuhimu wa kujilinda,.na kuwa na tabia ya kufikisha malalamiko yao kunako husika kwa njia ya halali  na ya amani kwenye vyombo vya sheria.  Na kwamba sungusungu wametakiwa kufanya kazi yao kwa kufuata sheria na wanapompata mhalifu wasichukue sheria mikononi wamfikishe kwenye usalama.

Pia Mhe.Mwambungu aliwashukuru wananchi na waandishi wa habari kwa ushirikiano wao na serikali katika kuifanya manispaa ya songea kurejea katika hali ya usalama na utulivu kwa muda mfupi sana.

Aidha aliwataka wananchi wa nje ya mkoa huo kuwa hali ya utulivu na amani katika mkoa wa Ruvuma na wilaya zake zipo kama mwanzo, ambapo wananchi wanafanya kazi zao kama kawaida za kilimo na zauzalishaji mali.

                                                                                                                                

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI MKUU WA MKOA WA RUVUMA MHE.SAID THABIT MWAMBUNGU AMEWAELEZA WANANCHI TAARIFA YA KAMATI YA KUCHUNGUZA VURUGU ILIYOTOKEA TAREHE 22 FEBRUARI MWAKA HUU MJINI SONGEA.

 Mhe.Mwambungu amesema kamati ya watu 8 aliyoiunda ikiongozwa na Injinia Tossi kufuatia vurugu zilizotokea tarehe 22 mwezi Februari 2012 katika manispaa ya Songea na kupelekea watu watatu kupoteza maisha wakiwemo watu wawili aliyouawa kwa risasi na mmoja kwa ajali ya pikipiki kutokana na vurugu hiyo,wamebaini mambo kadhaa.
Kamati hiyo imebaina mambo ya kiutawala na mambo ya kisheria yatafanyika kutokana na vurugu zile,na kwamba katika mambo ya kiutawala juhudi zimeshachukuliwa za ulinzi shirikishi na polisi jamii kulinda katika mitaa ili kuahakikisha usalama unakuwepo.
Aidha Mkuu wa mkoa huyo amewashukuru wananchi wa mkoa huo ,kwa ushirikiano wao na uongozi wa wilaya na mkoa katika kurejesha hali ya amanai na utulivu katika Manispaa ya Songea na Mkoa kwa ujumla wake.Na pia kawashukuru waandishi wa habari kwa kusidia kuwaelimisha wananchi mambo mengi ya maendeleo na usalama kama lile lililotokea Februari mwaka huu.
Alisema wananchi wawe na amani kwani amani imepatikana,kutokana na ulinzi shirikishi wa sungusungu na polisi kwa ushirikiano wa wananchi wenyewe, unaenda vizuri,amewataka wawe na amani wafanye shughuli zao za shamba bila wasiwasi.
 Bwana Nyumayo na baadhi ya waandishi wakimsikiliza mkuu wa mkoa kwa makini.
 Baadhi ya waandishi wa habari ofisini kwa mkuu wa mkoa wakisiliza taarifa hiyo leo mjini Songea
 Afisa habari wa mkoa wa Ruvuma Bwana Revocatus akiwa makini katika kufuatilia taarifa akiwa na waandishi wa habari wa Mkoa wake katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa leo.
Mwandishi wa habari mpigapisha maarufu Bwana Mhidini Ndolanga alikuwa miongoni mwa waandishi wa habari leo.

Thursday, March 8, 2012

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI LEO, NI SIKU MUHIMU SANA KWANI MWALIMU WA KWANZA KATIKA FAMILIA NI MWANAMKE KISHA NI MAMA KATIKA JAMII DUNIANI NANI KAMA MAMA

 Wanawake wa mkoa wa Ruvuma leo wameungana na wanawake wezao Duniani kuadhimisha siku yao leo ambayo kila mwaka inaadhimishwa Duniani,na kwamba Ushirikishwaji  wa wasichana katika maendeleo ni chachu ya  maendeleo.Wanawake hao wa mkoa wa Ruvuma  wanasema kuwa wao hawafungamani na chama chochote.
 Ni baadhi ya wanawake wakiwa katika makumbusho ya majimaji  mjini Songea siku ya kupinga ukatili wa kijinsia ,iliyofanyika mwaka jana.
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe.Said Thabit Mwambungu wamewaambia wanawake wa mkoa wa Ruvuma leo kushikamana katika vikundi vya uzalishaji mali na kujiunga katika SACCOS ili wasiwe tegemezi zaidi kutoka kwa wanaume katika Wilaya Mbinga Kijiji cha Mkako ambapo leo alikuwa mgeni rasmi.

Wednesday, March 7, 2012

SONGEA SASA SHWARI,ULINZI WA SUNGUSUNGU UMESHAMIRI AMANI NA UTULIVI VIMETAWALA

Agizo la Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mhe.Said Thabit Mwambungu la kuwa taka wananchi wa Manispaa ya Songea kushirikiana na Jeshi la polisi katika kuiweka Manispaa hiyo katika hali ya utulivu kwa wananchi wanaoishi katika Manispaa hiyo limefanikiwa kwani wananchi wanafanya shughuli zao na wanalala kwa amni..
Mhe. Mwambungu alitoa agizo hilo katika kikao kilichoitishwa na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya na Mkoa wakati wa wimbi la mauaji lilivyo ibuka katika Manispaa hiyo mwezi uliyopita ,na kusababisha wananchi kuandamana na kusababisha vurugu zilizo ondoa amani.
Hali ya utulivu imerejea kama awali,wananchi kupitia viongozi wao wa mitaa wanalinda katika mitaa yao,kuhakikisha usalama unakuwepo,wakitumia ulinzi shirikishi ( sungusungu ) kuna kila dalili ya kumpongeza mkuu huyo wa mkoa na uongozi wote wa wilaya na mkoa kwa pamoja kwa uamuzi walio uchukua.