Tuesday, September 16, 2014

FREEMAN MBOWE ASHINDA KWA KISHINDO NAFASI YA UWENYEKITI WA CHAMA CHA CHADEMA KATIKA MKUTANO MKUU WA CHAMA HICHO ,NA KUTOA TAMKO LA MGOMO USIO NA KIKOMO KWA TAIFA LOTE IWAPO BUNGE MAALUMU KA KATIBA LITAENDELEA KUJADILI RASIMU ZA KATIBA HIYO

Mheshimiwa Freeman Mbowe amepata ushindi wa kishindo kufuatia uchaguzi wa nafasi ya uenyekiti kwenye Chama chake cha CHADEMA katika mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika Jijijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Aidha baada ya uchaguzi huo Mhe. Mbowe alitoa tamko la maandamano yasiyo na kikomo kwa nchi nzima ,iwapo Bunge Maalumu la Katiba litaendelea kujadili Rasimu ya Katiba hiyo kwa madai kuwa kuendelea na mjadala wa Rasimu ya Katiba ni kuhujumu fedha za watanzania.

Wachambuzi wa mambo wasio wababaishaji wanahoji,Mhe.Mbowe alikuwa wapi kupinga Bunge hilo lisiendelee wakati lilipo anza akiwa Mjumbe wa Bunge hilo? mbona  na yeye alishapokea fedha hizo kwa nini asingezikataa maana kwa kufanya vile naye alikuwa mmoja wa wahujumu wa fedha hizo  za watanzania.

Wanafalsafa  wanajihoji,kulikoni  inawezekana,kuwa mtu anaweza kupoteza umaarufu wake bila ya kujielewa kwani wengi hupoteza umaarufu wao kwa kufanya vituko ambavyo jamii inavishangaa.kwa kufanya kitu kizuri katika wakati mbaya. 'Inaupasa tuwe na Demokrasia yenye nasaha ili nchi iendelee uwa na Amani,Utulivu,Upendo na Maelewano baina ya watawala na watawaliwa'

No comments:

Post a Comment